· Uzito uliopitiliza:
Mara nyingi wanawake
wenye uzito mkubwa huwa wanakumbwa na matatizo ya homoni kutokuwa sawa kitu
kinacholekea Mvurugiko wa Hedhi, na mayai kushindwa kupevuka kwa wakati. Hivo
kama una uzito mkubwa na unatamani kupata mimba basi ni vizuri kuanza kupungua
uzito wako kwanza na mambo yatatiki haraka sana. Ikiwa uzito mkubwa umekuwa
kikwazo kwako basi Jaribu kufuata utaratibu wa kula niliouelekeza mwanzo wa
kitabu hiki kwa mwezi mmoja utakaa sawa
· Uzito mdogo sana:
Kama ilivyo kwa mtu
mwenye uzito mkubwa pia mwanamke anapokonda sana huwa inakuwa kikwazo kwake
kupata mimba kwa haraka kwa sababu ya mvurugiko wa Homoni. Ikiwa wewe unashida
ya Uzito mdogo jitahidi kula parachichi moja kubwa kila siku kwa mwezi moja na
nusu utakuwa vizuri kabisa.
· Uchache wa Mbegu za Kiume.
Wanaume wengi siku hizi
wamekuwa wanakabiliwa na changamoto hii ya mbegu kuwa chache sana, kutokuwa
kamili au kushindwa kuogelea vizuri. Kitu kinachopelekea kushindwa kutungisha
mimba kwa haraka. Ikiwa wewe ni mwanaume unakabiliwa na changamoto hii basi
chukua majani ya mapera na yachemshe uache yapoe kisha kunywa hayo maji kikombe
cha chai kutwa mara tatu kwa siku 7 hadi 21 kwa uwezo wa Mungu tatizo hili
litakwisha.
· Maradhi ya P.I.D Ukisikia neno PID tambua kuwa ni kufupisho cha maneno ”Pelvic Inflammatory Diseases” yanayomaanisha “Magonjwa yanayoshambulia Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke” tukimaanisha Mfuko wa Uzazi, Mirija, Mfuko wa Mayai na Mlango wa Kizazi. Mara nyingi tatizo hili husababishwa na Magonjwa ya Ngono kama Kaswende, Kisonono, Chlamydia na mengineyo.
Nafikiri sasa utapenda kufahamu kuwa tatizo hili huwapata
watu gani? Tatizo hili huwapata wanawake Pekee na sio Wanaume. Mwanaume yeye
huwa ni msambazaji kama ilivyo kwa Mbu na Malaria, Mbu yeye haumwi Malaria ila
husambaza kutoka kwa Mtu mwenye tatizo kwenda kwa mtu asiye na Tatizo.
DALILI
ZA P.I.D
Mara nyingi wanawake wenye tatizo hili huwa hawaoneshi dalili zozote zile.
Na baadhi huonesha dalili zifuatazo
1.
Maumivu chini ya Kitovu
2.
Maumivu juu ya Kitovu
3.
Maumivu wakati wa Tendo Landoa
4.
Maumivu wakati wa Kukojoa
5.
Kupata hedhi bila mpangilio
6.
Kutoa Uchafu wenye harufu kali Ukeni.
7.
Kuhisi Uchovu
Mara nyingine PID husababisha Maumivu ya Wastani au Makali sana Kwenye
Kitovu yanayoambatana na Kutapika, homa, na hata Kuzimia.
Hivo ukipatwa na dalili kama hizi ni vema kumuona daktari ufanyiwe vipimo
kwa haraka ili uweze kupata tiba vinginevyo ungojwa huu unaweza kusababisha
Ukapoteza kabisa uwezo wa Kuzaa au hata kupoteza Maisha.
Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku