Kwa kutumia utafiti usio rasmi, utakubaliana nami kuwa kumekuwa na mtazamo
uliojengeka katika jamii kuwa mwanaume ukiwa umemuoa mwanamke na kuwa
mwili mmoja, basi una kila haki ya kumshika sehemu yoyote uipendayo hasa
wakati unahitaji kufanya nae tendo la ndoa.
Lakini utafiti na uzoefu uliokusanywa na wataalam wa mahusiano na ndoa
waliofanya mahojiano na wanawake kama kuna sehemu wazisopenda kuguswa
na waume zao na nyakati husika, umetoa picha na mtazamo ambao wanaume
wanapaswa kuufahamu mapema kabla hawajaingia katika hatari ya kuwa kero au
kuwakwaza wenza wao.
Kama ulikuwa haufahamu, nikujuze kuwa wanawake ni viumbe wenye mlango
mmoja wa ziada wa fahamu kuwapita wanaume. Hii nitaizungumzia siku nyingine
kwa urefu. Lakini mlango huu wa ziada ndio huwapa hisia ya ziada pamoja na
kuwafanya kujali sana vitu ambavyo mwanaume hasa mwenye haja ya kufanya
tendo anaweza asizingatie sana wakati anataka kukidhi haja yake.
Ukifuatilia sehemu hizi za mwili wa mwanamke nitakazozitaja na nyakati zake,
utabaini kuwa ni rahisi sana kubaini kuwa umegusa pasipo kwani mwanamke
katika nyakati hizo anaweza kuonesha kusita sana au hata kubadilika kihisia.
1. Chuchu wakati miili yao inaendelea na shughuli nyingine za ndani
Idadi kubwa ya wanawake huwa hawapendi kuguswa na wanaume chuchu zao
wakati wananyonyesha au wakati wako katika hedhi. Hiki ni kipindi ambacho
kama mwanamke ananyonyesha na mwanaume anataka kumgusa sehemu hiyo
basi maziwa yanaweza kutoka kwa kasi na kumfanya ajisikie hayuko ‘confortable’
kuendelea na zoezi la kushiriki tendo (kama hayuko hedhi).
2. Kwapani wanapokuwa wanatoka jasho
Wanaume wengine huwa na hisia za matamanio zaidi wanapoyaona makwapa ya
wake zao. Hii ni hali ya kisaikolojia inayojengeka kwa baadhi ya wanaume. Kuna
wanaume wakiona kwapa la mwanamke basi matamanio yao huongezeka mara
dufu. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hujisikia vibaya na kukosa
amani pale wanaume zao wanajaribu kuwashika kwapani wakati ambapo wametokwa
jasho.
3. Sehemu za siri kabla ya kuoga
Hili ni eneo ambalo wanawake wengi wameonesha kuwalalamikia waume zao.
Kwa mazoea wanaume wengi huwa kama wanawabaka wake zao bila kufahamu,
hasa pale wanapotoka safari zao wakiwa na matamanio. Lakini wanawake wengi
wameeleza wazi kuwa hupoteza hali ya kuwa ‘comfortable’ pale wanapoguswa na
wanaume zao sehemu za siri wakati bado hawajaoga.
Wanaume wengi hujikuta wakishiriki tendo la ndoa na wake zao ghafla baada ya
kukamilisha kazi kadhaa za ndani wakati wanawaangalia. Wanaume wanaweza
kuwa wanafurahia zaidi tendo hilo lakini wanawake pamoja na kwamba hufurahia
pia lakini mlango wao wa ziada wa fahamu huwafanya kukosa amani kwa kiasi
fulani wakati wa tendo ukilinganisha na nyakati ambazo wanajiamini ni wasafi.
4. Nywele zao dakika chache baada ya kutoka saloon kujiremba
Ingawa unaamini kuwa mkeo alienda saloon kujiremba kwa ajili ya kukuvutia
wewe, usithubutu kutaka kuzivuruga nywele zake dakika chache baada ya kutoka
kwa mtaalam wa kutengeneza nywele, hata kama pesa aliyotumia ulimpa wewe.
Hiki ni kama kituko hivi, lakini ndio ukweli. Wanawake hutumia muda mrefu
sana kwenye vibanda au saloon za gharama kwa ajili ya kujiremba ili waongeze
mvuto. Lakini, hugeuka kuwa walinzi wa vichwa vyao angalau kwa saa kadhaa.
Msifie uwezavyo, lakini nywele zake usizivuruge mapema mtaharibiana ‘mood’.
Haya ni kati ya mambo machache ambayo wanaume huyaona madogo sana na
kufuatilia yale wanayoamini ni makubwa zaidi. Lakini mambo haya ni kati ya
machache yanayokwangua taratibu kuta za hisia za mwanamke kwa mumewe.
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku