Asali ni chakula muhimu sana kinachousaidia mwili katika kupambana na magonjwa mbalimbali pamoja na matatizo mengine yatokanayo na uzee.
Tafiti za wataalamu mbalimbali wa madawa lishe na vifaa tiba duniani zimedhihirisha kwamba uwezo wa asali katika kutibu huongezeka maradufu kama itachanganywa na mdalasini.
1. Asali ikichanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.
2. Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini.
3. Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino, inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni dawa asilia ya shinikizo la juu la damu ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa asilimia kubwa ya madawa mmimiko na asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya kupaka.
4. Ugonjwa wa mafua ambao huwakera na kuwanyima watu wengi raha unaweza kupungua na kupotea kabisa ikiwa watatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa chafya na kuvimba kwa koo.
5.Asali na mdalasini huaminika pia kuamsha hamu ya tendo la ndoa endapo itatumiwa kwa kunywa vijiko viwili vya mezani kila siku kabla ya muda wa kulala usiku.
6.Asali na mdalasini husaidia katika kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji.
7.Asali na mdalasini husaidia kupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
8. Ulaji wa asali pamoja na mdalasini husaidia kuondoa mchafuko wa tumbo uletwao na gesi.
9. Matumizi ya mara kwa mara ya asali na mdalasini wakati wa kifungua kinywa husaidia kuzuia uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku