DIET YA JUISI YA UKWAJU KWA KUPUNGUZA UZITO HARAKA! Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

DIET YA JUISI YA UKWAJU KWA KUPUNGUZA UZITO HARAKA!Ninaamini kuwa umefika kwenye makala hii kwasababu tayari umesikia kuhusu jinsi juisi ya ukwaju inavyopunguza uzito haraka.
Watu wengi wanafahamu matumizi ya ukwaju katika kutengeneza vinywaji kama juisi ya ukwaju au katika kuongeza ladha kwenye chakula kama kutengeneza chachandu, sosi (sauce) au chutney nk.
Kwenye makala hii utaona faida nyingine nyingi za juisi ya ukwaju pia jinsi inavyosaidia kupunguza unene.

1. UKWAJU KAMA TIBA YA MATATIZO YA TUMBO.

Ukwaju unafahamika kuzuia vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na dawa kama Ibuprofen.
Juisi ya ukwaju pia ina anti-oxidants ambazo husaidia kupunguza inflammation mwilini hivyo kulinda dhidi ya tatizo la inflammation linalotokea kwenye tumbo na utumbo.
INFLAMMATION NI NINI?
Inflammation ni tatizo linalotokea kwenye sehemu fulani ya mwili ambapo husababisha kutokea kwa ishara 5 kwenye sehemu iliyoathiriwa ambazo ni:
 1. Maumivu
 2. Kuongezeka joto
 3. Kubadilika kuwa na rangi nyekundu
 4. Kuvimba
 5. Kushindwa kusogeza mahala palipo husika mf inflammation kwenye goti husababisha ushindwe kusogeza mguu au kutembea vizuri.
Inflammation inaweza kusababishwa na vitu vilivyopo nje kama Kemikali.
Pia inaweza kusababishwa na infection pale vijidudu vinapoingia mwilini.
Chanzo kingine kikubwa cha inflammation ni mfumo wa kinga ya miili yetu.
Kwa kawaida mfumo wa kinga ya mwili hutengeneza sumu kwa ajili ya kuua vijidudu vinavyoingia mwilini ili kutulinda na magonjwa.
Sumu hii haitakiwi kutudhuru sisi bali wale wadudu wabaya.
Lakini kwa baadhi ya watu hutokea kuwa hiyo sumu inafanya kazi kwa wadudu huku pia ikiumiza sehemu za ndani ya mwili hivyo kusababisha inflammation.
Inflammation inaweza kutokea kwenye tumbo na utumbo kutokana na sababu mbalimbali kama vijidudu na pia kinga ya mwili.
Kwasababu ukwaju unafahamika kuwa na anti-oxidants ambazo husaidia kuzuia inflammation, huwa unatumika kuleta nafuu kwa watu wenye matatizo haya.
Matatizo ya inflammation ya tumbo na utumbo ni kama homa ya tumbo (Gastroenteritis), Crohn’s disease nk

2. UKWAJU KUTIBU CHOO NGUMU

Ukwaju una asidi inayoitwa Tartaric acid ambayo hufanya kazi sawa dawa zilizopo katika kundi la dawa aina ya Laxatives ambazo kazi zake kuu ni kutibu constipation.
Laxatives husaidia kuleta choo laini kwa kusababisha utumbo mpana unyonye maji kutoka mwilini na kulainisha choo wakati kikiwa kwenye utumbo mpana.
Pia Laxatives husaidia utumbo mpana kujikaza ili choo kipite kiurahisi.

3. JUICE YA UKWAJU NA KISUKARI

Inafahamika kwa watu wengi sana kwamba juisi ya ukwaju husaidia kucontrol sukari kwenye damu.
Hii ni kwasababu ukwaju una asidi inayoitwa Acetic acid ambayo huenda kujijumuisha kwenye mfumo wa asili wa mwili wa kucontrol sukari kwenye damu.
Watu wenye kisukari hupata unafuu kwa sababu ya hii tabia ya ukwaju kushusha sukari.
Lakini tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwani sukari inaweza kushushwa sana hadi kuleta madhara pia.
JUISI YA UKWAJU INAYOSAIDIA KUPUNGUZA UNENE

4. JUISI YA UKWAJU KWA MAMA WAJAWAZITO

Kutokana na uchungu wake na tabia ya kuupa afya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, juisi ya ukwaju imekuwa ikitumika sehemu nyingi duniani kusaidia kupunguza tatizo la kichefuchefu na kutapika kwa wamama wajawazito.

5. JUISI YA UKWAJU NA KIFUA/MAFUA NA HOMA

Tafiti nyingi zimeonesha kuwa ukwaju una tabia sawa na dawa zinazoua vijidudu vinavyosababisha magonjwa mfano Bakteria na parasites wanaosababisha malaria. ( 1 , 2 3 )
Watu wengi hutumia juisi ya ukwaju mara tu mafua na kifua yanapotaka kuanza ili kuondoa kukereketa shingoni pia kuondoa homa.

6. JUISI YA UKWAJU KWA KINGA YA KISEYEYE

Kiseyeye ni ugonjwa unaoletwa na upungufu wa vitamin C mwilini.
Ukwaju una kiasi kikubwa wa vitamin C hivyo kukinga dhidi ya ugonjwa huu.

7. JUISI YA UKWAJU HUUA MINYOO YA TUMBONI

Watu wengi duniani wamekuwa wakiwapa watoto ukwaju ili kuua minyoo.
Tafiti za kisayansi zinakubaliana na hili na kuthibitisha kuwa kweli ukwaju hasa majani na gome la miti wake huua minyoo. ( 4 )

8. JUISI YA UKWAJU KAMA TIBA YA MATATIZO YA INI

Ukwaju una Vitamin A,B,C,E, K ambazo ni muhimu sana katika kuimarisha afya ya ini.
Una 12% ya vitamin B3 (Niacin) ambayo ni muhimu sana kwa ini.
Pia antioxidants zake kama Flavonoids, Vitamin C na Beta Carotene hufanya kazi pamoja kulinda ini.

9. JUISI YA UKWAJU NA AFYA YA MOYO NA MAUNGIO.

Antioxidants husaidia kuzuia inflammation kwenye moyo na mishipa mikuu inayopeleka damu kwenye moyo pamoja na maungio kama magoti nk
Pia ukwaju hupunguza kiasi cha mafuta na cholesterol kwenye damu pamoja na kushusha pressure ya damu hivyo kuzidi kuimarisha afya ya moyo. ( 5 )

10. JUISI YA UKWAJU NA MMENG’ENYO WA CHAKULA

Ukwaju unasaidia utengenezwaji wa nyongo mwilini ambayo ni muhimu sana katika kukamilisha mmeng’enyo wa chakula.

11. UKWAJU DHIDI YA KUKAUKA MACHO

Tatizo la kukauka macho huwapata watu wengi ambapo macho hushindwa kutengeneza machozi ya kutosha.
Kutokana na hili waathirika hujikuta wakipata maumivu sana wakifungua macho yao kana kwamba kuna mchanga ndani yake.
Mbegu ya ukwaju zina kemicali ambayo inafanana sana na ile inayotumika kutengeneza unyevu wenye kunata kwenye macho hivyo kusaidia kuondoa tatizo hili. ( 6 , 7 )
Zipo dawa nyingi za matone kwa ajili ya tatizo hili ambazo zimetengenezwa kwa mbegu za ukwaju. ( 8 )

12.UKWAJU NA VIDONDA VYA KUUNGUA

Kama tulivyoona mapema kwenye makala hii ukwaju unaweza kuua vijidudu kama bacteria na parasites.
Kwasababu vidonda vingi huweza kupata maambukizi ya vijidudu hivi kirahisi utumiaji wa ukwaju kwa kupaka eneo lililoungua mara baada ya tukio husaidia sana kuepusha maambukizi na kusababisha kupona haraka.
Pia ukwaju una kemikali zinazosaidia seli za mwili kuongezeka hivyo kupaka kwenye kidonda hufanya seli za ngozi kujitengeneza tena hivyo kuziba kidonda na ngozi kurudi katika hali ya zamani.

13. JUISI YA UKWAJU DHIDI YA CANCER

Kila wakati kwenye miili yetu kuna seli mpya zinazotengenezwa na kuna seli zilizozeeka zinazokufa ili kufanya mwili uwe na afya.
Cancer hutokea pale seli za mwili zinapozidi kuongezeka kasi isiyoya kawaida bila seli za zamani au zilizozeeka kufa.
Kwenye ukwaju kuna Polysaccharides ambazo huzuia cancer kwa kusababisha seli zilizozeeka zife ili seli mpya zifanye kazi kawaida.

14. JUISI YA UKWAJU INAVYOPUNGUZA UZITO

Ukwaju unasemekana kusaidia kupunguza uzito kwa njia kuu 2.

Kupunguza hamu ya kula:

Ukwaju una asidi inayojulikana kama Hydroxycitric acid (HCA).
Hii husaidia kupunguza uzito kwa kupunguza hamu ya kula hivyo kukuzuia kula kiasi kikubwa sana cha chakula kuliko mahitaji ya mwili wako.

Kupunguza mafuta mwilini:

HydroxyCitric acid pia hupunguza kasi ya uhifadhi wa mafuta mwilini kwa kuingilia kazi ya enzyme inayosababisha kubadilishwa kwa chakula kuwa mafuta mwilini (ATP Citrate lyase).

JINSI YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU

 1. Osha ukwaju kwa maji yanayotiririka kisha ondoa ganda la nje.
 2. Weka maji kiasi unachotaka kwenye sufuria kisha uchemshe ukwaju wako kwa dakika 10-15.
 3. Ipua kisha koroga ukwaju uwe kama uji uji.
 4. Chuja Juisi yako ya ukwaju na uweke sukari kidogo au asali.
 5. Hifadhi kwenye fridge tayari kwa kunywa.

JINSI YA KUNYWA JUISI YA UKWAJU KWA AJILI YA KUPUNGUZA UZITO

Watu wengi hudai kuona matokeo baada ya kunywa glasi moja kabla ya kila mlo.
Kuna watu ambao wapo sensitive sana kiasi cha kuwa hata nusu glasi inaweza kufanya waharishe sana.
Hakikisha unapata ushauri wa daktari wako kwanza pia sikiliza mwili wako, kama unaharisha sana basi punguza kiasi au ongeza maji kwenye juisi yako.

MAPUNGUFU YA VITHIBITISHO VYA JUU YA UKWAJU KUPUNGUZA UZITO

 1. HAKUNA TAFITI ZILIZOFANYWA KWA BINADAMU: Tafiti zote zilizofanywa juu ya jinsi juice ya ukwaju inavyopunguza unene zimefanywa aidha kwa PANYA au KUKU aina ya BROILER.
 2. JUISI YA UKWAJU HUSABABISHA KUHARISHA : Kwasababu ukwaju una tabia kama za dawa za laxative huwa unasababisha mtu apate choo laini sana mara nyingi kwa siku. Hii husababisha kutoka uchafu kwenye utumbo mpana hivyo kufanya mtu aonekane amepungua tumbo. Pia kuharisha husababisha kupunguza uzito wa maji mwilini. Hivyo inawezekana kunywa juice ya ukwaju kunasababisha kupungua haraka kwa sababu hii.
KWA KIFUPI:
Inawezekana ni kweli juice ya ukwaju husaidia kupunguza uzito hasa tumbo kutokana na upungufu wa uchafu kwenye utumbo mpana,upungufu wa maji pamoja na kupunguza kiasi cha chakula.
Lakini ni muhimu kukumbuka ukipunguza uzito haraka hasa kwa kuharisha una uwezekano wa zaidi ya 95% wa kurudisha uzito uliopoteza tena na nyongeza ndani ya muda mfupi pia.
Kazi ya ukwaju katika kupunguza utengenezwaji mafuta yanayokaa chini ya ngozi umeonekana kuwa ni ya muda mfupi tu na kiasi kinachozuiwa ni kidogo.
Itabidi tafiti mpya zifanywe kwa binadamu ili kuhakikisha kama kweli diet ya juice ya ukwaju husababisha kupunguza uzito kwa binadamu.

TAHADHARI: MADHARA YA JUISI YA UKWAJU

1.Watu wenye kisukari, wamama wajawazito, wamama wanaonyonyesha na watu wanaokaribia kufanyiwa operation wapate ushauri wa daktari kabla ya kunywa juisi ya ukwaju.
2.Usitumie juisi ya ukwaju ukiwa katika dozi ya ASPIRIN au IBUPROFEN kwasababu ukwaju hufanya kiasi kikubwa kuliko kawaida cha hii dawa kuingia kwenye damu hivyo kufanya usikie zaidi yale madhara ya hizo dawa.
Mwisho kabisa faida za kunywa juice ya ukwaju ni nyingi sana kwa hiyo hata kama ni kweli inasaidia kupunguza uzito au la ni kinywaji kizuri kwa afya.
Cha muhimu ni kukumbuka kutotegemea mbinu fupi za haraka za kupunguza uzito.
Badala yake ni muhimu kufata njia na misingi sahihi ya kupunguza unene ambayo ni lishe sahihi na mazoezi ya viungo.
Je umewahi kutumia juice ya ukwaju kwa ajili ya kupunguza uzito? Matokeo yako yalikuwaje?

Comments

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo