FANYA HIVI ILI KUPATA MTOTO WA KIUME Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

FANYA HIVI ILI KUPATA MTOTO WA KIUME


Kupata mtoto wa kiume ni jambo linalohitaji ushirikiano wa pande zote mbili, yaani mke na mume na ni jambo linalohitaji hatua kwa hatua na kwa umakini, ingawa njia nitakayoeleza hapa haimaanishi kuwa inaweza kufanya kazi kwa asilimia 100. Bali ni njia ambayo imekuwa ikitumika mara kwa mara na ndiyo njia rahisi na ukiifuata unaweza ukapata kwa asilimia 75.

Mwaka 1960 mwanasayansi Landrum Shettles aliandika kitabu kinachohusu uchaguzi wa jinsi ya mtoto. Mwanasayansi huyo wa tiba ndiye aliyeileta nadharia yake iliyojikita zaidi katika vitu vilivyomo ndani ya seli, yaani malighafi za kijenetiki ziitwazo chromosomes ambayo ndiyo inayotumika na kamaikifuatwa vizuri basi huweza kuwa na mafanikio.

Sayansi ya kijenetiki inaeleza kuwa mwanamke huwa na mbegu ya XX na ya kiume huwa na XY, na pale yai la kike linaporutubishwa hutokea mgawanyiko wa seli na mbadilishano wa malighafi za kijenetiki hutokea.

Hivyo kiumbe kinachotungwa yaani mtoto, huwa na nusu ya malighafi za kijenetiki kutoka kwa mama na nusu nyingine kutoka kwa baba, na akipata mbegu XX huwa ni jinsi ya kike na akipata XY ni wa kiume. Kiasilia mbegu Y huwa ni ndogo kimaumbo, zina mwendokasi mkubwa lakini
hufa mapema ukilinganisha na za kike X ni kubwa, hazina kasi, lakini huishi kwa muda mrefu. Kwa kutumia ufahamu huu ndipo mwanasayansi Shettels aliweka nadharia ambazo zinatumika katika uchaguzi wa jinsia.

Kuna hatua tano za kufuata kwa umakini ili uweze kufanikiwa, ingawa haimaanishi kuwa ni lazima ufanikiwe kwani hatua hizi huongeza nafasi zaidi ya kupata jinsi ya kiume na kwa yule atakayehitaji jinsi ya kike afanye kinyume cha hatua hizi:-

Hatua ya kwanza.
Hatua ya kwanza ni kugundua wakati wa ovulation, ama siku ambayo yai la kike linatoka. Hiki ni kipindi ambacho yai la mwanamke lipo tayari kurutubishwa na mbegu ya kiume hivyo mimba huweza kutungishwa.

Ili kugundua kuwa upo katika ovulation, inabidi kufuatilia yafuatayo: Inabidi uwe na chati ya kuangalia na kufuatilia ute wa kizazi unaotoka ukeni, maana muda mfupi kabla ya ovulation ute huwa wa majimaji na wa kuvutika hufanana kama vile wa mayai ya kawaida, nikimaanisha ya kuku, ambayo yamezoeleka kwa wengi.

Ni vizuri kupanga chati hii kwa zaidi ya miezi mitatu ili kusudi uwe na uzoefu wa kugundua tofauti ya ute. Vilevile inabidi uwe na chati ya kuweka rekodi ya joto la chini la mwili wakati ukiwa umepumzika, nikiwa na maana mara nyingi ukiwa umelala.

Joto la chini la mwili hupanda kwa nyuzi joto 0.5 sentigredi kipindi cha ovulation. Ni vizuri chati hii iwe pamoja na ya ute wa kizazi, kusudi uweze kufuatilia mabadiliko haya kwa pamoja.

Kipimo cha kugundua ovulation ni kipimo ambacho huangalia wingi wa homoni aina ya Lutenizing ambayo hutolewa kwa wingi kipindi hiki. Kipimo hiki ni vizuri kufanya mara mbili kwa siku, kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 9:00 mchana. Vilevile kati ya saa 11:00 jioni na saa 4:00 usiku.

Hatua ya pili
Hii ni hatua ya kutegea wakati muafaka wa kufanya tendo la ndoa. Ni vizuri kufanya tendo la ndoa kipindi cha saa 24 kabla ya ovulation na saa 12 baada ya ovulation. Kwa sababu tindikali na utelezi katika ute wa kizazi hupungua na hivyo husaidia mbegu za mwanaume hasa aina ya Y kusafiri haraka na kulifikia yai la mwanamke na kulirutubisha.

Hatua ya tatu.
Pendelea mtindo au staili inayofanywa na wanyama kama mbuzi wakati wa tendo la ndoa, yaani mtindo wa mwenza wako kuinama. Mtindo huu huwezesha mlango wa uzazi kuwa karibu na sehemu ya kiume pia kuingia umbali mrefu zaidi ndani ya uke, hivyo basi mbegu za kiume humwagwa
karibu na shingo ya kizazi na kulifikia yai haraka zaidi.

Hatua ya nne.
Ni muhimu mwanamke kufika kileleni kabla ya mwanaume; kufika kileleni kwa mwanamke husaidia kubadili mazingira katika uke kuwa ya ukakasi (alkaline) hivyo kusaidia mbegu za kiume “Y” kuwa imara zaidi. Uke kuwa na tindikali huipunguza uimara wa mbegu ya kiume.

Hatua ya tano.
Hii ni kwa upande wa mwanaume. Ni vizuri kuvaa nguo zisizoweka joto kali na kubana. Unapaswa kuvaa chupi au nguo ambazo hupwaya na zimetengenezwa kwa pamba. Nguo za ndani zinazobana ambazo huongeza joto hupunguza idadi ya mbegu za kiume. Joto pia hupunguza ubora na utengenezaji wa mbegu za kiume.

Vilevile inabidi kunywa vinywaji vyenye caffeine kabla ya tendo la ndoa. Hii huongeza nguvu ya mbegu za kiume aina Y. Mambo mengine ya kuzingatia ni mlo. Hakikisha unakula vizuri wiki moja kabla na siku ya tendo. Tafiti zinaonyesha kuwa ulaji wa vyakula vyenye sukari huiwezesha mbegu ya Y kuimarika zaidi na kuongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume. Vyakula hivi ni kama matunda matamu, vyakula vya wanga na vinywaji vyenye glukosi.

Vyakula vingine ni kama vile nyama nyekundu, mayai, maziwa, vyakula vya baharini kama vile samaki, kamba na pweza. Kwa upande wa mwanamke, anapaswa kula zaidi vyakula visivyo na tindikali kama vile kuepuka kula matunda yenye uchachu na vyakula jamii ya kunde
kupitia kiasi.

Mambo mengine ni kuzingatia mazingira ya tendo lenyewe, hakikisha upo vizuri kiafya, kimwili na kiakili. Usiwe na msongo wa mawazo na sonona kwa sababu huleta mwingiliano na tendo, hivyo kulifanya kuwa dhaifu.

Ni vyema pia kutafuta mazingira mazuri ya kufanyika kwa tendo lenyewe. Lengo ni kuwa na utulivu wa kimwili na kiakili pia. Hii itakuepusha pia na usumbufu utakaoweza kuleta mwingiliano na tendo lenyewe.


TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU

Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE 

Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya

Comments

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo