Kuna njia nyingi sana za kupunguza tumbo/ uzito haraka lakini nyingi huwa zinakulazimisha ukae na njaa siku nzima hadi unajisikia kukata tamaa!. Hii ni njia rahisi zaidi kwa sababu una uwezo wa kula ukashiba na kukifurahia chakula.
Kabla haujaendelea ni muhimu kukumbuka aina hii ya kupunguza unene unayoenda kuisoma haitakiwi uiache baada ya muda mchache.
Ili upate mafanikio ya kudumu zaidi unashauriwa kuifuatilia kwa muda mrefu
Kutokula vyakula vya wanga kunasaidia kupunguza njaa hivyo kunafanya upunguze kiasi cha chakula unachokula.
Kwasababu miili yetu hutumia wanga kutengeneza nguvu ya kujikimu na shughuli zote za mwili, uhaba wa fungu hili la chakula mwilini husababisha miili yetu kutafuta mbadala wa kutengenezea hii nguvu kwa ajili ya uhai.
Kwahiyo miili yetu huamua kutumia glycogen na mafuta ambayo yanakuwa yametunzwa mwilini ambayo yanafanya tuonekane wanene ili kutengeneza nguvu kwa ajili yetu.
Mafuta yanapotumika kutengeneza nguvu badala ya wanga ndipo tutaona mabadiliko ya kupungua mwili.
Pia kupunguza vyakula vya wanga kunaleta kupungua kwa hormone ya insulin. Hii inasababisha figo kuondoa chumvi na maji mwilini hivyo kama tumbo limejaa linapungua haraka sana.
Mara nyingi watu wanapata tumbo kujaa(bloating) na wanadhani ni gesi tu inasababisha lakini kula vyakula vingi vya wanga na chumvi nyingi kunasababisha mwili ujae maji hivyo tumbo linakuwa limechomoza sana
Endapo umependa mada hii na unapenda kujua jinsi ya kujitibia maradhi tofauti tofauti ukiwa nyumbani, unaweza kupata kitabu chetu ambacho tumeelezea jinsi ya kujitibia maradhi zaidi ya 60. Kitabu hicho ni soft copy (digital book) na unaweza kukipata kupitia whatsapp au email yako kwa shilingi 5000/- tu. Wasiliana nasi kupitia 0676 298 270. Kama una shida yoyote ya kiafya tafadhali waweza wasiliana nami kwa simu namba 0676 298 270 au unaweza fika ofisini kwetu, Mbezi kwa Msuguri Dar es salaam
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku