Moja kati ya kitu ambacho kimekuwa kikiwasumbua wanawake wengi sana kwa sasa ni jinsi ya kujua mzunguko wao wa hedhi na jinsi ya kujua siku za kubeba ujauzito. Leo napenda kuelezea somo hili kwa kirefu na kwa njia rahisi ambayo mtu yeyote atakayesoma makala ataweza kuelewa, nafanya hivi kwani nimekuwa nikipigiwa simu nyingi sana na watu wanaoshindwa kujua mzunguko wao. Kwanza kabisa napenda kutoa maana ya neno 'mzunguko'. Watu wengi wamekuwa wakichanganya maana ya neno mzunguko na idadi ya siku wanazokuwa kwenye period. Unakuta unamuuliza mtu una mzunguko wa siku ngapi anakwambia siku 3 kumbe anamaanisha idadi ya siku anazokuwa anatokwa na hedhi. Sasa iko hivi, mzunguko ni idadi ya siku zilizopo kati ya period moja na period nyingine yaani ili uweze kujua una mzunguko wa siku ngapi unatakiwa uanze kuhesabu kuanzia siku ya kwanza uliyoona damu mpaka siku moja kabla ya siku utakayoona damu awamu nyingine. Kwamfano mwezi huu umeona damu tarehe 10 tuseme, kisha ukaja tena kuona damu tarehe 8 mwezi unaokuja basi utatakiwa kuhesabu kuanzia tarehe 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 01 02 03 04 05 06 07 hivyo ukihesabu hapo kwa umakini utaona zipo siku 29 basi huo ndo unakuwa mzunguko wako, maana yake kila baada ya siku 29 utakuwa unaingia period (unaanza mzunguko mpya). Niliotoa hapo ni mfano hivyo unaweza ukautumia kwa kulinganisha mzunguko wako ulivyo. Pia napenda kuelezea kitu kimoja, watu wengi wamekuwa wakiamini kuwa wanawake wote Duniani ni sawa kwamba wote wanamzunguko unaofanana, hapana. Mzunguko unatofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine wapo wenye mzunguko wa siku 21 wapo wenye mzunguko wa siku 23, 27, 30, 34 na hata wengine wanaenda mpaka siku 36 hivyo ili kujua kuwa unamzunguko wa siku ngapi unatakiwa kufuatilia walau kwa muda usiopungua miezi mitatu ili ujue kwamba kila baada ya siku ngapi ndiyo huwa unaingia period, ukishapata idadi ya siku hizo basi ndiyo mzunguko wako. (Usikariri tarehe ya kuingia period bali jua idadi ya siku kati ya period moja na period nyingine) kubadilika kwa tarehe ni kitu cha kawaida. Fuatilia part 2 ili kuelewa zaidi juu ya siku ya kubeba ujauzito.
TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku