Homa ya ini ni ugonjwa hatari kuliko Ukimwi Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

Homa ya ini ni ugonjwa hatari kuliko Ukimwi


Hakuna shaka kwamba umewahi kusafiri nje ya nchi yako na kutakiwa kupata chanjo.
Kwa wengine, chanjo hiyo ikiwamo ya homa ya ini imeonekana kama usumbufu na  udhia mtupu. Hata hivyo, wapo wengine ambao hawaufahamu ugonjwa huu.
Kwa wanaoujua, wanahofia kuwa ugonjwa huu una madhara makubwa pengine kuliko  saratani na Ukimwi.
Homa hiyo au Hepatitis B inapewa uzito mdogo licha ya kuwa ni  ya hatari kubwa.
Wataalamu wanaeleza kuwa Hepatitis B au homa ya ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa urahisi, wenye madhara makubwa na wenye uwezo wa kuambukiza kwa wepesi kuliko Ukimwi.

Kitaalamu, ugonjwa huu, husababishwa na virusi vya Hepatitis B (HBV) ambavyo huathiri  mfumo wa utoaji wa sumu mwilini. Inaelezwa kuwa robo tatu ya watu ulimwenguni wameathiriwa kwa muda na homa ya ini na wengine milioni 350 wameathirika moja kwa moja.
Takwimu zinaonyesha kuwa homa ya ini huua watu 600,000 kila mwaka katika sehemu mbalimbali, idadi ya watu inayolingana na wale wanaokufa kutokana na malaria.
Maradhi haya ya ini yanaelezwa kuwa yanaweza kusababishwa na kunywa kileo kupita kiasi au sumu inapoingia mwilini.
Hata hivyo, mara nyingi ugonjwa huu husababishwa na virusi.
Wanasayansi kwa upande mwingine wamegundua virusi vitano vinavyosababisha ugonjwa huu na wanasema kwamba huenda kuna vingine vitatu.
Matokeo yake, sheria zimewekwa  katika nchi mbalimbali ambazo zinamtaka kila raia mgeni anayetaka kuingia katika nchi husika, kupata chanjo ya ugonjwa huu ili kuepusha maambukizi.
 Kila anayechanjwa  hupewa kadi maalum  itakayomwezesha kuingia katika nchi husika ili kuthibitisha kuwa amechanjwa.
 Hata hivyo, ujanja mwingi umekuwa ukifanyika katika baadhi ya nchi ikiwamo Tanzania ambapo watu hujipatia kadi za homa ya manjano kwa kutoa rushwa na kukwepa kuchoma chanjo hiyo pindi wanapotaka kusafiri nje ya nchi bila kujua madhara ya kutopata chanjo hiyo.
 Vilevile, chanjo hiyo iliwahi kukosekana nchini kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na sababu ambazo haziwekwi wazi na mamlaka zinazohusika.
Hatari kubwa ya ugonjwa huu inatajwa ni namna ya uambukizaji wake ambapo, unaposhika damu au majimaji ya mwilini ikiwemo mbegu za uzazi huweza kuambukizwa.
 Wataalamu wanaeleza ubaya wake ni kuwa unaweza kuambukizwa kwa kufanya ngono na hata kwa kushika majimaji ya mwili wa mtu aliyeathirika ikiwemo damu, mate, machozi na mkojo.
Taarifa za Shirika la Afya Duniani(WHO) zinaeleza kuwa  kirusi cha homa ya ini kinaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu kwa siku saba na kwa wakati huu, kirusi hiki kinaweza kusababisha maambukizi iwapo mtu hajapata chanjo ya kuuzuia.
Watanzania wengi bila kujua wamekuwa wakiugua maradhi mbalimbali yanayosababishwa na homa ya ini na bila kufahamu ini limekuwa likiathirika taratibu.
Dk Yuki Mark wa Hospitali ya Parktown North, Johanesburg, nchini Afrika Kusini anasema kuwa homa ya ini aina ya B inaweza kuua kimyakimya bila kuonyesha dalili zozote.
“Huenda dalili zikaonekana waziwazi miaka mingi baada ya mtu kuambukizwa. Zinapoonekana, huenda tayari ini limenyauka au lina saratani na magonjwa hayo huua asilimia 25 ya watu walio na virusi vya HBV,” anasema Dk Mark.
 Aidha, mtaalamu huyo anasema, dalili kuu zinazojulisha kuwa mtu ana homa ya ini ni kutapika, kuchoka kupita kiasi, kuathirika kwa ini, homa na mkojo kuwa wenye rangi ya njano iliyokolea sana.
“Unaweza kuharisha na kutapika au kupata maumivu katika eneo fulani la tumbo lako, macho na ngozi kuwa vya njano,” anaeleza.
Homa ya ini aina ya B, inaweza kuingia mwilini mwa mtu kwa njia ya ngono, kama ilivyo Ukimwi na magonjwa mengine ya  zinaa. Hivyo basi, majimaji   katika mwili wa mwanadamu yanaweza kuwa chanzo cha maambukizi.
“Watu  wengi wanaendelea kuambukizwa kwa kutiwa damu yenye virusi hivyo, hasa katika nchi ambako hakuna vifaa bora vya kuchunguza virusi hivyo katika damu. Virusi vya HBV vina uwezo mkubwa zaidi wa kuambukiza kwa kulinganishwa na virusi vya Ukimwi,” anasema Dk Mark
Anaongeza: “Hata kiasi kidogo cha damu yenye virusi hivyo kama ile inayobaki kwenye wembe, inaweza kupitisha virusi hivyo na tone la damu iliyokauka kwa juma moja au hata zaidi inaweza kumwambukiza mtu virusi hivyo.”
Dk Mark anasema, madhara mengi huweza kumkumba mtu aliyepata maambukizi ya homa ya ini, kwani anaweza kupata shinikizo la damu, anaweza kuathirika ubongo au hata kupooza sehemu ya mwili wake.
Angalizo ambalo mtaalamu huyo anaeleza ni kuwa baada ya mtu kuambukizwa homa hiyo, hawezi kupona, kwani dawa kuu ya ugonjwa huu ni chanjo ya kuzuia homa ya manjano (yellow fever vaccination).

TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU

Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE 

Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya

Comments

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo