Je wewe ni mmoja kati ya watu wanaosumbuliwa au kukoseshwa amani na tatizo la kutoa harufu mbaya kwenye kwapa? Endapo unasumbuliwa na tatizo hilo basi amini ya kwamba hauko pekeyako mwenye tatizo hilo na huenda ukawa umekwisha hangaika kwa njia mbalimbali lakini bado hali hiyo inakusumbua. Basi napenda kukuhakikishia ya kwamba kupitia makala hii fupi utaweza kupata suluhisho la tatizo lako. Kwanza kabisa napenda nikwambie ya kwamba kihalisi au kiasili jasho ya binadamu haina harufu yoyote ile. Kinachopelekea harufu siyo jasho lenyewe bali backteria ambao wanapatikana eneo hilo. Kama tujuavyo ya kwamba backeria hupenda kuishi na kuzaliana hasa katika maeneo yenye unyevunyevu hivyo endapo mwili wako hukaa na jasho kwa muda mrefu bila kufutwa basi sehemu hiyo yenye jasho inakuwa ni rafiki kwa backteria. Hao backteria wanapozaliana eneo hilo hutengeneza uchafu (takamwili ya backeria) hivyo uchafu utokanao na backeria hao ndiyo hupelekea harufu ambayo mtu huuiskia. Kwa maana hiyo njia bora zaidi siyo kuzuia jasho kutoka bali kuzuia au kumaliza mazalia ya backeria katika eneo husika. Unaweza kufanya hivyo kwa kuoga au kusafisha maeneo yanayotoa harufu mbaya kwa kutumia sabuni zenye sifa ya kuua backeria (antibacterial soaps). Sambamba na kufanya hivyo unashauriwa kunywa maji mengi au kunywa maji mara kwa mara kwani maji yanasifa ya kufanya dilution kwenye urea ambayo inapatikana katika jasho na mkojo pia. Hivyo kunywa maji mengi kila siku huleta mafanikio makubwa zaidi kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo tajwa hapo juu.
TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku