Mti wa mwembe mbali ya kuzaa tunda la embe ambalo hutumika kama chakula au kinywaji ( juisi ) chenye ladha
ninayo vutia, una faida lukuki za
kiafya kwa mwili wa mwanadamu.
Zifuatazo ni baadhi ya faida za
kiafya za mti wa mwembe.
1. MAJANI YA MTI WA
MWEMBE :
Majani machanga ya mti
wa mwembe yakichemshwa huwa na faida
zifuatazo ;
i. Hutibu pumu
ii. Hutibu kifua kikavu
iii. Hutumika katika kuoshea
vidonda vitokanavyo na majeraha mbalimbali
( Majani ya maembe yamethibitika kuwa
na uwezo mkubwa wa kukausha majeraha ya
vidonda )
iv. Unga wa majani
ya mwembe hutumika katika kutunza meno
ambapo mtu mwenye matatizo ya meno
atatakiwa kusukutua kwa kutumia unga
unaotokana na majani ya mwembe.
v. Vilevile Majani hutumika kutibia kabisa tatizo la kisukari type 2,
Mgonjwa anatakiwa kuloweka majani ya kutosha kwenye maji nusu lita aache yalale
huku halafu asubuhi afikiche vizuri hayo Majani kasha achue na anywe hayo maji.
Anatakiwa kufanya zoezi hili kwa muda wa Mwezi Moja.
2.KOKWA LA EMBE
Unga unaotokana na kokwa la embe
husaidia kuzuia kuharisha na kuhara damu.
3. TUNDA LA EMBE
i.Ulaji wa tunda
la embe husaidia kutibu minyoo na
kuzuia uvujaji wa damu ovyo.
ii. Tunda la embe
lina vitamin C na
hivyo ulaji wake husaidia kuponesha vidonda
kwa haraka, hivyo basi mlaji sana wa
tunda la embe endapo atapata vidonda
basi atapona kwa haraka sana kuliko mtu
asiye tumia tunda hili mara kwa mara.
iii. Huwasaidia watu
wenye matatizo ya kutokupata choo.
iv. Utumiaji wa maembe
mabichi husaidia kuondoa mawe kwenye figo
na hivyo kuepuka kufanyiwa upasuaji.
v. Embe bichi
likichanganywa na chumvi na sukari na kasha
kuchemshwa ni tiba ya tatizo
la mapigo ya moyo kwenda kwa haraka.
4.MAGOME YA MWEMBE
Magome ya mti wa mwembe yakichemshwa ni dawa nzuri ya homa.
5. MIZIZI YA MWEMBE
Mizizi yake ni dawa nzuri sana kwa meno haya meno yaliyotoboka,
Unachotakiwa kufanya ni kuchukua mizizi ya kutosha kasha chemsha na usukutue
utwa mara 3 kwa siku 7 kwa uwezo wa Mungu utakuwa umepona kabisa tatizo la
Meno.
JUISI YA EMBE :
Juisi ya embe
ikichanganywa na maziwa fresh
husaidia kurejesha afya ya mtu aliye dhoofika.
Vile vile kunusa juisi ya
embe kunasaidia kuzuia tatizo la kutoka
damu puani. Hivyo basi juisi ya
embe inaweza kutumika kama huduma ya
kwanza kwa mtu anaye tokwa na
damu puani.
USHAURI
Unapotengeneza Juisi ya Maembe hakikisha huweki sukari kabisa, unapoweka
sukari unapunguza nguvu ya Hii Juisi katika matibabu. Vilevile unapotumia
Sehemu yoyote ya Mti huu au matunda hakikisha vipo katika hali nzuri usitumie
vitu vilivyooza au kuharibika.
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku