Ndizi ina aina tatu za kipikee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama
Sucrose, Fructose na Glucose na vile vile ina kiasi kingi cha ufumwele (fibre)
ambacho husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.
Ndizi ina uwezo mkubwa wa kuongeza na
kuimarisha nishati ya mwili. Unaweza kupata nishati ya kufanyakazi ya muda wa
dakika 90 kwa kula ndizi mbili tu. Bila shaka ndizi ni tunda muhimu sana kwa
wanamichezo. na ni tunda lenye uwezo pia wa kuponya na kuzuia matatizo mengi ya
kiafya:
MFAIDHAIKO WA AKILI (DEPRESSION):
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama Cha
Afya ya Akili cha Taifa (MIND) cha nchini Uingereza, kwa watu wanaosumbuliwa na
tatizo la mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana na tatizo hilo hujisikia
vizuri baada ya kula ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli kwamba ndizi ina
kirutubisho kinachojulikana kama tryptophan, ambacho ni aina fulani ya protini
inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.
MATATIZO WAKATI WA HEDHI (PMS)
Kama wewe ni miongoni mwa wale akina mama
wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula
ndizi mbivu na unaweza kuponywa. Vitamin B6 iliyomo kwenye ndizi, hurekebisha
kiwango cha sukari ambacho huweza kuathiri hali ya mtu.
UPUNGUFU WA DAMU (ANAEMIA):
Ndizi ikiwa ni chanzo kizuri cha madini aina
ya chuma (iron), inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya upunguvu wa damu kwa
sababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.
SHINIKIZO LA DAMU:
Tunda hili ni la aina ya kipekee, lina kiwango
kikubwa cha madini ya potasiamu (potassium) na wakati huo huo lina kiasi kidogo
sana cha chumvi (sodium) hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na
tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu.
Ukweli huo, hivi karibuni umeifanya Mamlaka ya
Dawa na Chakula ya nchini Marekani, iwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa
ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya
shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.
NGUVU YA AKILI:
Hivi karibuni, wanafunzi wapatao 200 wa Shule
ya Twickenham nchini Uingereza, walisaidiwa kufaulu mitihani yao kwa kula ndizi
mbivu wakati wa mlo wa asubuhi (breakfast), wakati wa mapumziko na wakati wa
chakula cha mchana, ndizi ziliongeza uwezo wa akili zao. Utafiti unaonesha kuwa
potasiamu iliyojazana kwenye ndizi, ina uwezo wa kumsaidia mwanafunzi kuamsha
uwezo wake wa kujisomea.
MNING'INIO (HANGOVERS):
Moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu
unaotokana na ulevi wa jana yake (hangover) ni kunywa”Milkshake'
iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali. Ndizi hutuliza tumbo, ikisaidiwa na
asali, hurejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu, wakati maziwa
hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.
Mbali na matatizo yaliyoelezwa hapo juu, ndizi
pia husaidia katika matatizo mengine mengi kama vile kutuliza mishipa ya
fahamu, kuondoa wasiwasi, kutuliza vidonda vya tumbo, kuondoa asidi tumboni,
kushusha joto mwilini, kurekebisha mapigo ya moyo, n.k
NGUVU ZA KIUME
Mbali ya Faida
hizo hapo Juu tunda hili limethibitika kuwa na uwezo wa kuongeza vichocheo
vinavyoboresha nguvu za kiume kwa haraka sana. Mtu mwenye tatizo la kuwahi
kufika kileleni mapema anatakiwa kutumia Ndizi mbivu na karoti Nusu saa kabla
ya kushiriki tendo hilo la ndoa.
Vilevile ulaji wa ndizi mbivu mara kwa mara husaidia kuboresha mzunguko
mzuri wa Damu ambao ndio Jambo muhimu zaidi katika kuweka sawa nguvu za kiume.
UNENE
unaweza kuondoka kwa kuacha kula kila kitu isipokuwa ndizi
baada
ya dozi hiyo, rudia kula ndizi 5 hadi 10 mara 3 kutwa,
baada
ya dozi hiyo rudia kula ndizi 2 tu kwa kila mlo.
Matokeo
yatakuwa wazi baada ya kumaliza dozi hiyo.
Ndizi
isitiwe mafuta mengi
Usile
ndizi na pombe (usababisha kiungulia)
Ndizi
isitumiwe mara 1 kwa wingi.
Hivyo ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni
bora, ukiilinganisha na Epo (Apple), ndizi ina protini mara nne zaidi, wanga
mara mbili, vitamin A na chuma mara tano na vitamini na madini mengine mara
mbili zaidi ya epo.
Mwisho; USIWEKE NDIZI KWENYE JOKOFU!
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Iyo dozi ya ndizi niya Siku ngap
ReplyDelete