NJIA RAHISI YA KUPUNGUZA KITAMBI NA UNENE Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

NJIA RAHISI YA KUPUNGUZA KITAMBI NA UNENE

Mtindo wa maisha, vyakula na shughuli za kila siku za mwanadamu ni baadhi ya vitu vinavyosababisha idadi kubwa ya wake kwa waume kuwa na uzito auunene kupita kiasi na wakati mwingine kuwa na vitambi.

Matatizo haya yamekuwa yakiwapata watu wa jinsi zote na kuwanyima raha wanawake wengi, ambao hufikia hatua ya kutumia mikanda maalumu ya kufunga tumbo au kuhangaika kupitia njia mbalimbali ili kupunguza kadhia hiyo kwao.


Kutokana na kuongezeka kwa tatizo hilo, kumezuka dawa nyingi zinazodaiwa kuwa na uwezo wa kupunguza vitambi na uzito mkubwa, lakini wataalamu wa afya wanaonya kuwa ni sumu.
Tafiti nyingi za kisayansi zinaonesha kuwa dawa hizi kwa kiasi kikubwa zina kemikali kama vile phentermine, sibutramine, phenolphthalein, caffein, hydroxycitric acid (HCA) na senna ambazo zina madhara makubwa kwa afya ya mwanadamu.

Dk. Phil McGraw anasema baadhi ya dawa hizo huathiri sehemu ya ubongo inayohusika na hamu ya chakula. "Hamu ya chakula ni muhimu kwa ajili ya ubora wa afya na maisha. Dawa yoyote inayoharibu hamu ya chakula kwa kipindi kirefu, inaweza kusababisha madhara ya kiafya", anasema Dk. Phil.

Mama mwenye uzito wa kilo 108, Doreen Shayo anasema amewahi kujaribu dawa za kupunguza mwili, lakini akapatwa na homa kali iliyohatarisha maisha yake baada ya wiki moja, hivyo alishindwa kuendelea na dozi hiyo. "Nilishawishiwa kununua dawa hiyo ya kupunguza uzito na nilishauriwa kula mbogamboga, matunda na maji kwa wingi wakati wa dozi, sikuwa nakula
wanga wala chakula kamili. Nilipata homa ya ghafla madaktari wakanishauri kwamba dawa zile hazikuwa nzuri kwangu hivyo niachane nazo, wakati huo nilikuwa na kilo 120 lakini nilipungua kutokana na maelekezo ya madaktari", anasema Doreen.

Baadhi ya madaktari bingwa wa afya ya binadamu wanasema msukumo wa dawa hizo unaowafanya wahusika kuharisha mafuta mengi kwa wakati mmoja, ni njia isiyo sahihi ambayo pia huathiri baadhi ya viungo ndani ya tumbo, huku madhara yake yakijitokeza miaka kadhaa mbeleni.

Tabibu wa tiba mbadala kutoka kituo cha Fore Plan Clinic, Juma Mwaka anasema asilimia kubwa ya dawa za kupunguza kitambi na mwili kwa uharaka ni sumu.

"Mtu anapewa dawa anaharisha sana, swali la kujiuliza nini dawa inafanya tumboni na kusababisha kupata choo laini au kuyeyusha mafuta kwa muda mfupi? Lazima tujue kwamba zina madhara baada ya muda, wengi wanauziwa vitu vibaya na mbegu fulani ambazo ni sumu halafu mwili unabadilika
anaharisha sana, anaambiwa dawa ndio inafanya kazi yanatoka mafuta mengi, si njia sahihi ya kupunguza uzito wa mwili au kitambi."

Dk. Samuel Shita kutoka Hospitali ya Mwananyamala anasema kwa kawaida kuharisha humfanya mtu kupunguza maji mengi na chumvichumvi mwilini na hivyo huathiri kazi ya seli na mfumo wa fahamu.

"Dawa hizo nyingi hazijaruhusiwa kutumika na Wizara ya Afya na wala hazijathibitika kwamba ni sahihi kwa matumizi ya binadamu, lakini wanazitumia na madhara yake yanaanza kujitokeza baada ya kutumia mtu anaharisha sana na yeye anadhani ana mafuta lakini ule ni uteute unaokaa tumboni unaosaidia tumbo kufanya kazi.

"Utafiti unaonesha kuwa watu wanaopendelea kula katika migahawa mikubwa ndio wanaoongoza kuwa na miili mikubwa, teknolojia zipo na dawa zitumikazo lazima ziwe zimefanyiwa utafiti kwa zaidi ya miaka 10. Kuna madhara mengi yanayoweza kuwakuta watu ikiwamo ya figo, moyo, ini na
mishipa ya damu."

Dk Shita anasema kuna njia sahihi za kupunguza tumbo ambazo pia ni salama. "Mtu anatakiwa kufanya mazoezi mepesi na matumizi sahihi ya vyakula, tunatakiwa kupunguza vyakula vya wanga kupita kiasi, sukari na mafuta. Pia tunatakiwa kupunguza mafuta yatokanayo na wanyama kwa kuwa yana Cholesterol nyingi na ulaji holela."

Anasema soda, pipi na chocolate ni vyakula ambavyo havitakiwi kutumika
kupita kiasi.

Mwaka anazitaja hatua sahihi za kupunguza kitambi na kuondoa sumu mwilini akisema: "Kutumia juisi za matango, karoti na nyanya kila siku kwa muda wa mwezi mmoja sumu zote zinaondoka."
Hata hivyo, Mwaka anasema mtu anapokula chakula ni lazima kiishe tumboni kabla ya kuingiza kingine, vinginevyo anakuwa ametunza sumu mwilini kutokana na kuwa na mabaki maengi ya chakula cha takriban hata mwaka mmoja.

"Mfuko wa chakula una uwezo wa kutunza chakula kwa muda mrefu, ndiyo maana binadamu hufa akikosa chakula kwa siku nyingi. Miongoni mwa vitu vinavyofanya uondoe sumu mwilini ni kufuata sheria za ulaji na njia za asili za kuondoa sumu hiyo na si njia za haraka kwani zina madhara," alisema.

Wataalamu wa masuala ya dawa Deborah Mitchel na David Dadson, katika kitabu chao kilichochapishwa mwaka 2002 cha "The Diet Pill Guide: The Consumer's Book of Over-the-Counter and Prescription Weight -Loss Pills and Supplements," wanasema: "Ingawa ushahidi wa dawa hizi unazidi kuongezeka, bado watu wengi wanaaminishwa kwa uongo kuwa zina manufaa. Hata hivyo, pia watu wanaendelea kuamini kuwa dawa hizi zinazotokana na mimea na ni dawa salama za asili zinazofanyiwa utafiti wa kina na kuthibitishwa na mamlaka za udhibiti na usalama wa dawa kama nyingine za hospitalini."

Namna ya kupunguza kitambi.

Maji ya moto yakitumiwa kwa umakini yana uwezo wa kupunguza kitambi, tumbo au uzito mkubwa wa mwili kwa asilimia 60.


Maji ya moto yana uwezo wa kupunguza tumbo kwa zaidi ya asilimia 60, unachotakiwa kufanya ni kuyachemsha yawe ya vuguvugu kiasi kunywa kati ya glasi nne mpaka sita na iwe ni katikati ya mlo mpaka mlo ndiyo maana kuna watu wanashauri unywe asubuhi au iwe katikati ya mlo wa jana usiku na ule utakaokwenda kuula baadaye.

Lakini pagumu zaidi ni pale ambako kabla hujakwenda kupiga mswaki ndiyo unatakiwa kuyanywa haya maji. Tunapata vitamin B12 ambazo zinazalishwa mdomoni wakati binadamu akiwa amelala na mojawapo ya vitamin hiyo ni pamoja na kusaidia msagiko (mmeng'enyo) ule wa vyakula.
Tatizo la wengi kukaa na vyakula kwa muda mrefu tumboni, ni moja ya sababu pia ya kuwa na tumbo kubwa yaani kuwa na mafuta ya ziada tumboni na wengine wanakuwa na vyakula vingi wanavyoingiza kuliko wanavyovitoa.

Asubuhi kabla hujapiga mswaki ukaondoa zile vitamin mdomoni zinywe pamoja na maji, kunywa maji ya vuguvugu glasi nne mpaka sita kila siku unapoamka asubuhi mfululizo mpaka siku 21, baada ya muda fanya hivyo kwa wakati mwingine na wakati ukifanya hivyo pia epuka vile vitu vitakufanya
uendelee kuwa na tumbo ili unachokifanya kiweze kuwa na majibu na si kuoga na kujipaka tope, na  kupunguza vyakula vya wanga ni njia mojawapo itakayomfanya mhusika kupata majibu ya haraka.

TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU

Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE 

Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya


Comments

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo