NJIA RAHISI YA KUTIBU MENO/JINO BILA KUNG'OA Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

NJIA RAHISI YA KUTIBU MENO/JINO BILA KUNG'OAIdadi ya wagonjwa wanaong’oa meno inazidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda. Wengine hubadili meno yaliyotoboka na kununua bandia ili kuwa na mwonekano wao.

Kutoboka kwa jino ni hali ya kuwa na tundu. Wakati mwingine meno kadhaa huwa na matundu ambayo ni matokeo ya sababu mbalimbali zikiwemo bakteria wa kinywa, ulaji wa vyakula vyenye sukari mara kwa mara na kutosafisha kinywa vizuri.

Licha ya uwepo wa tiba ya tatizo hili, ipo haja ya watu kubadili mfumo wa maisha ili kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi yatakayochangia meno kutoboka yanayozidi kuenea duniani yakiathiri kila mtu, wakiwamo watoto wadogo.

Kutoa taarifa ya maumivu ili kuchunguza meno na kinywa chote ni moja ya namna sahihi za kutambua jino au meno yaliyotoboka ama kuoza. Endapo kutakuwa na haja kwa ushauri wa daktari, mgonjwa anaweza akafanyiwa X-ray.

Kila mwenye meno ana uwezekano wa kupata matundu kwenye meno kutokana na sababu tofauti ambayo yasipotibiwa mapema huweza kuathiri matabaka ya jino na kusababisha maumivu makali ambayo yakizidi mgonjwa huweza kuling’oa endapo jitihada za kulitibu hazitafanikiwa.

Sababu
Zipo sababu nyingi zinazochangia meno kutoboka. Nyingi zinaepukika na mhusika kuwa na uhakika wa afya ya kinywa chake. Mara nyingi meno yanayotoboka ni ya nyuma. Yanaitwa magego au masagego. Kwa umbile, yana mifereji ambayo ni rahisi kwa mabaki ya chakula kujishika.
Yapo nyuma ukilinganisha na meno mengine hivyo kuongeza ugumu wa kuyasafisha. Wengi hawafikishi mswaki maeneo ya nyuma ya kinywa.

Kutokana na hilo, tindikali huweza kujikusanya na kuyashambulia kwa urahisi zaidi kuliko meno ya mbele. Hii haimanishi ya mbele hayawezi kutoboka kwani watu ambao meno ya mbele yametoboka wakati ya nyuma ni mazima.

Vyakula na vinywaji
Baadhi ya vyakula na vinywaji huweza kujishika kwenye meno kwa muda mrefu. Hivi ni maziwa, ice cream, keki, na mkate hivyo kusababisha meno kutoboka kuliko vinywaji na vyakula ambavyo vinaweza kusafishika na kusafirishwa na mate kiurahisi.

Sukari
Unapotumia vinywaji vya sukari mara kwa mara unatoa fursa nzuri kwa bakteria walioko kinywani kushambulia meno yako kwa sababu unatoa fursa ya meno yako kukutana na tindikali muda mwingi ukilinganisha na mtu asiyetumia.

Kumlisha mtoto wakati wa kulala
Wazazi wanapaswa kuepuka kuwalisha watoto wadogo vyakula hasa vyenye sukari ili kuwafanya walale kwa sababu vitaendela kuwapo kinywani kwa muda mrefu baada ya mtoto kusinzia hivyo kuozesha meno yake mapema. Inashauriwa, si vizuri kumuacha mtoto kutwa nzima akiwa anakula ama anakunywa vitu vya sukari kwa faida ya afya ya kinywa chake.

Kutopiga mswaki
Ingawa inaripotiwa kuwa karibu kila mtu duniani anapiga mswaki, ukweli ni kwamba kuna upungufu kwenye upigaji huo miongoni mwetu. Watu wengi wana haraka kwenye kupiga mswaki hivyo kujikuta hawaufikishi sehemu zote za kinywa.

Kukosa floridi
Madini ya floridi huzuia kutoboka kwa meno na kusaidia kuliponya jino lililotoboka likiwa hatua za mwanzo. Kutokana na faida yake madini haya huongezwa kwa makusudi kwenye maji ya kunywa kwa viwango stahiki.

Kutokana ukweli huo, unywaji wa maji ya kutosha kila siku, licha ya faida nyinginezo mwilini, huimarisha ubora wa meno. Vilevile dawa za meno huwekwa madini hayo ili kuyaimarisha meno yetu. Ni muhimu kuhakikisha dawa ya meno unayotumia ina madini ya floridi.

Kinywa kikavu
Kinywa kikavu ni matokeo ya upungufu wa mate ambayo kiasili huzuia kutoboka kwa meno kwa kuondoa mabaki ya chakula na utando mlaini kwenye meno. Vilevile kemikali zilizomo kwenye mate husaidia kupambana na tindikali izalishwayo na bakteria na kutoboa meno. Ukavu wa kinywa huweza kuleta vitu vinavyoathiri meno kama vile baadhi ya dawa za kutibu magonjwa mbalimbali, magonjwa yanayoathiri matezi, matibabu ya mionzi ya saratani kichwani au shingoni.
Haya yote huongeza uwezekano wa kutoboka kwa meno kutokana na kupunguza uzalishaji wa mate ambayo ni kinga ya kwanza kuepuka kutoboka.

Matibabu
Tiba ya jino siyo kung’oa kama inavyoaminika. Ukweli ni kwamba kung'oa jino kutokana na sababu nyingi za kitabibu ambazo zinajitosheleza kwenye muktadha husika.

Kwenye tasnia ya tiba ya kinywa na meno, kung’oa jino lenye tatizo huwa ni hatua ya mwisho baada ya matibabu mengine kushindikana kutokana na sababu tofauti.

Sababu hizi zinaweza kuwa mgonjwa kushindwa kumudu gharama za kutibu jino lake pasipo kung’olewa au kutokua tayari kwenda hospitali mara kwa mara kwa ajili ya kuendelea na kukamilisha matibabu. Nyingine ni mgonjwa husika kwenda hospitali wakati ana maumivu makali na
huenda usiku wa siku hakula.

Baadhi ya wagonjwa huwa na aina ya matibabu wanayoyataka vichwani mwao. Hawa ni ngumu kuwabadilisha na kuwapa tiba mbadala kwa tatizo alilonalo. Ili ufaidike na matibabu ya kitaalamu ni vizuri kuwa na utaratibu wa kufanya uchunguzi wa kinywa na meno mara kwa mara kabla ya mambo hayajaharibika. Kumuona daktari mapema kunaongeza uwezekano wa kuokoa meno yenye
tatizo. Mara nyingi kutibu jino lililotoboka ambalo halina maumivu ni nafuu Zaidi ukilinganisha na jino lenye maumivu. Licha ya kung’oa, mgonjwa anaweza kuondokana na tatizo la jino lililotoboka
endapo atazingatia ushauri wa daktari. Ushauri ni moja ya matibabu muhimu kwa watu wenye meno yaliyotoboka.

Kwa ushauri wa daktari mgonjwa atapata elimu ambayo wakati mwingine huweza kuwa msaada mkubwa kuliko kung’oa jino husika kama wengi wanavyofikiria. Elimu hii hutolewa kulingana na ukubwa wa athari zilizobainishwa na vipimo.

Kuziba matundu
Kuziba meno ama kufanya ukarabati ni matibabu yanayoaminika Zaidi kwa meno yaliyotoboka hasa kwa matundu ambayo yamepevuka. Hili hutakiwa kufanywa mapema kwani mgonjwa akichelewa atalazimika kuling’oa ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza.

Dawa zinazotumika kuziba meno hutofautiana kulingana na mahali lilipo jino bovu hivyo gharama za dawa husika.

Kulijengea
Hapa ni kwa meno ambayo yameliwa na matundu na haiwezekani kuyaziba kikawaida. Matibabu haya huwa na hatua kadhaa. Pia yanaweza yasifahamike sana miongoni mwa watu wa kipato cha chini maana ni gharama. Endapo njia hizo zimeshindikana jino linaweza likang’olewa. Hili hufanywa kwa meno ambayo yametoboka, kuoza na kuisha kiasi ambacho huwezi kufanya ukarabati wowote.

Meno hayo yanashauriwa yaondolewe kwa usalama wa yanayobaki kwani uwepo wake wakati huwezi kusababisha maambukizi kwenye kinywa.


TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU

Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE 

Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya

Comments

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo