HARUFU MBAYA YA KINYWA (HALITOSIS) || JINSI YA KUTIBU Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

HARUFU MBAYA YA KINYWA (HALITOSIS) || JINSI YA KUTIBU

Photo 1 : Halitosis/ Harufu mbaya ya Kinywa
Wapo watu wana harufu mbaya ya kinywa kiasi cha kukosa amani mbele ya hadhara.  Hawa ni wale wanaotambua juu ya tatizo hilo.  Wengine hawaelewi lakini huwa kero kwa jamaa zao wanaolazimika kuwa wavumilivu ili kutoharibu uhusiano uliopo.

Harufu mbaya ya kinywa inaweza kuwa tatizo linalokukera hata kukusababishia wasiwasi unapojumuika na wenzako katika masuala mbalimbali, iwe ofisini au mtaani.
Kitu ambacho wengi hawafahamu ni kwamba dawa nyingi zinazouzwa na kuelezwa kutibu tatizo hilo hazina uwezo wa kuleta suluhu ya kudumu bali ya muda mfupi tu.  Dawa hizo hazitibu tatizo bali linagusa tu athari zake.

Usishangae kwa sababu ya uwapo wa dawa kadha wa kadha zilizotengezwa kwa ajili ya kupambana na harufu ya kinywa.  Dawa hizi hazijaelekezwa kwenye kiini cha tatizo bali linapoishia.
Ili kumaliza harufu ya kinywa ni lazima kujua imesababishwa na nini ambacho kitadhibitiwa kikamilifu ili kupata suluhu ya kudumu.  Zipo sababu nyingi zinazochangia harufu hii.
Baadhi ya vyakula, magonjwa au tabia huweza kusababisha harufu mbaya ya kinywa.  Pamoja na hayo habari njema ni kwamba unaweza kuondokana na kadhia hiyo kwa kufanya usafi madhubuti wa kinywa chako.

Ili kukabiliana na tatizo hili inashauriwa kuwa macho wakati wote.  Hili litafanikiwa endapo utazifahamu dalili za kuwa na harufu isiyopendeza kutoka kinywani mwako.  Lakini ni muhimu kufahamu kwamba harufu mbaya hutofautiana kutegemea chanzo.
Kuna baadhi ya watu wana mashaka na harufu ya vinywa vyao hata kama wana tatizo wakati wapo wenye harufu mbaya ila hawajitambui.

Kwa sababu ni vigumu kutathmini harufu ya kinywa chako mwenyewe, unaweza kumuuliza mtu wako wa karibu ili kujiridhisha kama una harufu mbaya ya kinywa.
Ukithibitisha kuwa nayo, ni vyema ukapitia ufanyaji wako wa usafi wa kinywa.  Jaribu kufanya mabadiliko ya mfumo wa maisha kama vile kupiga mswaki mara baada ya kula na kunywa maji mengi.

Ukiona tatizo linaendelea licha ya kufanya mabadiliko haya, ni vyema ukamuona daktari wa kinywa na meno kwa msaada zaidi.
Ni daktari huyu pekee anapaswa kukueleza chanzo cha tatizo hilo ambalo mara nyingi huwa linatokana na matatizo yaliyomo kinywani.
Uchunguzi wa daktari wa kinywa na meno unaweza ukakupeleka kwa madaktari wengine kwa uchunguzi zaidi kama ataona tatizo lako halitokani na hali ya afya ya kinywa chako.

Sababu.
Mara nyingi harufu mbaya ya kinywa huanzia mdomoni ingawa vyanzo vyake ni vingi.  Ugonjwa wa fizi ni moja ya sababu ya harufu hii kwani husababisha kuvimba na kutoa damu wakati wa kupiga mswaki, kung’ata kitu ama kutema mate.

Photo 2;Fizi zilizoharibika

Ugonjwa wa fizi hutokana na upigaji wa mswaki.  Wakati mwingine huwa hauna maumivu kiasi kwamba mtu anaweza kuwa nao na asijue.

Kutopiga mswaki ni sababu nyingine.  Kama hupigi mswaki na kufanya flosi, mabaki ya chakula yakikaa kwa muda huoza na kutoa harufu mbaya.  Ulimi nao unastahili kufanyiwa usafi kwani unafanana na taulo hivyo kushika mabaki ya chakula na kuweza kukaribisha bacteria baada ya kula.

Meno ya Bandia
Meno ya bandia yasiyosafishwa mara kwa mara au ambayo hayakai vizuri huweza kuhifadhi mabaki ya chakula na bacteria ambao kwa pamoja huweza kuchangia kuwapo kwa harufu mbaya ya kinywa.
Photo 3: Meno bandia
Meno Yaliyotoboka
Meno yaliyotoboka hayasafishiki unapopiga mswaki.  Matundu yaliyopo kwenye meno hayo huweza kuhifadhi chakula ambacho baada ya muda huoza na kutoa harufu mbaya.

Japokuwa tatizo hili husababishwa na meno yote yaliyotoboka, lakini ya nyuma (magego) huchangia zaidi kwani mara nyingi watu wengi huwa hawayasafishi.  Hawafikishi mswaki kwenye meno hayo.

Photo 4; Meno yaliharibika

Kinywa Kikavu
Kwa kawaida mate husaidia kusafisha kinywa na kuondoa mabaki ya chakula hivyo mtu mwenye kinywa kikavu huweza kuwa na harufu mbaya kutokana na upungufu huo.

Kwa kawaida kinywa kikavu hutokea usiku mtu anapolala na akiamka huwa na harufu ya asubuhi ambayo huongezeka iwapo mtu huyo alilala kinywa wazi.  Hali hii pia huweza kusababishwa na magonjwa ya tezi la mate matumizi ya baadhi ya dawa ambazo huathiri ufanyaji kazi wa tezi la mate.

Dawa
Baadhi ya dawa zinachangia harufu mbaya ya kinywa endapo zitasababisha ukavu wa kinywa.  Lakini kuna dawa nyingine zinapotumiwa kisha kumeng’enywa mwilini hutoa kemikali ambazo humfanya mtumiaji atoe harufu yake wakati wa kupumua.

Maambukizi Kinywa
Harufu mbaya inaweza kusababishwa na maambukizi hasa kwenye vidonda vilivyomo kinywani.  Vidonda hivi huweza kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo kung’oa jino kisha pengo likapata maambukizi.

Tumbaku
Uvutaji wa sigara au matumizi ya bidhaa zozote na tumbaku mfano ugoro au shisha huambatana na harufu ambayo mara nyingi huwa mbaya.  Wavutaji wa sigara wana uwezekano wa kupata ugonjwa wa fizi ambao ni chanzo kingine cha harufu mbaya.

Vyakula
Kuna baadhi ya vyakula huleta harufu isiyo nzuri kinywani.  Vyakula kama vile vitunguu maji, tangawizi na vinginevyo baada ya muda huleta harufu mbaya ya kinywa.

Magonjwa Mengine
Mara chache harufu mbaya ya kinywa huweza kusababishwa na maambukizi sugu ya tezi (chronictonsilitis) ambayo bakteria wanaosababisha pia huchangia harufu mbaya.  Halikadhalika maambukizi sugu kwenye pua na koo huweza kuchangia tatizo hili.

Saratani ya kinywa na koo na magonjwa yanayohusiana na mfumo wa chakula pia huweza kusababisha harufu mbaya ya kinywa.  Vilevile, kuna watu ambao hupata tatizo la tindikali ya tumboni kuja kwenye koo na kinywani (gastroesophageal reflux disease, GERD) nao wanaweza kupata tatizo hili.

Matibabu
Ili kuondokana na harufu mbaya ya kinywa, jikinge usipate matundu kwenye meno na jizuie na magonjwa ya fizi kwa kufanya vizuri usafi wa kinywa.


Kwa ujumla matibabu ya harufu mbaya ya kinywa hufanywa kwa kuishughulikia sababu hiyo endapo daktari atagundua kuchangiwa na ugonjwa fulani bado ataagiza utibiwe maradhi hayo kwanza.
Kuna mambo muhimu yanashauriwa ili kupunguza uwezekano wa kuwa na harufu hii.  Wataalamu wanaagiza kupiga mswaki meno ulimi walau mara mbili kila siku, asubuhi baada ya kula na usiku kabla ya kwenda kulala.  Mara baada ya kufanya hivyo, unapaswa kusukutua kwa dawa maalumu za kufanya hivyo (mouthwash).

Fanya flosi angalau mara moja kwa siku huku ukinywa maji mengi endapo una tatizo la kikavu kwani yanasaidia kupunguza tatizo hili. Jitengenezee raba ya kumuona daktari wa kinywa na meno.
Kumbuka kwa mtu wa kawaida inampasa kumuona daktari wa kinywa na meno mara moja kila baada ya miezi sita, yaani mara mbili kwa mwaka.  Lakini mwenye harufu mbaya unaweza kumuona mara nyingi zaidi na kufuata maelekezo yake. 


TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU

Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE 

Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya

Comments

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.