Mchicha ni moja kati ya mboga maarufu sana kwa watu wengi. Huenda wengi wetu tunatumia mchicha pasi na kujua kuwa unafaida kiasi gani mwilini mwetu. Basi leo napenda kukwambia kuwa kamwe usiuchukulie poa mchicha na wala usiuone ni sawa na mboga zingine kwani mchicha una faida lukuki kiafya ikiwa ni pamoja na kukinga na kutibu maradhi mbalimbali. Baadhi ya maradhi ambayo unaweza kujikinga nayo kwa kula mchicha kwa ukawaida ni kama vile
1. Maumivu ya mgongo
2. Kusafisha njia ya mkojo
3. Ugonjwa wa figo
4. Minyoo
5. Baridi yabisi (Pneumonia)
6. Mchafuko wa damu
7. Matezi
8. Homa
Hayo ni baadhi tuu maradhi ambayo yanaweza yakazuilika au kutibika kwa kutumia mchicha kwa ukawaida.
MATAYARISHO:
Baada ya kujua faida za mchicha mwilini mwetu basi ni vyema ukajua namna Bora ya kuuandaa mchicha ili uweze kuwa na faida tajwa hapo juu. Wengi wetu tumekuwa tukiupika mchicha kwa desturi kama vile tunavyopika mboga zingine. Ili mchicha uweze kuwa na faida hizo unatakiwa kuuchukua mchicha, uuoshe vizuri kisha chemsha kwa dakika zisizozidi 10 pasipo kuweka nyanya na viungo vingine, sana sana weka tuu chumvi na mafuta kidogo. Kunywa supu hiyo walau bakuli moja kwa siku kwa siku saba.
TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku