UMUHUMU WA MAZOEZI KWA MJAMZITO Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

UMUHUMU WA MAZOEZI KWA MJAMZITOMara nyingi ujauzito huambatana na changamoto mbalimbali, ikiwamo kuumwa mara kwa mara hasa kwa kina mama ambao wanaishi katika mazingira magumu. Pia, kuna kuugua kunakotokana na upungufu wa lishe.

Hata hivyo, licha ya wajawazito kushauriwa kutumia vyakula bora vyenye kila aina ya virutubisho kwa ajili yao na watoto wanaotarajia kuwaleta duniani, suala la mazoezi ni muhimu kwao.
Utafiti unaonesha kwamba wanawake wanaofanya kazi nyingi ngumu katika kipindi cha miezi mitano ya mwanzo ya ujauzito wanakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujifungua salama.

Ingawa utafiti huo umebaini kwamba wajawazito hao wana fursa nzuri ya kujifungua salama, haina maana kwamba hawapaswi kutumia lishe inayotakiwa katika kipindi hicho. Lishe bore katika kipindi cha ujauzito ni suala muhimu lisilohitaji mjadala ili kunusuru maisha ya mama na mtoto.

Kufanya kazi nyingi ngumu kunaweza kusababisha mjamzito kumfanya mtoto aliye tumboni kutonenepa kupita kiasi, hivyo kumsaidia mzazi kujifungua kwa urahisi na salama wakati unapowadia.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Granada cha Hispania unaonesha kuwa, pia wanawake wana fursa nzuri ya kutumia miezi minane ya ujauzito kufanya kazi nyingi bila kujali kwamba wako katika hali hiyo.

Mtafiti kiongozi wa utafiti huo, Dk. Jonatan Ruiz anasema wanawake wanaofanya mazoezi ya kutembea, kukimbia au kurukaruka mara kwa mara katika miezi minne ya mwanzo ya ujauzito wake katika mazingira mazuri ya kujifungua bila kufanyiwa upasuaji kwa kuwa watoto huwa na maumbo madogo.
Dk. Ruiz anasema hata wanawake wasiofanya mazoezi katika kipindi hicho, lakini wakaanza kufanya yale ya kutembea mara kwa mara, mara tatu kwa wiki wakati ujauzito unapokuwa mkubwa, wanaweza kukikwepa kwa urahisi ‘kisu’ siku ya kujifungua.
Anasema kutembea mara tatu kwa siku umbali wa kilometa tatu, kunasaidia kumfanya mtoto aliyeko tumboni asizubae au kulala lala, hali itakayoufanya mwili wake usinenepeane kwa kuwa naye atakuwa kama anafanya mazoezi.

Mtafiti huyo anasema, mtoto mchanga aliyeko tumboni anapotembezwa katika hali hiyo, misuli na ubongo wake huwa kazini muda wote hivyo hawezi kunenepa kiasi cha kumtesa aliyembeba tumboni.
Hata hivyo, Dk Ruiz anaongeza kuwa tatizo huja pale mama anapoamua kupumzika na mtoto humchukua muda mrefu kutulia tumboni kwa vile akili yake hufikiria kuwa anapaswa kuwa mazoezini muda huo.
“inaweza kuchukua hata saa mbili hivi tumboni (mtoto) anacheza cheza na utaratibu huo humtesa mama hasa kama amechoka anataka kupumzika kwa kulala,” anasema.

Utafiti huo umethibitisha kwamba watoto wanaozaliwa na kina mama wenye mazoezi ya aina hiyo, hupungua mara tatu zaidi tofauti na iwapo wazazi wao wasingefanya mazoezi hayo. “kichanga kinapokuwa tumboni huanza kuwaza mambo fulani fulani ya kitoto na iwapo kitawaza kitapungua mwili kama ambavyo mtu mzima anavyowaza na kuwaza na hatimaye kupungua uzito au umbo,” anasema mtafiti huyo.

Dk Ruiz anasema kupungua kwa umbo la mtoto humsaidia mjamzito kutofanyiwa upasuaji kutokana na sababu mbili; kwanza sehemu zake za uzazi huwa zimepanuka kiasi cha kumudu kiumbe kutoka kwa urahisi na pili, mtoto anayetarajiwa kuzaliwa huwa na umbo linaloweza kumfanya atoke kwa urahisi.
Pia utafiti huo unaonesha mjamzito anayefanya mazoezi mara kwa mara hupunguza uwezekano wa kuongeza kupata kisukari, ugonjwa ambao huwatesa zaidi kinamama waliopo katika hali hiyo.

Hata hivyo, kwa wenye dalili za ugonjwa huo inapaswa kujihadhari zaidi, ikiwezekana kwa kuongeza muda wa mazoezi ili kuimarisha uwezekano wa mwili kukabiliana nao na maradhi mengine nyemelezi.
“mara nyingi wajawazito hufanyiwa upasuaji kutokana na watoto tumboni kuwa wakubwa au kukaa vibaya, hivyo kwa kufanya mazoezi tarajia mtoto atapungua na iwapo utakuwa na afya bora utajifungua bila ‘kisu’,” anasema mtafiti huyo.

Katika utafiti huo, inaelezwa mtoto anayezaliwa na mama mwenye mazoezi huwa mjanja zaidi kwa kuwa amezoweshwa tumboni ‘kuruka ruka na kutotulia’.
Hata wakati wa kujifungua, watoto wa namna hiyo hutoka haraka tumboni tofauti na wale wanaozaliwa na kinamama wasiofanya mazoezi.

Utaratibu unaotokana na hamasa ya kufanya mazoezi kwa wajawazito nchini Uingereza unachangia asilimia 25 ya vizazi visivyotokana na upasuaji sawa na zaidi ya watoto 190,000 kwa mwaka ambao ni sawa na idadi ya watoto wote waliokuwa wakizaliwa barani Ulaya miaka ya mwanzoni mwa 1980.

Kabla ya miaka ya 1990 hadi 2000 watoto waliokuwa wanazaliwa nchini humo kwa upasuaji, robo walipoteza maisha kutokana na kushambuliwa kwa urahisi na bacteria katika sehemu za vitovu na hawakuwa na mfumo imara wa ulinzi wa mwili.

Hata hivyo, theluthi ya idadi hiyo walikuwa wakiambulia maambukizi mbalimbali au ugonjwa wa kifua (asthema).
Dk Ruiz anasema hospitali hazipaswi kuwashauri tu wajawazito kuhusu mazoezi, bali zitenge nafasi kwa ajili ya kuwasimamia ili kuwasaidia kujifungua salama.

Daktari wa wanawake na watoto wa hospitali ya Mwananyamala jijini Dar Es Salaam, Dk Godfrey Chale anasema sababu za wajawazito kujifungua kwa upasuaji hutegemeana na tatizo analokuwa nalo mzazi.
“hapana, hakuna uhusiano sababu za uzazi wa upasuaji hutegemea na tatizo la mama kabla ya ujauzito, wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua inaweza kutokea dharura,” anasema.
Dk Chale anasema mazoezi kwa mjamzito yana faida na ni muhimu, isipokuwa
mpaka apate ushauri wa kitabibu kabla hajayaanza. “hata kwa asiyekuwa mjamzito, mazoezi ni muhimu, lakini ni lazima apate ushauri wa daktari kabla ya kuanza ili ushauri huo wa kitabibu uambatane na masharti iwapo mama atakuwa na tatizo la kiafya," anasema.

Comments

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.