MAKOSA MAKUBWA MANNE WAFANYAYO WANAUME WENGI WAKIWA KITANDANI Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

MAKOSA MAKUBWA MANNE WAFANYAYO WANAUME WENGI WAKIWA KITANDANI

 


1. Kosa la kwanza: KUWA MBALI NA MWILI WA MWANAMKE

Wakati unashiriki tendo la ndoa mwanamke anapata Raha zaidi Ikiwa mwanaume utamlalia mwili wako wote juu yake

Wanaume wengi hawajuwi hili. Usiweke mikono yako Kama stendi na kubaki juu juu tu huku uko bize na shughuli yako. Mlalie kabisa mwili wako wote ausikie na utaona mwenyewe atakavyokuzungushia kinu huko chini kwa raha zote

Hii ndiyo sababu mwanaume makini hutakiwi kuwa na kitambi. Kitambi ni ugonjwa na unatakiwa ukikatae kwa gharama yoyote

Wakati huo huo hii haitafaa kwa mwanamke mwenye ujauzito kuanzia miezi minne hivi hivyo uwe makini

Wakati huo huo pamoja na mambo ya digitali kuenea na watu kupenda usasa bado tafiti kote duniani zinaonyesha wanawake wengi bado wanafurahia zaidi staili ya Kifo cha mende yaani Ile iliyozoeleka zaidi ya mwanaume kuwa juu mwanamke chini

Wakati huo huo tumia wakati fulani kumtazama mkeo machoni na yeye akuangalie wakati mnaendelea na mechi yenu

Mwanaume mhimize mkeo akutazame usoni wakati mnaendelea na mechi yenu. Watu wengi hawajuwi faida ya hili. Pia si sahihi kufanya shughuli hii kwenye giza.

Kama ulikuwa hujuwi mimi leo nimekujuza hili BURE.

2. Kosa la pili : KUTAKA KUFANYA KILA WALIONALO KWENYE PICHA ZA X

Wanaume wengi hawafahamu kama movie zile za kikubwa ni mpango maalumu wa shetani kuharibu hiki kizazi cha sasa.

Watu hudhani kuna elimu fulani wanaweza kuipata kuhusu tendo la ndoa kwa kutazama hizo picha au video chafu. Hakuna elimu yoyote ya maana unaweza kupata kupitia hizo video zaidi ya ushetani.

Ikumbukwe hizo picha nyingi kati ya hizo zaidi ya asilimia 98 hazina ukweli wala uhalisia wa mambo. Wale ni waigizaji, ni watu walijuwa wanaenda kurekodiwa na watatazamwa na watu wengine wengi.

Hivyo hatuwezi kujua Yule mwanaume kwenye hiyo video alifanya nini nusu saa au lisaa limoja kabla ya kuanza mchezo huo. Kama alikunywa viagra kabla je wewe unajua? Kama alitumia midawa ya kuongeza nguvu je unajuwa? Kama alikunywa mizinga kadhaa ya konyagi unajuwa?

Huwezi kutazama hizo picha halafu ukataka yale uyaonayo humo ndiyo na mkeo akufanyie huo utakuwa ni utahira.

Moja ya madhara makubwa kwa mwanaume kutazama picha hizo kwanza inamuondolea hisia au hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Mwanzoni unapoanza kuzitazama utaona kama hamu yako kwa tendo inaongezeka au unasisimka zaidi lakini kadri unavyokuwa bingwa wa kutazama ujinga huo ndivyo na hamu yako na uwezo wa kuhimili tendo la ndoa unavyopungua. Hili watu wengi hawajuwi

Miaka ya karibuni baada ya kuenea kwa digitali kumekuwa na ongezeko kubwa la watu kuishiwa au kupungukiwa sana hamu ya kushiriki tendo la ndoa na wengi wanajiuliza chanzo ni nini na hawapati majibu lakini jichunguze binafsi kama umekuwa na ujinga huu wa kuangalia hizi picha basi hiyo ndiyo sababu kuu ya tatizo lako

Shida ya pili ya kutazama picha hizo ni kuwa mwanaume unaanza kujiona hufai, unajiona hutoshi, unajiona kama siyo vile ni mwanaume wa kweli jambo ambalo halina ukweli wowote ni matokeo ya kutazama ujinga huo.

Shida ya tatu ya kutazama mipicha hiyo ni kuwa inaweza kukuhamasisha kwenda kupiga punyeto jambo ambalo ni hatari kwa afya yako kuliko hata sigara!

Madhara ya punyeto nikianza kueleza hapa nahitaji post nyingine mpya inayojitegemea maana ni mengi ikiwemo kuishiwa nguvu za kiume, kuwa na uume mlegevu, kupoteza kumbukumbu kirahisi, uchovu mwingi, kukosa umakini, kuishiwa kujiamini na kuwa muoga kwa vitu hata vya kitoto na unaweza ukaishiwa kabisa uwezo wa kujiamini kumtongoza mwanamke.

Kosa moja kubwa sana wanalofanya wanaume wengi bila wao kujua ni kutazama video hizi chafu wakiwa na wake zao! Yaani kama kuna kitu kitaharibu mahusiano yako haraka bila wewe kujua sababu ni kutazama picha hizi na mkeo. Hata kama itakutokea kwa bahati mbaya kamwe usije hata siku moja kuangalia ujinga mkiwa wawili na mkeo. Kwa sasa unaweza usinielewe ila kadri siku zinavyoenda utakuja kunikubali.

Kwahiyo usije hata siku moja kutaka kutekeleza kila unaloliona kwenye picha hizo kwa mkeo au kwenye ndoa yako.

Asilimia 90 ya unayoyaona kwenye hizo picha mkeo hatakuwa tayari kuyatekeleza wakati ukishiriki naye tendo la ndoa na ujifunze kuyakubali yale ambayo mkeo au mchumba wako anayosema hayawezi au ni kinyume na mila na desturi yake!

Kama una picha au video hizi kwenye simu au computer yako zifute sasa dakika hii hii umalizapo kusoma ujumbe huu, kama kuna magroup upo huko na kuna watu wanapost mipicha hiyo ya kijinga jitowe (left) sasa hivi na usigeuke nyuma na ikitokea yoyote amekuweka tena jitowe haraka na umwambie asirudie ujinga huo utamchukulia hatua za kisheria haraka bila yeye kujua.

Kama kuna blogs au tovuti huwa unatembelea futa anuani zake na historia zake na jitahidi uzisahau huku ukimuomba Mungu akusamehe na kukubadilisha.

Nini cha kufanya; kwanza acha hiyo tabia chafu ya kuangalia hiyo mipicha isiyompendeza hata Mungu.

Unaharibu afya yako ya mwili na akili bila kujua. Pili pamoja na kupotoka huko kwako kwa kutazama mipicha hiyo tambua kuanzia leo kuwa kutaka kuyafanya yote uyaonayo kwenye hizo picha kitandani kwako ni kosa kubwa linaloweza kugharimu mahusiano yako kama hutakuwa mwangalifu.

3. Kosa la tatu : KUMPALAMIA MWENZA WAKO BILA MAANDALIZI

Kama kuna kosa kubwa wanaume mnalitenda dhidi ya wenza wenu basi ni hili.

Yaani kuna wanaume wakifika tu chumbani utasikia mama nanihii sogea hapa nikulenge. Hakuna kumbusu, hakuna kumshika wala kumchezeachezea dada wa watu wewe ukifika tu sogea hapa nikulenge!

Nikupe siri moja leo.

Kwenye tendo la ndoa mwanamke kile kitendo cha wewe kuingiza uume kwake ni cha mwisho kabisa yaani cha mwisho kabisa linapokuja suala la tendo la ndoa kwake.

Sasa mpo wanaume baadhi yenu ukitoka kazini unapitia bar unalewa weee huko mpaka saa tano usiku halafu unakimbia kurudi nyumbani na ukifika tu hata salamu tu hakuna tayari unataka huduma. Kuweni siriasi kidogo na wenza wenu jamani.

Mwanamke wa umri wowote anahitaji kuandaliwa kwanza kisaikolojia juu ya hilo tukio.

Siku hizi kuna simu unaweza kuanza kumtumia sms za kumwamsha tangu ukiwa barabarani unarudi nyumbani.

Kila mara tumia japo dakika 20 kumuandaa tu mwenzio kabla ya kumvua nguo ya ndani.

Kama ni mkeo na unamwamini hana magonjwa muandae kwa vyovyote utakavyoweza mhimu tu asiwe na magonjwa au mhuni mhuni maana kuna magonjwa ya kansa ya koo kama usipokuwa makini.

Vile vile hii isiwe kama vile sala ya baba yetu kwamba lazima kila siku na kila wakati iwe hivi, mara moja moja sana unaweza kumuambia tu njoo nikulenge lakini isiwe ndiyo desturi yako ya siku zote atakuchoka!

Mbembeleze ndiyo mkeo na ndiyo huyo ukiumwa saa nane za usiku wa kwanza kukusaidia, ni ubavu wako tafadhali mbembeleze na tumia muda mwingi kumuandaa kabla ya mechi yenu

Ukiwa mjanja wapo wanawake anaweza kufika hadi kileleni wakati tu ule akiandaliwa kiasi kwamba ukianza kumlenga unakuwa umebaki wewe huhitaji hata kutumia dakika nyingi kubaki hapo unalima ili kumfikisha kwani anakuwa alishafika zamani.

Wanawake ni watu wa hisia sana.

Hakikisha hana mawazo mawazo au stress ya aina yoyote maana kama ana stress kama vile wanawake wengine yupo chumbani anawaza madeni ya vicoba sasa huyu unaweza kukesha ukimuandaa na asiandalike.

Kuwa karibu naye kumsoma nini kinamsibu na nini unaweza kufanya kumsaidia aondokane na hali hiyo ili arudi kwenye hali yake ya kawaida

Wanaume naomba tubadilike maandalizi kabla ya tendo la ndoa ni lazima kuanzia leo kama ulikuwa unakwepa hii hatua na unafanya mambo kijeshijeshi tu naomba ubadilike kuanzia leo.

4. Kosa la nne : Kutohakikisha ikiwa wenza wao wamefika kileleni au la

Tendo la ndoa ni mawasiliano ya pande mbili. Kila upande kuna njaa fulani lazima iondolewe.

Tafiti zinasema asilimia 70 ya wanawake wote duniani hawajawahi kufikishwa kileleni na wengine hata hawajuwi hivi kufika kileleni ndiyo kitu gani hasa.

Kwa kawaida hata iweje mwanaume lazima atafika kileleni iwe kwa kuwahi au hata kwa kuchelewa ila lazima atafika kileleni. Tafiti zinaonyesha wanaume wengi wanawahi sana kufika kileleni. Sababu za wanaume wengi kupatwa na tatizo hili ni nyingi ila hilo siyo somo la leo.

Sasa kwa sababu tu wewe mwanaume umefika kileleleni haina maana kuwa na mwenzi wako naye atakuwa amefika kileleni. Na hii ni shida.

Kama mwanaume lazima uhakikishe kwanza kwamba kabla wewe hujafika kileleni basi mke wako naye pia awe amefika kileleni!

Kwahiyo kosa la nne ambalo leo nataka uliache ni hii tabia ya kutokuhakikisha ikiwa mwenza wako naye amefika kileleni au la kabla hujageukia upande wa pili ujifunike shuka ulale.

Ndiyo najuwa wapo baadhi ya wanawake ambao hata ufanye nini bado hawezi kufika kileleni. Kwahiyo ni mhimu kuhakikisha pia kuwa mwenza wako ana akili yenye utulivu na hana mawazo mawazo (stress) yoyote.

Shida kubwa ya kosa hili kwa wanaume ni kuwa wanaume wenyewe asilimia kubwa huwa hawajuwi ikiwa wapenzi wao wamefika kileleni au bado. Ukijua ishara na dalili anazozionyesha mwanamke anapofika kileleni au anapokuwa amefikishwa kileleleni itakusaidia sana kuepuka kosa hili.

Ndiyo mapenzi hayana kanuni maalumu kwa watu wote, pia inategmea na umri na muda gani tayari mmeishi kama mke na mme.

Kuna wakati mwanamke anaweza kukubali kushiriki tendo la ndoa ila kwa ajili yako tu mwanaume yeye muda huo hisia zake zinakuwa hazipo kwa ajili hiyo. Ikitokea hivyo pia itakuwa ni vigumu wewe mwanaume kumfikisha kileleni.


TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU

Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE 

Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya

Comments

  1. Kwakawaida wanawake wanachelewa Sana kufika lakin kuna Mambo unataka kumfanyia yeye mwenye mwanamke anakuwa hayupo tayar na Jambo ambalo unataka kumfanyia wakat mapenz ni furaha

    ReplyDelete

Post a Comment

Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo