DONDOO 85 ZA AFYA Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

DONDOO 85 ZA AFYA1. Asilimia 50-90 ya mwili wa kiumbe hai ni maji. Hivyo mtu anaweza kupoteza uhai kwa haraka zaidi kwa upungufu wa maji. Tende zina oxytocin hii husaidia katika kurahisisha mama wakati wa kujifungua.Hivyo ni vyema mjamzito kutumia tunda hili. Pia tende huongeza kiwango cha maziwa.

2.Hakuna madhara kwenye mafuta ya samaki, isipikuwa kunafaida kubwa. Katika mafuta haya kuna omega3 fat acidi. Hii hujulikana kwa uwezo wake wa kuupa mwili nguvu na uwezo wa kufanya kazi. Pia husaidia katika michakato ya kikemikali mwilini.

3. Ulaji wa samaki hupunguza hatari ya kupata matatizo ya magonjwa ya moyo shambulio la moyo.

4. Kufanya mazoezi ni jambo lililolazimishwa na wataalamu wa afya. Angalau kwa wiki mtu afanye mazoezi. Mazoezi huweza kuupa mwili afya na uwezo wakupambana na maradhi.

5. Usinywe maji punde utokapo masoezini, subirika kidogo kama dakika kadhaa mwili kupoa.

6. Hakikisha unapofanya mazoezi jasho likaukie mwilini hasa kwa wale wenye tracksut. Jasho husaidia kukausha mafuta yaliyoganya kwenye ngozi.

7.Kuoga pia ni lazima kwa mwanadamu, kuoga husaidia kuondoa stress yaani misongo ya mawazo.

8. Kuoga ni tiba ya matatizo ya kisaikilojia.

9. Katika ulimi wa mwanadamu kuna  bakteria, hawa husaidia katika kuzuia hatari ya vyakula vyenye sumu hasa vile vyenye nitrate kama nyama.

10.Ni vyema kupata muda wa kutosha kwa ajili ya kulala. Mwili huhitajia muda huo kwa ajili ya kurekebisha mifumo ya mwili na kupona kwa majeraha, pia nakupumzika.

11. Mtu anapolala huwa anageuka geuka, kitendo hiki ni muhimu kwa ajili ya afya. Kama mgonjwa hawezi kugeukageukja anatakiwa ageuzwe upande kila baada ya muda.

12. Wakati wa usiku mwili hutoa homini iiitwayo melatonin. Hii husaidia katika kuuandaa mwili kulala. Mapigo ya moyo hushuka.

13. Kutokupata muda wa kutosha kulala kunaweza kusabababisha mwili kupoteza uwezo wake wa kupambana na maradhi.

14. Kama mtu atakosa muda wa kulala kwa usiku miwili anaweza kupoteza uwezo wa kufanya kazi kwa ufasaha na kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri.  Mtu akikosa muda wa kulala kwa miusiku mitatu atapata matatizo ya kuona maluelue na atapoteza uwezo wa kufikiri vizuri.

15.Utafiti uliofanywa marekani umeonesha kuwa watu ambao hawana dini au imani ya mungu wapo hatarini kwa asilimia 60% kupata magonjwa ya moyo kuliko ambao wana imani.  Pia wataalamu hawa wa Saikolojia wakaongeza kuwa watu wasio na dini maisha yao ni mafupi sana kuliko qenye dini. Halikadhalika watu hawa wanasumbuliwa na maradhi mara kwa mara.
Pia tafiti nyingine zimeonesha kuwa watu ambao wanasamehe au wana uwezo wakusamehe wanakuwa na afya njema ya mwili na akili kuliko ambao hawasamehe au hawana uwezo wa kusamehe. Hivyo ni vyema kujifunza kusamehe. Pia wameongezea kuwa hasira ni hatari kwa afya ya moyo

16.Maji hutumika kupooza ingini. Halikadhalika hutumika kupooza mwili pia.

17.Upungufu wa vitamini A hupelekea kukauka kwa ngozi, uoni hafifu na kuathirikakwa koo na ngozi.

18.Upungufu wa vitamin B1 hupelekea kukosa hamu ya kula, udhaifu wa miguu,kupungua kwa hisia kwenye neva kudhoofu kwa misuli na kuathirika kwa akili.

19. Upungufu wa Vitamin B2 hupelekea kupata ugonjwa wa pellagra yaani vidonda vya mdomo na ulimi, ukuaji hafifu, kupasuka kwa nbgozi hasa sehemu za sikio na pua.

20.Upungufu wa Vitamin B12 husababisha matatizo katika uzalishaji wa seli hai nyekundu za damu, na kusababisha aina ya ugonjwa wa anaemia.

21. Upungufu wa vitamini C husababisha kutoka damu kwenye finzi, kuchelewa kupona kwa majeraha, maumivu ya viungo na kudhoofu kwa mishipa ya damu hasa kwenye ngozi.

22. Upungufu wa vitamin D husababisha kuleta matege.

23.Upungufu wa vitamin k husababisha kuchelewa kuganda kwa damu kwenye jeraha

24. Upungufu wa madini ya Iodine hupelekea kupata ugonjwa wa Goitre yaani kukuwa kwa tezi ya thyroid.

25. Upungufu wa madini ya potasium hupelekea udhaifu wa misuli kutokuweza kukunja kwa ufasaha.

26. Upungufu wa madini ya magnesium hupelekea utengenezwaji hafifu wa meno na mifupa na misuli hishindwa kukunja kwa ufasaha.

27. Upungufu wa madini ya sodium husababisha kukaza kwa misuli.

28. Upungufu wa madini ya clorine hupelekea mwili kushindwa kuzalisha asidi ya hydrocloric. Asidi hii husaidia katika mmeng’enyo wa chakula mwilini.

29. Upungufu wa madini ya phosphorous hupelekea udhaifu wa meno na mifupa na mwili kwa ujumla.

30.Madini ya calcium ya kipungua mwilini husababisha udhaifu wa meno na mifupa.

31.Katika mambo yanayopunguza kinga ya mwili yaani uwezo wa mwili kupambana na maradhi ni misongo ya mawazo, utaratibu mmbovu wa lishe au kutopata lishe bora na mlo kamili, mazingira na madawa.

32. Upigapo chafya ziba mdomo kwa kitu kilicho safi.

33. Kwa mama anayenyonyesha ahakikishe ziwa lake halina kemikali yaani losheni au mafuta ili mtoto asije nyonya kemikali zile.

34.Ugonjwa wa mnjano yaani hepatitis B ni katika magonjwa yanayouwa watu wengi duniani. Karibia watu 620,000 hufa kila mwaka, na karibia watu milioni 350 wameathirika na ugonjwa huu. (WHO). Ugonjwa wa manjano husababishwa na vitusi viitwavyo Hepatitia b (HBV) ambao hawa hushambulia ini na kusababishwa uvimbe. Uvimbe huu unapelekea kupatakansa ya ini. Njia ambazo ugonjwa wa manjano huambukizwa ni sawa na zile za kuambukizaUKIMWI. Dalili za ugonjwa wa manjano huchelewa kuonekana, na huonekana pale mtu anapokuwa ameshaathirika. Dalili hizo ni kama kukojoa mkojo wa rangi nyeusi,macho na ngozi kuwa njano, kichefichefu cha mara kwa mara, kupungua uzito, homa kali, mwili kuwa dhaifu, kupoteza hamu ya kula na maumivu makali ya tumbo karibu na ini.

35.Mbegu za maboga zinaweza kuwasaidia watu wanaoishi na kisukari. Mbegu hizi zimeonekana kuwa na uwezo wa kusaidia kurekebisha kiwango cha insulin. Madini ya zinc yaliyomo kwenye mbegu za maboga husaidia kuboresha afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu.

36. Karanga pia husaidi afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu. Kuna vitamin E kwenye karanga, hivi ndivyo vina kazi hii.

37. Mshubiri ni katika tiba za asili sana. Husaidia kuondoa miwasho kwenye ngozi.Pia kuponesha vidonda na michubuko kwnye ngozi. Kata jani lake kisha jipake kwenye jeraha, mchubuko au muwasho.

38.Na muarobani nao pia hutibi maumivi ya sikio , maradhi ya macho na miwash yangozi. Changanya mwarobaini uliopondwa na asali kisha weka tone moja wenye sikio.Fanya hivyo kwa siku kadhaa utapona.

39.Tende ni katika matunda ya asili na ni katika matunda yanayoweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kwa njia za asili. Wataalamu wa afya wanazungumza kuwa karibia virutubisho vyote anavyohitajia mwanadamu kuishi vinaweza kupatikana kwenye tende. Pia wataalamu wanaongeza kuwa mtu anaweza kuishi kwa muda mrefu kwa kula tende kokwa chache tu na glasi ya maziwa.

40.Maziwa ni katika vinywaji vya asili pia. Maziwa ya mama yanafahamika kwa ubora wake na umuhimu kwa watoto wachanga. Wataalamu wa afya wanasisitiza kuwa nyonyesha watoto kwa muda wa miaka miwili. Halikadhalika maziwa ya ng’ombe na wanyama wengine kama ngamia na mbuzi yamekuwa yakitumiwa sana na watu wazima. Watu wamekuwa wakinywa maziwa kwa ajili ya kuondoa sumu.Halikadhalika maziwa yana virutubisho muhimu na ambavyo mwanadamu anahitajia.Wagonjwa wa vidonda vya tumbo wanashauriwa sana kunywa maziwa.

41.Asali pia ni katika vyakula na vinywaji vya asili. Ukiachilia mbali virutubisho vingi sana vilivyomo kwenye asali, lakini asali pia huweza kutumika kama dawa.Kwa walioungua hupaka asali kwenye jeraha. Asali ina uwezo mkubwa wakuuwa bakteria kwenye kidonda.

42.Nyama ni katika vyakula vyenye protini. Watu wengi hupenda kula vyama.Wapishi wa nyama wanapashwa kuwa makini kwani vyama inatakiwa iiive na kama haitaiva walaji wanaweza kudhurika kama mnyama atakuwa na vijidudu. Vyama vyekundu kama ya ng’ombe na mbuzi zimekuwa zikipatikana zaidi. Lakini wataalamu wa afya wanapendelea zaidi ulaji wa nyama nyeupe kama nyama ya samaki, kuku n.k.

43. Samaki ni katika vyakula vya asili pia. Wataalam wa afya wanaeleza kuwa ukuaji salama wa ubongo kwa mtoto unaweza kuwa maradufu kama mtoto atakuala samaki. Wataalamu wa afya wanasisitika kula samaki akiwa katika supu ama namna nyingine.Mafuta ya samaki ni katika sehemu muhimu inayopasa kuliwa kwenye samaki.

44.Ni vyema kula matunda ukiwa una njaa kabla ya kula chakula. Ulaji wa matunda ukiwa na njaa utapelekea mmeng’enyo wa lile tunda kukamilika wote na kuingia kwenye mfumo wa chakula.

45.Ijapokuwa watu wengi hawapendi pilipili ila itambulike kuwa tunda hili ni zuri na lina vitamini ambavyo vinasaidia katika ukuaji wa ubongo.

46.Matunda yenye rangi ya njano kama maembe na machungwa yana kiasi kikubwa cha vitamikni C. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vitamini hivi ini mujarabu katika kuulinda mwili dhidi ya maradhi mablimbali.

47.Mimea yenye rangi a kijani yaani mboga ina vitamini A. Vitamini hivi pia vina kazi ya kuulinda mwili na maradhi. Matatizo ya kutokuona usiku ni kutokana na upungufu wa vitamini hivi.

48.Ni vema kupiga mswaki kabla ya kulala. Ukilala na mabaki ya chakula mdomoni unaweza kukaribisha bakteria kuzaliana kwa kiasi kikubwa kwenye kinywa chako.Hali hii inaweza kuleta madhara katika afya ya meno yako.

49. Vyakula vya mafuta huchangia kwa kiasi kikubwa kupata maradhi ya moyo hususani shinikizo la juu la damu yaani presha ya kupanda au shambulio la moyo yaani heart attack. Sababu kuu ni kuwa vyakula hivi husababisha mgando wa mafuta kwenye mishipa ya damu na kuifanya mishipa hii iwe na tundu nyembamba za kupitishia damu. Na hapa ndio panapoleta shinikizo la damu la kupanda. Wataalamuwa fizikia (physics) wanatambua kuwa eneo likiwa dogo basi presha huwa kubwa.Yaani kwa kuwa tundu za mirija zimekuwa nyembamba basi damu huwa na presha kubwa.

50. Uvutaji wa sigara huweza kuathiri afya ya mvutaji na hili halina tabu kabisa maana imeandikwa kwenye maboksi ya sigara na sigara zenyewe kuwa UVUTAJI WASIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO. Ila pia ijulukane kuwa hata mtu aliyepembeni ya mvutaji anaathirika kwa kiasi pia.

51. Ni vyema kunywa maji ya moto hususani asubuhi au ukiwa unaumwa. Hii ni kwa sababu maji ya moto hayahitaji kupashwa joto tumboni. Pia wataalamu wa afya wanasisitiza sana kunywa maji ya moto hasa wakati wa asubuhi.

52. Si vyema kulala na maua ya makopo ndani. Yaani kama umepanda maua kwenye makopo si vyema ukalala nayo ndani. Kwani mimea wakati wa usiku huvuta hewa ya oksijeni ambayo wanadamu huvuta. Hivyo kitendo hiki kitasababisha mminyano wa kugombea hewa wewe na mmea. Hivyo hewa huenda isitoshe kuhudumia mmea na wewe kwa pamoja.

53.Ijapokuwa sukari na chumvi ni muhumu kwenye maisha yetu, lakini inashauriwa tusitumie sukari nyingi au chumvi nyingi. halikadhalika kwa watoto sio jambo jema sana kupenda kuwapa vitu vya sukari kwa wingi kama pipi, peremende n.k. Kwani huenda vikasababisha madhara katika meno yake.

54.Ulaji ulio salama ni kati ya kushiba na kuwa na njaa. Yaani mtu anatakiwa kiafya asishibe sana kiasi cha kushindwa kujimiliki kama kukimbia n.k hivyo ale kwa ukati na kati.

55.Mtu anatakiwa ale kwa wakati alojiekea. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa miongoni mwa sababu za vidonda vya tumbo ni kuto kula kwa wakati. Mwili huwa unakawaida ya kujua wakati wa kula ambao huwa unakula. Hivyo unapofika wakati ule kuna majimaji yanazalishwa ili kuliandaa tumbo. Na kama majimaji haya yasipokutana na chakula yanaanza kukwagua kuta za tumbo na kuleta vidonda kama hali hii itaendelea kwa muda mrefu.

56. Unywaji wa maji ni jambo la muhimu sana kwa afya. Wataalamu wa afya wanasisitiza sana, kwani maji yanaweza kupunguza hatari za ugonjwa wa UTI, maumivu ya kichwa na kurekebisha migongeo ya chakula tumboni.

57.Mtu anatakiwa atumie muda katika kutafuna chakula. Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa mmeng’enyo wa chakula huanza rasmi mdomoni ambapo vyakula vya wanga huanza kumeng’enywa. Hivyo kama mlaji hatatafuna vizuri huenda asipate virutubisho kwa usahihi.

58. Unaweza ukadhibiti maradhi mbalimbali na mengi kwa kupangilia kula tu. Kwa msaada wa kanuni za afya unaweza kupambana na matatizo mengi ya kiafya kwa kurekebisha ulaji na kula kama inavyotakiwa. Kwa mfanoA)kizazi yaani nguvu za kiumeB)KisukariC)SarataniD)Vidonda vya tumbo.

59.Sio vizuri kulala ukiwa na jiko la mkaa likiwa lina moto. Wataalamu wa elimu za viumbe wanaeleza kuwa moto wa mkaa unatumia gesi ya okijeni kuwaka na badala yake hutoa gesi ya kabon monoksaid. Gesi hii huweza kuungana na oksijenikutengeneza kabondaioksaid. Hivyo hali hii itapelekea matumizi makubwa ya gesi ya oksijen ambayo mwanadamu atakuwa anatumia. Kama yupo chumbani anaweza kukosa hewa kabisa ikiwa chumba ni kidogo.

60.Si vyema kuvaa nguo nyingi na za kubana. Watu wengi leo wanasumbuliwa nafangasi sehemu za siri na hujikuna sana. Wadudu hawa wanapenda sana sehemu za majimaji hasa za siri. Hivyo nguo nyingi husababisha jasho sehemu za siri na kuwafanya wadudu hawa kupata mazingira mazuri.

61. Si jambo jema kuvaa nguo mbichi hasa sile za ndani. Jambo hili kiafya si jema kwani linaweza kuwafanya fangasi waliopo sehemu za siri kukuwa vizuri nakumfanya mtu ajikune kwa muwasho.

62. Unapojisikia haja ndogo au kubwa ni vizuri kuwahi haraka kwenda kuitoa. Haja kubwa au ndogo inaweza kupelekea matatizo ya kiafya kama haitatolewa kwa muda unaotakiwa.

63. Kuwahi kutoa haja kubwa kunaweza kupunguza athari za UTI kwani unapokojoa unawatowa wadudu wa UTI.

64.Haja kubwa ikichelewa kutolewa inakuwa ngumu kwani mwili utaendelea kufyonza majimaji yaliyopo kwenye haja kubwa. Haja hii ikiwa ngumu inawezakusababbisha mipasuko au michubuko kwenye njia na kusababisha damu.

65.Sio jambo jema kubana upepo (ushuzi). Kwani upepo huu unatakiwa utoke nje kwa muda ule. Halikhalika kijamii sio vyema kujamba mbele za watu.

66.Pindi ukipata majeraha si vyema kufyonza damu kwa mdomo. Kwani damu ile sio salama. Ni damu ambayo imekusanya vitu vingi kama urea, seli, plasma, homone n.k.Hivyo si vyema kuila damu hii.

67. Unaposikia maumivu ya kichwa kunywa maji mengi, huenda ni kutokana na upungufu wa maji.

68. Ni vyema kupiga mswaki zaidi ya mara moja kwa siku. Na huu ni ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ya kinywa.

69. Kunywa maji mengi hakuna madhara yeyote, ila kutokunywa maji mengi kuna madhara mengi zaidi.

70. Ni rahisi kwa wanawake kupata UTI kuliko wanaume. Ni kwa sababu wanawake mirija yao ya haja ndogo ni midogo, halikadhalika sehemu zao za haja ndogo na kubwa zipo karibu hivyo ni rahisi kwa vijidudu vya UTI kuingia njia ya haja ndogo kwa kutokea njia ya haja kubwa.

71. Inashauriwa kiafya kumwaga maji chooni kabla ya kufanya haja yako. Na hii hasa ni kwa wale ambao wanatumia vyoo vya kuchangia au vyoo vya kukaa.

72. Supu ya samaki inashauriwa sana na wataalamu wa afya. Bila kusahau mafuta ya samaki ambayo yana uwezo wa kupambana na saratani na kufanya ukuaji wa mtoto uwe salama.

73.Hakuana vyakula vilivyohakikiwa na wataalamu wa afya kuwa vinaongeza seli za CD4. Ila unaweza kuongeza uwezo wa mwili wako kupambana na maradhi kwa kulachakula bora na mlo kamili.

74. Juisi ya matunda asili kama karoti husaidia katika kulinda mwili na maradhi.Matunda mengine ni kama mananasi, mapensheni, mapalachichi na miwa.

75. Magonjwa mengi wanayougua leo watu duniani ni kutokana na mifumo mibaya ya vyakuyla.

76.Kama unatumia vidonge vya vitamini si vyema kula maini kwa wingi maana mainiya na vitamini vingi hivyo unaweza kupata maradhi yahusuyo na zidi kwa vitamini

77.Ni vyema kula matunda japo mara moja kwa siku na samaki japo mara moja kwa wiki.

78.Ukiwa na mafua pendelea kunywa vinywaji moto kama chai ya moto. Hii husaidia kupunguza athari za wadudu wa mafua kwani hawawezi kuvumilia joto.

79. Ni vyema unapokunywa maji unywe kipole pole.

80.Unapokunywa sumu wahi kunywa maziwa au ukikosa, kunywa maji mengi sana.Fanya hivi pia kwa mtu alokunywa sumu au sabuni au kemikali yeyote. Hii ni kama huduma ya kwanza tuu kishwa wahi hospitali. Aliyekunywa sumu jitahidi kumtapisha kwa kutia vidole ama kwa namna ingine yeyote. Ila kama sumu ni kemikali zinazochubua wacha kufanya hivyo.

81.Ndani ya tomato kuna aina za carotenoid kama vile: lutein na lycopene.Hizi husaidia katika kuimarisha afya ya macho. Au kupunguza athari zinazotokana na mwanga zisidhuru macho. Tomato ni katika matunda ambayo yauwezo mkubwa wa kulinda mwili dhidi ya maradhi. Pia huweza kuuwa seli za saratani. Tomato zina vitamini C kwa wingi. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vitamini hivi vina kazi kubwa ya kulinda mwili na maradhi mbalimbali. Pia vitamini hivi vinakazi ya kuzuia utengenezwaji wa selibila ya mpangilio yaani seli za saratani.

82. Wtoto wanatakiwa wapewe vyakula vya proini kwa wingi zaidi. Vyakula hivi ndio vinahusika katika ukuaji wa tishu na miili yao kiujumla.

83.Kuwa na uzito wa kupitiliza ni katika sababu zinazosababisha kupata kisukari.Sababu nyingine ni kama mazingira, vyakula na mfumo wa maisha kwa mfano kutokufanya mazoezi.

84.Saratani ni katika sababu zinazoongoza kwa vifo vya watu wengi duniani. Mwaka 2004 watu 7.4 milioni walikufa kwa saratani, na hii ni asilimia 13% ya vifo vyote. Inakadiriwa kufikia milioni 13 mpaka ifikapo mwaka 2030.

85. Mgonjwa wa kisukari kama atafuata maelekezo anaweza kuishi kama watu wengine bila ya kuwa na matatizo. Kwa mfano karibia watu milioni 23 marekani wanaishi na ugonjwa wa kisukari.


TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU

Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE 

Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya

Comments

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.