Watu wengi sana hasa wanandoa wamekuwa
na kiu kubwa sana ya kupata watoto wanaowataka kwa muda fulani lakini
changamoto ni kwamba wengi hawajui ni lini mke anaweza kubeba mimba hivo
napenda Leo tujifunze kwa kina jambo hili na kuondoa utata wote ambao huwa
unakusumbua. Watu wengi sana huamini kuwa mke anaweza kupata mimba muda mfupi
kabla ya kuanza hedhi au muda mfupi baada ya kumaliza Hedhi kitu ambacho sio
kweli kabisa. Sasa kwa kuwa wengi wamekuwa na taarifa zisizosahihi ndio
imepelekea wengi kujihisi hawana uwezo wa kuzaa kitu kinachopelekea kuanza
kutumia madawa mbalimbali wakati hawana tatizo lolote lile. Sasa ukweli ni upi?
Ni lini mwanamke anaweza kushika mimba? Lini anaweza kushika mimba ya mtoto wa
Kike na Lini anaweza kushika mimba ya mtoto wa kiume.
Hiki ndicho kipengele Muhimu sana unapaswa kutulia na kusoma neno kwa neno
na kwa umakini mkubwa kwa sababu ndio sehemu itakayokusaidia kupata watoto
uwatakao kwa haraka sana. Siku hii huwa ipo kuanzia Wiki moja tangu mwanamke
anapomaliza Hedhi yake. Lakini Zipo njia kuu nne unazoweza kuzitumia kuitambua
siku hiyo
1. UTE
Kwa kawaida wanawake hukotwa na ute wa aina mbalimbali kila ute huwa na
tafsiri yake na Kazi yake. Katika
kipengele hiki tunazungumzia ule ute unaofanana na Ute mweupe wa Yai. Ikifika siku hiyo mwanamke hutokwa na Ute huo
sana hiyo ni dalili ya kwanza japo kuwa sio wanawake wote hupata Ute huu.
2.
JOTO LA MWILI. Kipindi hiki joto la
mwili wa mwanamke huwa kali zaidi kuliko kawaida yake. Kama unatumia kipima
joto kipindi hiki joto huziti kwa 0.5 hadi 1 centigrade.
3.
NYEGE / HAMU YA KUSHIRIKI
TENDO LA NDOA hiki ni kiashiria kingine cha kuwa mwanamke yupo kwenye
siku za hatari za kusika mimba, kipindi hiki mwanamke huwa na hamu kubwa sana
yakushiriki tendo la ndoa kuliko kawaida…. Lakini katika hili unapaswa kuwa
makini sana maana kwa kawaida manamke huwa na nyege mara tatu kwa mwezi. Kabla
ya kupata hedhi, baada ya kupata hedhi, na siku ya kushika mimba hivo ni muhimu
sana kuzingatia hizi ni nyege za wakati gani ikiwa imepita wiki moja tangu
amemaliza hedhi yake afu ana nyege balaa basi tambua kuwa ndio siku yenyewe
hiyo.
4. Kuafata Kalenda au Mzunguko. Ili uweze kuitumia njia hii ni lazima mwanamke awe anajua idadi ya siku katika mzunguko wake. Najua hapo nimekuacha kidogo hahahaha wengi huwa wanafikiri ni idadi ya siku ambazo mwanamke anapata Hedhi sivyo hivyo hata kidogo. Ukisikia idadi ya siku katika mzunguko wako tunakusudia idadi ya siku zote kutoka unapoona damu mwezi huu hadi unapoona damu mwezi unaofuatia. Mfano kama mwanamke hedhi tarehe 4 afu akaja kupata tena hedhi tarehe 30 ya mwezi huo huo tunahesabu hivi 4,5,6,7,8,9,10,11,12,13,14,15,16,17,18,19,20,21,22,23,24,25,26,27,28,29,
Hesabu siku zote kuanzia ile tarehe uliyopata damu hadi siku moja kabla ya
kupata damu ya mzunguko mwingine. Ukiangalia kwenye mfano huo tumepata siku 26
Sasa unatakiwa kufanya zoezi hili kwa angalau miezi mitatu mfululizo ili
uwe na hakika kuwa mzunguko una siku ngapi kwa hakika.
Baada ya kuwa na hakika kuwa mzunguko wako una siku kadhaa hapo sasa
umemaliza mchezo. Kwa kawaida wanawake wote wanafanana idadi ya siku kuanzia
siku yai linaposhuka hadi siku ya kupata Hedhi wote ni siku 14. Hivo ilikujua
siku ya yai kushuka unatakiwa kuchua idadi ya siku kwenye mzunguko wako
upunguze 14.
Kwenye ule mfano wetu tulipata siku 26 ukipunguza siku 14 unapata 12, hiyo ndiyo siku ambayo Yai linashuka na
ndioa siku ya kupata mimba. Hivo katika mfano wetu hapo juu siku ya kubeba
mimba ni tarehe 15. Nafikiri umeelewa vizuri sana hapo… Hebu tabasamu kidogo
maana ni hesabu ndogo kabisa ambayo haihitaji kuumiza kichwa chako kabisa.
Najua sasa utapenda kuniulize je, natakiwa kushiriki tendo la ndoa siku
hiyo tu ili mke wangu abebe mimba? Jibu ni hapana kikawaida mbegu za kiume huwa
zinadumu ndani ya mwili wa mwanamke kwa hadi masaa 72 nikimaanisha siku tatu.
Hivo ukishiriki siku 3 kabla, siku 2 kabla, siku 1 kabla, siku yenyewe, siku
moja baada ya yai kushuka mke anaweza kubeba mimba.
Nafikiri utakuwa unapenda kufahamu ni kwa nini nasema siku moja tangu Yai
limeshuka ndio mwisho mke kubeba mimba. Kikawaida yai la mwanamke huwa
linasubiria mbegu ndani ya Masaa 24 tu tangu lilipotoka kule kwenye mfuko wa
mayai. Ikiwa hakuna mbegu itakayoingia ndani ya muda huo basi yai hili huanza
kuharibika na haliwezi kutungisha mimba tena.
Hivo katika mfano wetu hapo juu siku za kubeba mimba ni tarehe 12,13,14,15
na 16 tu. Na wewe hebu kufuatisha mfano huo jipigie hesabu ya mzunguko wako.
Daah kama nakuona vile jinsi ulivofurahi baada ya kulielewa somo hili
ambalo limekuwa likikusumbua kwa muda mrefu.
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Nina swali
ReplyDelete