Tendo la ndoa limezungukwa navmambo mengi sana ambayo hata wataalam wa mahusiano na
madaktari bingwa wameshindwa kuyamaliza. Tafiti mbalimbali zimekuwa zikija na matokeo mapya
na hata kubadili matokeo ya tafiti za awali kutokana na muda husika. Leo, nimeamua kukueleza
kuhusu mambo matano tu kati ya hayo mengi, unayopaswa kuyafahamu kwa ajili ya ufahamu wako tu lakini pia kwa afya yako ili yakusaidie katika maamuzi unayochukuwa unapokuwa eneo la tukio au unapopanga kufanya tukio hilo. Hii imewalenga zaidi watu walio kwenye ndoa na kuwaandaa wanaotaka kuingia kwenye ndoa.
1. Mwanaume hutoa mbegu hadi milioni 300 kwa tendo moja tu la ndoa, lakini
mbegu moja pekee hutumika kuzalisha mtoto inapokutana na yai la mwanamke
lililotayari.
2. Kufika kileleni kwa mwanamke ni msaada mkubwa kiafya kwake. Huweza
kumsaidia mwanamke kupunguza hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo,
kupooza, kansa ya matiti pamoja na msongo wa mawazo.
3. Mwanamke anapokuwa kileleni hukaa takribani sekunde 20 hadi 14, tofauti
na wastani wa mwanamme ambaye hukaa kwa wastani wa sekunde 6 tu. Hata
hivyo, tofauti na mwanamke, mwanaume anapokuwa kileleni hupitiwa na giza zito
katika ubongo wake kwa sekunde takribani tatu (blackout).
4. Tendo la ndoa hupunguza maumivu ya kichwa.
-Utafiti uliofanywa na wa wataalam wa saikolojia na uhusiano kutoka Chuo Kikuu
cha Munster chini Ujerumani umebaini kuwa tendo la ndoa husaidia kupunguza
maumivu ya kichwa. Utafiti huo uliochapishwa mwaka 2013, ulibaini kuwa mtu
mmoja kati ya watano waliofanya mapenzi wakiwa na maumivu ya kichwa, alimaliza
akiwa hana maumivu hayo tena.
5. Kwenda haja ndogo muda mfupi kabla ya tendo la ndoa ni hatari zaidi kwa
afya.
-Ingawa wataalam wengi wa afya wamekuwa wakieleza kuwa kwenda haja ndogo
kabla na ya tendo kunasaidia kuepuka ugonjwa wa UTI, huu sasa unatajwa kuwa
‘nusu ukweli’.
UTI hutokea pale kibofu cha mkojo kinapopata bakteria wanaoingia kupitia njia
ya mkojo. Na tendo la ndoa linaweza kusaidia maambukizi wa bakteria hao
kuwatoa kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Kwa mujibu wa Dk. David Kaufman wa New York Marekani, kwenda haja
ndogo kabla ya kufanya tendo la ndoa ndio chanzo cha kupata athari kubwa zaidi
ya bakteria ikiwa kutakuwa na maambukizi.
Alieleza kuwa kwenda haja ndogo kunasaidia kuweka nafasi kubwa zaidi kwenye
kibofu cha mkojo kiasi cha kutunza bila kusumbuliwa, bakteria wengi zaidi.
Hata hivyo, ni salama zaidi kwenda haja ndogo muda mfupi tu baada ya kufanya
tendo la ndoa kwasababu inasaidi ku-flash bakteria kwa kiaisi kikubwa
waliotokana na tendo la ndoa (sio virusi vya ukimwi).
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku