UGONJWA MBAYA ZAIDI "HASIRA" Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

UGONJWA MBAYA ZAIDI "HASIRA"Hasira ni ono linalowapata binadamu na wanyama mbele ya kipingamizi. Katika hali hiyo mtu hughadhibika, hata kuchukia kwa kupatwa na kitu ambacho yeye mwenyewe hapendi.
Mtu mwenye hasira ya mara kwa mara, hushauriwa ajaribu kuepuka mambo au vitu vinavyomuudhi, kwa mfano, anaweza kuondoka mahali penye maudhi, na kama ni kubishana aweze kunyamaza ili kuepukana na ugomvi.
Pia inashauriwa kuwa, kama unajua mwenzio hukasirishwa na kitu fulani, bora usimchokoze, kwa sababu ni hatari kwa maisha yako maana kwa hasira yake anaweza kufanya kitu chochote kibaya.
Isiporatibiwa na mhusika inaweza ikasababisha madhara makubwa, inavyofundisha mithali ya Kiswahili, "Hasira, hasara". Hasira hupelekea mtu kuvunja sheria kwa kujichukulia hatua mkononi na mwishowe kufanya jambo la hatari.
Ndiyo sababu inahesabiwa kati ya vilema vikuu ambavyo ni mizizi ya dhambi nyingine.

NI NINI CHANZO CHA HASIRA
Acid ni kemikali ambayo ni hatari sana,kemikali hii inapowekuwa katika chombo huathir zaidi
chombo hicho kuliko vitu vingine vyote vilivyopo jirani na chombo hicho.
Vivyo hivyo ndivyo mtu anapokuwa na hasira,kwani hasira ni hali ambayo humuathiri zaidi
aliyenayo kuliko mtu mwingine zaidi,kwani maumivu ya hasira huyapata yle aliyenayo zaidi
kuliko aliyechanzo cha hasira hiyo.
Kila kiumbe aliye hai hupatwa na hasira,yaani wanyama,ndege na hata wadudu wote hupatwa
na hasira.Hivyo hasira ni hali isiyoepukika katika hali ya kawaida.
Mwanasaikolojia T.W Smith yeye alisema kuwa,hasira ni muhemko usio epukika,muhemko
huu unaotokana na hisia hasi juu kitu,jambo au hali fulani.Nuhemkohuu hutofatiana kutoka
katika hali ya kawaida hadi katika hali inaweza kusababisha madhara kwa mtu binafsi na hata
kwa watu wengine.
Binadamu ndiye kiumbe amabaye hupatwa na hasira mara kwa mara kuiko viumbe wengine
wote,na hasira hii huchukua muda mrefu hadi kuisha,na hii hutegemeana na uwezowa mtu wa
kuzuia hasira hiyo.Hali hii huonekanani ya kawaida sana na ya kuzoeleka kwa kuwa
husababishwa na hisia juu ya kitu fulani,na kawaida ya hisia hubadilika muda baada ya muda.

Katika maisha ya kila siku tunakutana na mambo mengi sana ambayo kwa namna moja au
nyingine na kwa mitazamo tofauti tunayokuwa nayo,yanaweza kusababisha au kupelekea mtu
kupatwa na hasira.
Haijalishi jambo lina uzito au udog kiasi gani,lakini jambo hilo linapokupa au kukuamshia hisia
tofauti na ulivyotegemea hasira huweza kutokea mara moja.Hivyo hasira kwa kiasi kikubwa
husababishwa na hisia juu ya mambo haya yafuatayo:
Kuumizwa kwa njia yoyote ile bila sababu yoyote ile,hiihutokea zaidi katika mahusiano
hasa ya kimapenzi.
Kulazimishwa kufanya jambo au kitu usichokipenda
Kutokutendewa haki unayostahili bila kujalisha ni kweli ama si kweli.
Vitisho na mawazo ambayo hupendezwi nayo katika maisha yako.
Msongo wa mawazo pia ni chanzi kikubwa cha hasira,kwani mtua anapopata msong wa
mawazo maana yake anakua na mkusanyiko wa mambo mengi sana kichwani ambayo
yamekosa suluhisho la kuyapunguza. Hivyo anakuwa na uwezo wa kufanya chochote
atakachoamua,hivyo hasira zake zipo karibu zaidi.
Kukataliwa katika jambo au mambo ambayo huamini kuwa na thamani katika maisha
yake ya kila siku.
Pamoja na sababu nyingine nyingi ambazo hutofautiana kati ya mtu na mtu,na huwa na hisia
otfauti,huweza pia kupelekea mtu kupatwa na hasira.
Kumbuka:Kitu kinachoweza kukufanya wewe kupatwa na hasira za mara kwa mara,kinaweza
kumfanya mtu mwingine kuwa na furaha au kuwa katika hali ya kawaida.Hii yote hutokana na
tafsiri juu ya jambo fulani ambapo tafsiri hiyo hupelekea kupatwa na hisia tofauti na
uliyoitegemea katika jambo lile,na mwisho wake hupelekea kupatwa na hasira.Na hali huweza
kupelekea ugumu katika kuielewa na kuizia hasira.

Nini Matokeo ya hasira
Hasira ni hali inayoweza kuzuilika,lakini pia kuna wakati hasira hushindwa kuzuilika na
hatimaye mtu hukutana na changamoto zifuatazo katika mazingira tofauti:
Kushindwa kupata suluhisho la matatizo mbali mbali unayokutana nayo katika maisha
ya kila siku.
Kushindwa kufanya maamuzi sahihi pale unapokutana na hali inayohitaji maamuzi.
Kushindwa kujenga na kuimarisha mahusiano yaliyo imara na bora zaidi,haijalishi ni
mahusiano ya aina gani.
Lakini pia mtu mwenye hasira za mara kwa mara huweza kuathiriwa kiafya na kujikuta
amedhoofika sana

Kuna utaflti uliofanywa na wasomi wa saikolojia huonyesha kuwa,mtu aliye na hasira za mara kwa mara 
huweza kupatwa na matatizo mengine kama vile;Ugonjwa wa moyo(Cardinal heart disease),matatizo ya 
kula(Eating disiorder).

Jinsi yaKuzuia Hasira
Unaweza kuzuia hasira yako pale unapoweza kuitambua mapema kabla haijawa na madhara kwako na kwa 
wengine pia.Hizi ni baadhi tu ya njia utakazoweza kutumia kuweza kuzuia hasira yako pindi 
utakapotambua kuwa imekaribia kuwa na madhara.
Tambua na kubali kuwa una tatizo,na hapo ndipo anza kupangajinsi ya kukabiliana hna hilo tatizo.
Tambua na uelewe kwa umakini na utulivu wa hali ya juu chanzo au vyanzo vya hasira yako kwa mtazamo 
chanya.
Shirikisha watu wako wa karibu na unaowaamini zaidi juu ya tatizo ulilo nalo,famili na raflki zako 
wa karibu ndio watu wa muhimu zaidi.
Ingilia na zuia mzunguko wako wa hasira pale utakapoanza kuhisi hasira hasa kwa kutumia mbinu 
tofauti(Relaxation techniques) kama kuvuta hewa ndani kwa muda na kuitoa taratiiibu.
Chukulia tatizo linalikupa hasira kam ni la mwenzako na uhisi kama ni 
yeye,ungelichukuliaje(Empathy).Kumbuka kila mtu hukosea,na kupitia kukosea tunajifunza.
Weka na tengeneza furaha katika maisha yako,na uchukulie changamoto kwako kama ni ushindi.Hapo 
utakua umeshinda kila kitu.Jifunze kucheka na kufurahi kila siku.
Jifunze kuwa msikivu na muelewa kwa kila kitu,kwani kutofautiana katika mawasilia ni chanzo pia cha 
hasira.
Siku zote kuwa na kiasi kwa kila unachokifanya,heshimu unachokipenda na uheshimu pia uhitaji wa 
mwenzio.
Jifunze kuishi kwa muda na kufanya maisha yako kama yapo katika siku za mwisho.Kumbuka maishani 
mafupi sana,unapotumia muda mwingi kuwa na hasira unapunguza kwa kasi kubwa sana hizo siku zko 
chache zilizobaki.
Mwisho,SAMEHE NA SAHAU.

Comments

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo