Watu wengi sana wamekuwa kuwa wakisumbuka na tatizo la macho kuwa mekundu au rangi nyingine ambayo wao hawapendezwi nayo na kuna baadhi wamefika mbali zaidi mpaka kufikia hatua ya kubadilisha kiiini cha macho yao na kuweka mboni ya bandi ili tuu wawe na macho meupe. Katika maisha ya mwanadamu hakika hakuna tatizo dogo, ila kitu chochote ambacho kinaweza kumkosesha amani basi kitu hicho hugeuka na kuonekana kuwa ndiyo tatizo. Na hii ndiyo asili ya kila mtu kuna wengine hutumia mamilioni ya pesa kutafuta suluhisho la kitu ambacho mwingine anaona ni kitu kidogo. Hivyo leo nimeamua kuja na somo la jinsi ya kujiandalia dawa ambayo itatibu kabisa tatizo la kuwa na macho mekundu na hatimaye kurudisha macho yako katika asili yake ya weupe.
MAHITAJI:
1. Kabichi nyeupe robo kilo
2. Carrot kubwa nzuri 3
3. Maji safi nusu glass.
MAANDALIZI NA MATUMIZI YAKE:
Osha vizuri kabichi, kisha kata kata katika vipande vidogo vidogo kiasi.
Chukua karoti, zioshe vizuri kisha kata vipande vidogo vidogo pia. Weka vitu vyote hivyo kwenye blender, weka maji hayo nusu glass kisha saga kww pamoja mpaka inavyokuwa juice kabisa.
Chuja juice hiyo kisha kunywa glass moja asubuhi na jioni kabla ya kwenda kulala. Fanya hivyo kwa siku 7 na hakika utaona mabadiliko makubwa katika macho yako kuanzia muonekano, rangi mpaka uwezo wa kuona.
TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya
Hyo juice wawez hufadhi kwenye friji ana?
ReplyDeleteNashauri fresh ndo nzuri,friji inapoteza virutubisho na vyakula /vimiminika hupooza vinapohifadhiwa humo.
DeleteAhsante Sana TOPTEN HERBS
ReplyDelete