Je, Unajua Bawasiri/Hemorrhoids Ni Nini?
Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe. Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS
na kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles. Tatizo la bawasiri huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50% ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 40 mpaka 50.
Nini Chanzo Cha Bawasiri?
Bawasiri kwa kiasi kikubwa huletekezwa na kuongezeka kwa mgandamizo ama presha mara nyingi ni pale unapojikaza ili kutoa haja kubwa. Hivo bawasili huwatokea zaidi watu wenye matatizo ya mfumo wa umeng’enyaji mfano unapata choo kigumu, tumbo kujaa gesi, kukosa choo kwa siku kadhaa. Wanawake wenye ujauzito pia huwa kwenye hatari kubwa ya kupata bawasiri kutokana na mtoto aliye tumboni kugandamiza tumbo la chakula na hivo kuathiri utoaji wa haja kubwa, kwa bahati nzuri bawasiri inayosababishwa na ujauzito huanza kuisha pale tu mama anapojifungua. Watu wenye kitambi na uzito mkubwa pia wapo kwenye hatari kubwa ya kupata bawasiri kutokana na mwili kushindwa kutengeneza nishati ya kutosha kusukuma uchafu kwenye utumbo.
MAHITAJI:
(i.) Unga wa magome ya mng’ongo vijiko vya chakula vinne( 4)
(ii.) Unga wa habat soda vijiko vya chakula vinne( 4)
(iii.) Bakali hadi vijiko vya chakula vinne( 4)
(iv.) Manemane vijiko vya chakula vinne( 4)
(v.) Mafuta ya nyonyo
MATAYARISHO NA MATUMIZI YAKE:
Changanya mng’ongo, habbat soda, bakali hadi, na Manemane kisha chemsha kwenye maji ya lita sita, viache vichemke kwenye moto wa wastani kwa dakika 20 hadi 30, epua na uache ipoe ikiwa imefunikwa. Baada ya kupoa chuja kwa chujio au kitambaa safi upate maji yake tu. Mgonjwa anatakiwa kunywa nusu kikombe cha dawa hii kutwa mara mbili kwa siku 25, Pia mgonjwa anatakiwa kuwa anapaka mafuta ya nyonyo kwenye huo uvimbe wa bawasiri kila anapotoka chooni.
Endapo umependa mada hii na unapenda kujua jinsi ya kujitibia maradhi tofauti tofauti ukiwa nyumbani, unaweza kupata kitabu chetu ambacho tumeelezea jinsi ya kujitibia maradhi zaidi ya 60. Kitabu hicho ni soft copy (digital book) na unaweza kukipata kupitia whatsapp au email yako kwa shilingi 5000/- tu. Wasiliana nasi kupitia 0676 298 270. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Mbezi kwa Msuguri - Dar es Salaam kwa ushauri zaidi.
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku