Baada ya kujua jinsi ya kuhesabu mzunguko wako kama nilivyoelezea kwenye part I nasikuu ya kushika ujauzito kama nilivyoelezea kwenye part II ya makala hii basi ni muda wa kujua kuwa je siku za hatari huwa zinakuwa zipo ngapi? Hii naamini itakusaidia sana wewe unaetaka kutumia karenda kama njia ya uzazi wa mpango. Kwanza kabisa napenda ujue kuwa yai mwanamke huwa linakaa kwenye mji wa uzazi kusubiri mbegu za mwanaume kwa masaa 24 tuu. Baada ya muda huo yai hutengeneza gamba gumu kulizunguka ambapo gamba hilo huzuia mbegu zisiweze kuingia ndani ya yai na kutunga ujauzito. Hivyo baada ya kujua siku ambayo yai litashuka kwenye mji wa uzazi kutoka kwenye ovari kama nilivyoelezea Part II, basi kama yai limeshuka leo basi litakaa leo na kesho tuuu kisha baada ya hapo ujauzito hautaweza kutungwa kwani yai linakuwa limekwishatengeneza gamba gumu na tayari linakuwa limeanza kuharibika taratibu kusubiri mzunguko ujao. Ila mbegu za mwanaume huwa zinaweza kuishi ndani ya via vya uzazi vya mwanamke mpaka masaa 72 kusubiri yai. Hivyo hata kama siku ya hatari (ovulation day) ilikuwa ni keshokutwa halafu wewe ukashiriki mapenzi leo basi unakuwa kwenye uwezekano mkubwa sana wa kupata ujauzito kwani siku ya hatari inavyofika bado mbegu za mwanaume zitakuwa zipo kwenye via vya uzazi kusubiri yai. Hivyo kwa kifupi siku za kubeba mimba zitakuwa ni siku mbili kabla ya siku ya hatari na siku moja baada ya siku ya hatari. Mfano, baada ya kuhesabu mzunguko wako tuseme umepata siku 27 kwa mfano, ukitoa 14 utapata 13 hivyo siku ya 13 tangu ulipoona hedhi ndo siku yako ya yai kushuka (ovulation day). Sasa siku za kubeba mimba zitakuwa siku mbili kabla ya 13 mpaka siku moja baada ya 13 hivyo jumla zitakuwa ni siku 4 yaani siku ya 11,12,13 na 14 tangu ulivyoona hedhi mara ya kwanza.
Endelea kufuatilia part 4 kujua jinsi ya kurekebisha mzunguko uliovurugika
TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku