Kama umepita mitaani naamini utakuwa umeona mara kadhaa wanawake wakiweka pesa katika sidiria zao, Jambo hili limekuwa ni kawaida sana kwa wanawake wajasiriamali na wengi wao huona ni kitu cha kawaida kabisa kwani kimekuwa kikifanyika kwa miaka mingi. Huenda madhara take yasiweze kuonekana moja kwa moja lakini madhara yake huwa ni makubwa hasa endapo mwanamke huyu anaeweka pesa kwa mtindo huu anapokuwa ni mama aayenyonyesha. Kihalisi tabia ya kuweka pesa kwenye sidiria ni hatari sana kwa afya ya mtoto. Najua utakuwa unajiuliza kuwa ni hatari kivipi wakati imekwishazoeleka siku zote?
IKO HIVI:
Mara nyingi pesa tunayopokea kutoka kwa mtu huwa hatujui kuwa pesa hiyo imepitia mazingira gani huko ilikotoka na kila mmoja anajinsi ya kuhifadhi pesa anayoijua yeye kulingana na mazingira aliyopo. Kwa mfano, kuna watu wanafanya kazi buchani hivyo pesa zao hu wanavyozihifadhi lazima watashika na mikono yenye damu damu za nyama, wengine ni huhifadhi pesa soksi hasa hasa wanaume, wengine huweka pesa katika mazingira ambayo si salama sana kiafya. Hivyo kitendo cha kuchukua pesa na kuiweka kwenye sidiria ni hatari sana maana hapo ndipo mtoto anapopata chakula chake na ni wachache sana ambao huosha maziwa yao kabla ya kuanza kumnyonyesha mtoto hali inayopelekea mtoto kuanza kupata matatizo mbalimbali ya kiafya kama vile kuharisha, kutapika au hata kupata maradhi mbalimbali ambayo huenda usijue yametokea wapi. Hii siyo kwa wanawake wanaonyonyesha tuu bali Ni kwa wanawake wote kwani matiti nj kiungo sensitive sana katika mwili wa mwanamke na endapo utaruhusu vimelea vya maradhi kukaa kuzunguka eneo hilo basi huenda ikapelekea kupata matatizo mbalimbali ya kiafya ambayo huenda athari zake usizione hivi karibuni lakini muda utakaokuja kuona tatizo likawa kubwa zaidi hivyo ni vyema kujilinda mapema.
TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku