Tatizo la kukosa choo kwa watoto au kuwa na choo kigumu hasa watoto wadogo limekuwa likiwasumbua wazazi wengi sana miaka ya hivi karibuni. Mara nyingi hali hii hujitokeza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kupewa maziwa ya kopo au pale mtoto anapoanza kula vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama. Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama pekee huwa hawasumbuliwi na tatizo hili. Leo napenda kuelezea baadhi ya vitu ambavyo unaweza kuvifanya hapo nyumbani na kumsaidia mtoto wako kuondokana na tatizo hilo.
1. Anza kumpatia mtoto wako maji safi, mpe walau kiasi kifo kwa siku kisha uendelee kumuongezea kiasi kadri siku zinavyosonga mbele.
2. Mpatie juisi ya tufaa (Apple) robo glass. Juisi hii huleta matokeo chanya kwa haraka zaidi.
3. Jitahidi kumpatia mwanao vyakula vyenye ufumwele (fiber). Kama mwanao amekwisha anza kula vyakula vigumu basi pendelea zaidi kumpa vyakula vyenye ufumwele kuliko vyakula vya wanga. Vyakula vyenye ufumwele kwa wingi ni kama vile apple, peas na papai. Epuka kumpa wali au uji wa mchele endapo mtoto anatatizo hili kwani utamuongezea tatizo zaidi.
Fuata maelekezo tajwa hapo juu na kwa uwezo wa Mungu tatizo la mwanao litakwisha kirahisi kabisa.
TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku