Mungu ameumba miti na mimea kwa
ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye
mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.
UBUYU WENYEWE
Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una Vitamin C nyingi kuliko hata machungwa na ina kiwango kingi cha madini ya kashiamu (Calcium) kuliko hata maziwa ya ng’ombe.
Aidha, unga wa ubuyu ni chanzo kikubwa cha madini mengine aina ya chuma (iron), Potasiamu (Pottasium) na manganizi (magnesium). Inaelezwa kuwa kiwangao cha Potasiamu kilichomo kwenye unga wa ubuyu ni mara sita zaidi ya kile kinachopatikana kwenye ndizi. Ubuyu ni muhimu sana kwa watu wenye matatizo ya figo.
Vile vile unga wa ubuyu una uwezo mkubwa wa kuongeza kinga ya mwili (antioxi-
dant) kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vya kuongeza kinga mwilini dhidi ya magonjwa nyemelezi. Kiwango chake kinazidi hata kile kinachotolewa na matunda mengine kama vile Krenberi, bluberi na blakberi. Ili upate faida za unga wa ubuyu zinazoelezwa hapa, lazima ule ubuyu halisi usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha.
Endapo umependa mada hii na unapenda kujua jinsi ya kujitibia maradhi tofauti tofauti ukiwa nyumbani, unaweza kupata kitabu chetu ambacho tumeelezea jinsi ya kujitibia maradhi zaidi ya 60. Kitabu hicho ni soft copy (digital book) na unaweza kukipata kupitia whatsapp au email yako kwa shilingi 5000/- tu. Wasiliana nasi kupitia 0676 298 270. Kama una shida yoyote ya kiafya tafadhali waweza wasiliana nami kwa simu namba 0676 298 270 au unaweza fika ofisini kwetu, Mbezi kwa Msuguri Dar es salaam
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku