Neno U.T.I ni kufupisho cha maneno Urinary Tract Infections ikiwa na maana maambukizi kwenye njia ya mkojo na mfumo wake. U.T.I husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bacteria waitwao Escherichia coli (E. Coli) ambao huingia mwilini na kwenda kuathiri mfumo wa mkojo. Wanawake ndio wako kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa huu kuliko wanaume kutokana na sababu za kimaumbile. Ikiwa umepimwa na kuambiwa kuwa una tatizo hili basi tumia dawa hii.
MAHITAJI:
(i.) Vitunguu maji vikubwa vinne(4)
(ii.) Baking soda (Bicarbonate)
(iii.)Maji lita moja na nusu
MATAYARISHO NA MATUMIZI:
Katakata vitunguu vyako na uvichemshe kwenye maji lita moja na nusu kwa dakika kumi (10), epua na acha yapoe ukiwa umefunika sufuria yako. Baada ya kupoa yachuje na uyahifadhi kwenye chombo safi chenye mfuniko. Chukua kikombe cha maji ya vitunguu kisha weka nusu kijiko cha chai cha baking soda na ukoroge vizuri. Mgonjwa anywe kikombe kimoja asubuhi na kingine jioni kwa siku 3 mfululizo kwa uwezo wa Mungu atakuwa amepona kabisa. Pia unaweza kuepukana na tatizo hili kwa kunywa maji mengi, kuacha kutumia dawa za uzazi wa mpango, kula vyakula vya asili, kukojoa mara baada ya kushiriki tendo la ndoa, kujitahidi kuwa msafi nyakati zote na kuacha matumizi ya pombe na sigara.
Endapo umependa mada hii na unapenda kujua jinsi ya kujitibia maradhi tofauti tofauti ukiwa nyumbani, unaweza kupata kitabu chetu ambacho tumeelezea jinsi ya kujitibia maradhi zaidi ya 60. Kitabu hicho ni soft copy (digital book) na unaweza kukipata kupitia whatsapp au email yako kwa shilingi 5000/- tu. Wasiliana nasi kupitia 0676 298 270. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Mbezi kwa Msuguri Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku