Pre
mature ejaculation ni nini?
Hii ni hali ambayo mwanaume anatoa mbegu
mapema sana kipindi cha tendo la ndoa na mara nyingi huambatana na kushindwa
kumridhisha mpenzi wake.
Tatizo hili limekua likiwapata wanaume wengi
na kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada
ya hali hii kutokea.
Kimsingi mwanaume anatakiwa achukue dakika nne
mpaka nane kabla ya kutoa mbegu za kwanza lakini watafiti wanasema tatizo hili
hugundukiwa mtu anapotoa mbegu ndani ya dakika moja au kabla ya dakika moja.
Tatizo hili huweza kutokea mara tu baada ya
kubalehe,{primary pre mature ejaculation} mda mrefu baada ya kubalehe{secondary
PE} au kutokana na aina ya mwanamke uliompata.{situational PE}
Chanzo ni nini?
Tatizo hili halina sababu za kitaalamu
zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila wanasayansi wanaamini sababu zifuatazo
zinaweza kua chanzo kikuu cha tatizo hilo.
Kupiga punyeto au kujichua;
Mara nyingi watu wanaopiga punyeto hua
wanafanya haraka kwa kujificha ili wasikutwe na mtu. tabia ile ya kulazimisha
mbegu zitoke haraka huweza kuleta tatizo hili.
Kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la
ndoa;
Kukaa muda mrefu sana bila kushiriki tendo la
ndoa husababisha mkusanyiko mkubwa wa mbegu za kiume ambazo zinaleta msisimko
mkubwa na ukichelewa sana kushiriki tendo la ndoa zitatoka kwenye ndoto nyevu.
Kawaida mwanaume anatakiwa ashiriki tendo angalau mara nne kwa wiki.
Kuwa na wasiwasi wakati wa tendo la ndoa;
Mtu akiwa na historia ya kupata hali hii
kabla, huwa hajiamini na kuwa na wasiwasi kwamba litatokea tena na matokeo yake
hulipata kweli.
Madhara ya dawa zinazofanya kazi kwenye
mishipa ya fahamu;
Baadhi ya dawa za usingizi, mawazo na zingine
zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu huleta tatizo hili mfano
amitriptyline.
Kurithi;
Baadhi ya koo au familia fulani hurithi
vimelea vya kuwa na ugonjwa huu kwa vizazi mbalimbali vya familia husika.
Magonjwa ya mfumo wa uzazi wa mwanaume mfano
prostatitis.
Diagnosis {kuutambua ugonjwa}
Mwanaume yeyote ambaye anatoa mbegu chini ya
dakika moja au mbili ni muhanga wa hili tatizo na anatakiwa apewe matibabu.
Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyika sehemu
kuu mbili kulingana na ukali wa tatizo husika.
Non pharmacological treatment {matibabu yasiyo
hitaji dawa}: Matibabu haya hupewa watu ambao wanahimili mpaka dakika tatu bila
kutoa mbegu.
Pharmacological treatment {matibabu yanayohusu
dawa}: Matibabu haya hupewa watu ambao hutoa mbegu ndani ya dakika moja baada
ya kuanza kushiriki tendo la ndoa, watu hawa hushauriwa kutumia na mbinu zote
mbili za matibabu.
Yafuatayo ni matibabu yasiyohitaji dawa.
Tumia condom:
Condom ni moja ya tiba nzuri ya tatizo hili
kwani hufanya kazi kwa kupunguza hisia kali za mapenzi mtu anazozipata pale
ambapo hatumii condom.
Kandamiza perineum kwa kidole:
Perineum ni eneo kati ya mkundu na korodani, ile
sehemu ikikandamizwa na kidole huweza kuzuia kukojoa haraka wakati wa tendo la
ndoa.
Punguza wasiwasi:
Hebu lifikirie tendo hili kama njia ya
kujifurahisha sio njia pekee ya kutafuta kutoa mbegu, hii itakusaidia kuondoa
mawazo ya kutafuta mbegu na kuchelewa kumaliza.
Fanya taratibu:
Picha za ngono zinadanganya sana watu kwamba
kulala na mwanamke lazima ufanye kwa haraka haraka kama mbwa. HAPANA; ukifanya
taratibu ndio njia nzuri ya kumfikisha mwenzako na wewe kuchelewa kufika
kileleni.
Badilisha style:
Ile style ya zamani ya kumlalia mwanamke kwa
juu{missionary position} inaleta msuguano mkubwa kwenye kichwa cha uuume hivyo
itakufanya ufike haraka sana.
Tumia style ya wewe mwanaume kutangulia chini
afu mwanamke juu au kulala kwa upande wote mnaangalia upande mmoja hii
itakusaidia sana kuchelewa
Toa mawazo kwamba unafanya ngono:
Hebu jaribu kufikiria mambo mengine ya kikazi
au masomo wakati unafanya tendo hilo, hii itakupunguzia hisia kali za mapenzi
na kuchelewa kufika.
Fanya na kuacha:
Hii ni ile hali ya kuzuia msuguano pale
unapoona unakaribia kutoa mbegu kwa kama sekundi 30 kisha unaanza upya.
Hakikisha haufiki “point of no return”. pointi ambayo huwezi kujizuia tena
kumaliza.
Kandamiza sehemu ya shingo la uume:
Hii sehemu ya shingo ya uume kwa chini ambayo
ukiibana itakusaidia kuanza upya tena kihisia. Nimetumia shingo la uume
kwasababu najua uume hauna mabega.
Tumia kilevi:
Unywaji wa pombe mfano bia mbili kwa siku kwa
wanaume pombe hupunguza kidogo nguvu ya mishipa ya fahamu na kufanya mtu aliyekunywa
kuchelewa sana kufika kileleni, [watu wanaokunywa pombe lazima mtakubaliana na
hili] hivyo unaweza kunywa bia, wine au whisky nusu saa kabla ya tendo na
kuondoa shida hii.
Pengine umejaribu
kufuata ushauri huo hapo juu lakini bado unaona tatizo linazidi kuendelea na
pengine unaona kama ndio linazidi kuwa kubwa sasa hapo inawezekana ukawa na
tatizo la upungufu wa Nguvu za Kiume. Acha tulichambue kidogo
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku