Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.
Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.

Sababu za kukosa nguvu za kiume

 Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
 • Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
 • Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
 • Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume

Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano na ndoa.

1. BlueberryBlueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.

2. Mtini (Figs)

Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.

3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)

Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.
Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.

4. Karanga


Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.

5. Vitunguu saumu

Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.

6. Ndizi

Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).


Vyakula ni bora kuliko madawa makali

Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.
Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala
Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.
Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la nguvu za kiume.


TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU

Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE 

Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya

Comments

 1. Somo zur san nimepnda
  Ila Dr naomb kujua dawa halisi yakutengeneza nyumban daw ya fangasi chini ya umme

  ReplyDelete
  Replies
  1. Nimeweza kufanya mpenz wiki tatu toka nilipo hoa lakin sahiv siwez jongoo ananguvu kabisa nifanyeje wataalamu nisikimbiwe

   Delete
  2. Kama ujapon nichek kwa no 0783152817 nikupatie dawa kutibu tatizo lako

   Delete
  3. DR Nina shida ya kukojoa mara kwa mara sana sana nyakti za usku naweza kukujoa mara Tano kwa usku mzima inaweza kuwa ni shida gan

   Delete
 2. BIg up you may help many guys this is because now days erectile dysfunction is big problem in most marriage so thanks dear i like it

  ReplyDelete
 3. Aya matunda mengine sijui yanapo patikana. Nitatumia kwamda gan adi kupata majibu. Au kupona kabisa

  ReplyDelete
 4. Je pilipili yenye ukitumia inaweza saidia????

  ReplyDelete
 5. Somo Ni zuri na lenye kuheleweka lakini Kuna baadhi ya matunda uliyoyaorodhesha kwakweli sijui yanapo patikana

  ReplyDelete
 6. Karibu katika blog yangu kujifunza zaidi kuhusu masuala ya afya teknolojia na mashairi

  www.mrbunduki.com

  ReplyDelete
 7. Ndio somo la afya lisilo na matokeo hasi mbeleni ko afya ni chakula kuliko dawa

  ReplyDelete
 8. Its a good Documentary...my qn is How long will it take to recover from the effects of masturbation?

  ReplyDelete
  Replies
  1. Okay..!! Masturbation Will Hear Not only by Taking The Above Provided Diet only First abstain Porn and Masturbating then Fellow the Above with the Regard of You Hormones and Other Foods that you it will also affect the recovery Time but Probably A From three weeks Mostly Good outcomes start to reveal

   Delete
 9. Tatizo la ngiri (hernia) halisababishi upungufu wa nguvu za kiume?

  ReplyDelete
  Replies
  1. linasababisha chamsingi kama una ngiri tembelea vituo vya afya ili uweze kupata oparation kwan tatizo la ngili ni tatizo lakudum kama kama hutofikia muhafaka litakunyima furaha nyumban.na wala oparation yake sio kubwa na pia aichukuwi muda kupona.unafanyiwa oparation huku ukiwa upo macho wala sio oparation yakutisha jitaid ndugu yangu kutembelea Hospital ili uweze kusaidiwa

   Delete
 10. Uti inasabisha uume kuto kusimama vizuri

  ReplyDelete
 11. Kuna kipengele nimeona umeandika et inaongeza wingi wa shahawa na mbegu za kiume , haya maneno tofauti yake nini Dr??

  ReplyDelete
 12. Je ukila ndiz,karanga,vitunguu swaum je vinawez kukusaidia na ni kias gan inapasw ule

  ReplyDelete
  Replies
  1. Kiujumla matunda ni muhmu unashauliwa kula tofauti tofauti matunda ni vema Sana Kama utaweza kupata asali na tetele ni nzuri pia Sana tu hzo ni nyongeza tu najarbu kuongezea vitu vinavyo weza saidia

   Delete
 13. kitamutamu750@gmail.com sawa ila wanasema ukila chakula na baadae ukila matundaa haifai hii kweli?!

  ReplyDelete
 14. somo nzuri sana na natumain litaweza kutusaidia..ahsante docta

  ReplyDelete
 15. Tuko pamoja sana by me Dr jeremia from mbeya Tanzania 0759144539

  ReplyDelete
 16. Asante kwa darasa na somo zuri.
  Maswali langu ni kwamba
  1. Je ni namna gani mtu anaweza kutumia vyakula vilivyoorodheshwa hapo juu
  2. Je tatizo la Bawasiri linaweza kusababisha jematatizo ya nguvu za kiume na vip linawezaje kutibiwa ? Asante

  ReplyDelete
 17. Nahitaji kufahamu kwa wale wanaojichua wafanye Nini ili hiyo tabia ikome maana ikisha kamata inakuwa ni ngumu kuiacha,na je pia anatakiwa kutumia vyakula gani maana pia anapoteza nguvu zake kumwaga vile virutubisho for free, Naitwa Richpaullz Ahsante.

  ReplyDelete
  Replies
  1. 0762401086 Ndio mawasiliano yangu Kama itawezekana tuwasiliane

   Delete
 18. 0655142626 Kama unapata changamoto yoyote kuhusu nguvu za kiume wasiliana namm kwa ushauri, na nimazoez gan waweza fanya na product za kuongeza nguvu if necessary. Kwa uweza wa Mungu utakuwa sawa.

  ReplyDelete
 19. Kwa mtu mwenye shida ya kufika kilelen mapema au kukosa hamu ya tendo Niko na kahawa maalumu kwajili hiyo no mm
  Dr Lee nutricare # 0693214766 ukinitafta nakusaidia kwani nimesaidia wengi na hata wale wasio simamisha kabsa dawa ipo ikiwemo na hii kahawa asante na karibu kwa masomo zaidi kuhusu afya ya uzazi kwani Nina magroup yangu kujiunga ni bure kwajili ya kusaidia watu

  ReplyDelete
 20. Mimi nafanya mapenz naweza enda hadi round 4 6 bila kuchoka na bila mboo kushindwa kusimama ila changamoto nilionayo namwaga shahawa chache sanaa yanii nifanyajeee ili niwe namwaga shahawa nyingiiii???

  ReplyDelete

Post a Comment

Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku

Popular posts from this blog

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo