HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO


Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali.
Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini.
Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI.
Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb).
Kwa mjibu wa wataalamu wa tiba asili nchini China, mdalasini huongeza joto mwilini. Mdalasini hutengeneza joto mwilini lijulikanalo kwa kichina kama “yang”. Yang hutibu “yin” (yin kwa kichina humaanisha baridi). Wakati asali yenyewe kwa asili huweka sawa usawa wa joto na baridi mwilini.
Haya ndiyo maajabu 24 ya asali yenye mdalasini ulikuwa huyajuwi bado

1. HUUA BAKTERIA
Asali ina sifa ya kudhibiti bakteria. Nadharia hii inathibitishwa na tafiti nyingi kadhaa. Asali hupigana dhidi ya maambukizi ya ndani na ya nje. Mdalasini pia una sifa ya kuondoa vivimbe, pia huondoa sumu mwilini. Vinapoungana vitu hivi viwili vya asili vinatengeneza muungano mmoja mhimu wa dawa dhidi ya maambukizi ya nje.
2. NZURI KWA UGONJWA WA MOYO
Chakula sahihi, mazoezi ya viungo, na kuepuka kukaa kwenye kiti masaa mengi ni mhimu kwa ajili ya kuwa na afya nzuri ya moyo.
Kunywa kinywaji chenye asali yenye mdalasini mara kwa mara kunaweza kusaidia kuepuka ugonjwa wa moyo kwa kuzuia kuzibika kwa ateri.
3. INATIBU MAAMBUKIZI KWENYE KIBOFU CHA MKOJO
Asali yenye mdalasini ni dawa bora sana kwa kutibu maambukizi kwenye kibofu cha mkojo na bakteria wowote wanaoweza kushambulia kibofu cha mkojo.
Mchanganyiko huu unasafisha kibofu na kukiacha safi hivyo kukupa mazingira ya kutokuumwa lolote katika kibofu chako cha mkojo.
4. TIBA YA BARIDI YABISI (Arthritis)
Watu wengi wanaripoti matokeo mazuri baada ya siku chache tu za kutumia kinywaji hiki chenye mchanganyiko wa asali yenye mdasini kutwa mara 2.
Ili kutibu baridi yabisi ongeza kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi ndani ya glasi 1 ya maji ya uvuguvugu na unywe nusu glasi kabla ya chakula cha asubuhi na nusu glasi nyingine kabla ya kwenda kulala.
Utafiti huo ulifanyika katika chuo kikuu cha Copenhagen ambako wanafunzi walipewa asali yenye mdalasini ili kutibu baridi yabisi. Baada ya wiki 1 iligundulika kuwa wanafunzi 73 kati ya 200 walikuwa hawaonyeshi dalili tena za ugonjwa huo. Baada ya mwezi mmoja kila mmoja alikuwa amepona na kuwa na uwezo wa kutembea na kufanya kazi.
5. HUTIBU FIZI KUTOA DAMU
Watafiti nchini New Zealand wamegundua kuwa asali mbichi ikichanganywa na mdalasini inaleta ufanisi mkubwa dhidi ya fizi kutokwa damu, kuuma fizi, ganzi kwenye meno na maambukizi mengine katika fizi.
Unaweza kupakaa kwenye mswaki na utumie kama dawa yako ya kusafisha meno ili kupata faida hii.
6. INATIBU MENO YANAYOTOBOKA
Hii kidogo inashangaza. Watafiti katika jiji la New York nchini Marekani wanasema asali inaweza kusababisha meno kutoboka. Hata hivyo wanasayansi wengine nchini New Zealand wanasema asali inaweza kuwa msaada katika kuzuia meno kutoboka kutokana na sifa yake ya kuua bakteria mbalimbali.
Namna rahisi ni kutumia mchanganyiko wa asali yenye mdalasini kama dawa yako ya meno utumie kusafisha meno yako ili kuepuka meno kutoboka na kuoza pia.
7. HUSAIDIA MFUMO WA MMENG'ENYO WA CHAKULA
Husafisha utumbo mpana kwa kuondoa sumu na taka nyingine. Husaidia uzalishwaji wa bakteria wazuri kwenye utumbo mpana na kama matokeo yake huusadia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
8. HUONDOA GESI TUMBONI
Asali yenye mdalasini husaidia kulinda tumbo kwa kufunika kuta za tumbo. Kwa kusafisha mfumo wa bakteria wabaya huwa imesaidia kutibu maambukizi yoyote na hivyo kusaidia kutibu tatizo la tumbo kujaa gesi na asidi.
9. HUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO
Kuna shuhuda nyingi zisizotiliwa shaka juu ya ufanisi wa asali yenye mdalasini katika kupunguza uzito. Asali na mdalasini vinapotumika pamoja, mchanganyiko huo huchoma mafuta kwa haraka sana.
Wakati huo huo mchanganyiko huu hushusha njaa na hivyo kumfanya mtu kujisikia ameshiba muda mrefu.
Angalizo hata hivyo, asali ni tamu na ina nguvu (kalori), hivyo ili kupunguza uzito unashauriwa usitumie zaidi ya vijiko vikubwa vitatu vya mchanganyiko huu ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu kwa siku, Ukizidisha tu unaweza kuongezeka uzito tena.
10. HUONGEZA AKILI
Watu wengi wanaripoti kuwa asali yenye mdalasini inawaongezea uwezo wao wa kukumbuka vitu. Asali yenye mdalasini hongeza uwezo wa ubungo kufanya kazi na kuongeza uwezo wa kumbukumbu.
11. HUTIBU KANSA
Ingawa bado haijathibitishwa kisayansi ni jinsi gani asali yenye mdalasini inatibu kansa lakini uwezo wake wa kuondoa sumu na vimelea vingine vya magonjwa (free radicals) kunaifanya kuwa na sifa hiyo ya kutibu kansa.
Baadhi ya watu wameripoti kupona kansa ya titi na kansa ya utumbo mpana kwa kutumia asali yenye mdalasini.
12. INAONGEZA NGUVU YA MWILI
Asali ina madini na vitamini nyingi ndani yake, wakati mdalasini wenyewe una kalsiamu, chuma, vitamini C, vitamini K, manganizi na nyuzinyuzi (fiber).
Vinapoungana vitu hivi viwili hufanya dawa moja mhimu sana ya kuongeza kinga ya mwili. Kunywa chai yenye asali na mdalasini mara kwa mara kunaongeza kinga ya mwili, nguvu ya mwili na nguvu ya ubongo kwa pamoja.
13. HUTIBU CHUNUSI
Kupakaa asali yenye mdalasini kwenye ngozi yako yenye chunusi kutaondoa chunusi hizo bila kuchelewa. Asali hudhibiti bakteria na mdalasini hudhibiti maambukizi kwenye ngozi na huondoa sumu.
Mchanganganyiko huu husaidia asali kubaki juu ya ngozi kwa muda mrefu na hivyo kufanya uponyaji unaohitajika.
14. HUTIBU KIKOHOZI
Kuinywa asali yenye mdalasini ndani ya glasi ya maji ya uvuguvugu hupunguza vyote kikohozi na kikohozi kikavu. Husafisha msongamano kohoni na kutibu kikohozi cha kawaida na hata kile kikavu.
15. HUZUIA MADHARA YA KUNG'ATWA NA WADUDU
Ni nzuri kwa ajili ya uvimbe au kuondoa maumivu yatokanayo na kuumwa na wadudu. Chukua kijiko kidogo kimoja cha asali na uchanganye ndani ya vijiko vidogo viwili vya maji ongeza na mdalasini ya unga nusu kijiko cha chai na upake juu ya sehemu ulipong’atwa na mdudu.
Maumivu hayo yataondoka mara moja.
16. HUSAIDIA KUOTESHA NYWELE
Changanya kijiko kidogo kimoja cha asali ndani ya ujazo sawa wa mafuta ya zeituni na uongeze kijiko kidogo cha chai tena cha mdalasini ya unga kwenye huo mchanganyiko.
Pakaa mchanganyiko huo kichwani sehemu ambako nywele zimeanza kupotea na uache kwa dakika 15 kisha jisafishe na maji ya uvuguvugu na shampoo ya asili.
17. HUTIBU LEHEMU (Cholesterol)
Matumizi ya mara kwa mara ya asali yenye mdalasini husaidia kupunguza lehemu. Pia husaidia kushusha shinikizo la juu la damu na kusafisha ateri zinazoziba.
Pia kubadili matumizi ya mafuta mengine na kuamua kutumia mafuta ya zeituni kutarahisisha kuweka sawa kolesto yako kirahisi zaidi.
18. HUTIBU MAUMIVU YA JINO
Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha mdalasini ya unga na vijiko vikubwa viwili vya asali mbichi na upake kidogo kidogo juu ya jino linalouma mara kadhaa kwa siku kila siku mpaka maumivu yatakapopotea.
19. HUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI
Changanya kijiko kikubwa kimoja cha asali na kiasi kingine sawa cha mdalasini ya unga ndani ya maji glasi moja ya uvuguvugu na unywe mara tu ukiamka asubuhi.
Hii itakutibu tatizo la harufu mbaya mdomoni na utapumua vizuri bila shida yoyote.
20. HUTIBU UANITHI NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Jaribu na uone tofauti! Changanya vijiko vikubwa vitatu vya asali yenye mdalasini ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvugu na uache mchanganyiko huo kwa dakika 15 hivi.
Kunywa nusu glasi asubuhi kabla ya chakula cha asubuhi na nusu nyingine kabla ya kwenda kulala kwa siku kadhaa hata wiki kadhaa.
21. HUONGEZA KINGA YA MWILI
Ongeza kinga yako ya mwili na magonjwa hayatakugusa. Vyote asali na mdalasini hupigana dhidi ya bakteria na virusi na hivyo kufanya dawa nzuri ya kupigana na kuua bakteria wabaya na virusi.
Asali pia ina madini na vitamini mhimu nyingi hivyo kuupa mwili viinilishe mhimu unaovihitaji.
22. HUTIBU MAFUA
Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali yenye mdalasini ndani ya glasi moja ya maji ya uvuguvgugu kutwa mara moja kila siku kuondoa chafya na kuvimba koo.
23. HUTIBU UGUMBA
Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi. Wapenzi wa jinsia zote wanashauriwa kunywa walau vijiko viwili vya chakula kila siku kabla ya kwenda kulala kila siku.
Mdalasini umetumika miaka mingi katika dawa za kichina na kihindi kuongeza uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa.
24. FAIDA NYINGINE LUKUKI
Kumbuka asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa na watu wamekuwa wakiitumia kutibu magonjwa mengine mengi bila idadi ikiwemo matatizo ya kisukari, kukakamaa kwa miguu na mikono, udhaifu wa jumla wa mwili, kuongeza kumbukumbu, vidonda vya tumbo, kutibu majeraha nk nk
NAMNA YA KUANDAA NA KUITUMIA ASALI YENYE MDALASINI
Kwenye lita 1 ya asali ongeza vijiko vikubwa vitano vya mdalasini ya unga na ukoroge vizuri kabla ya kuutumia. Uhifadhi mchanganyiko huu kwenye bakuli kubwa ili iwe rahisi kuukoroga tena vizuri kila unapotaka kuutumia.
Unaweza kuutumia katika maji au wenyewe kama ulivyo ukipaka juu ya ngozi au ukitumia kwenye vyakula kama mkate na kadharika. Kama utakunywa basi vijiko vikubwa vitatu ndani ya maji ya uvuguvugu glasi moja kwa siku inatosha.
ANGALIZO KUHUSU MDALASINI FEKI:
Kabla sijakuacha, ni mhimu sana nikueleweshe juu ya mdalasini hasa ambao hutumika kama dawa. Siyo kila mdalasini unaouona unaweza kukupa maajabu haya, mwingine ni sumu kabisa mwilini. Na watu wengi hawajuwi hili jambo.
(a) Ceylon cinnamon
Mdalasini ambao hutumika kama dawa hujulikana kwa kitaalamu kama ‘Ceylon cinnamon’ na kwa kawaida wenyewe huuzwa gharama sana. Huwa na radha tamu na harufu ya kuvutia zaidi, unatoka katika nchi ya Sri Lanka katika mmea ujulikanao kama Cinnamon Zeylanicum. Hujulikana pia kama mdalasini wa India.
Huwa na rangi ya kahawia (light brown), mwembamba na mlaini.
(b) Cassia cinnamon
Wakati ule ambao ni feki na ni sumu pia hujulikana kama ‘Cassia cinnamon’ ni mdalasini huu ambao katika baadhi ya nchi umepigwa marufuku kutumika wala kuingizwa nchini mwao. Hujulikana pia kama mdalasini wa China na wengine huuitwa Saigon.
Mdalasini huu unatoka katika nchi za China, Vietnam na Indonesia. Wenyewe huwa una joto zaidi na huwa na radha kali na ya kuwasha ukiutumia. Madhara yake ni pamoja na kudhuru Ini na figo ukitumika kwa kipindi kirefu.
Cassia cinnamon huuzwa bei rahisi sana na mwingi unaopatikana huko masokoni ni huu. Huwa na rangi inayokaribia na uweusi.
Kwa kawaida ni vigumu kutofautisha aina hizi mbili za mdalasini ukishakuwa tayari katika mfumo wa unga tofauti na ukiwa bado katika fimbo au magome. Mhimu ni ununuwe kutoka kwa mtu unayemuamini zaidi.
ANGALIZO KUHUSU ASALI FEKI:
Napenda kukufahamisha kuwa miaka ya karibuni kumejitokeza baadhi ya wafanyabiashara kutengeneza asali feki kwa kutumia maji ya miwa na sukari guru au kuongeza maji na vimiminika vingine ndani ya asali ili wajipatie faida kubwa, endapo utatumia asali ya namna hii basi utakuwa ukiihatarisha afya ya mwili zaidi badala ya kujitibu.
Zifuatazo ni mbinu za kuitambua asali ambayo ni salama kwa maana ya kwamba haijachakachuliwa:
* Weka maji kwenye glasi na kisha mimina asali ndani yake na kwamba ikikaa chini ya glasi bila kuchanganyana na maji basi hiyo ni asali asilia na inakuwa haijachanganywa na chochote.
* Njia ya pili ni kuiweka asali kwenye njiti ya kiberiti na kisha kuiwasha hiyo njiti ya kiberiti, ikiwa njiti hiyo itawaka basi asali haijachakachuliwa kwa kuchanganywa na chochote lakini njiti ya kiberiti isipowaka asali hiyo inakuwa ni feki.
* Njia nyingine ni kuionja bidhaa hiyo na kwamba iliyochakachuliwa kwa kuchemshwa hutoa harufu ya moshi tofauti na ambayo ni halisi (original).


TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU

Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE 

Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya

Comments

 1. Nime kubali sana Dr shuhran tena sana

  ReplyDelete
 2. Asante sn dokta Mungu akubariki sana nitakuja kuchukua mdalasini og

  ReplyDelete
 3. Naomba kuuliza hapo kwny kutest asali ojii na feki imetokea asali imetulia kwny glass hlf kwny kiberiti haikuwaka je itakuw ojii au vp...!?

  ReplyDelete
 4. Na mdalasi ule unatoka tanga - Tanzania na wenye ni nzuri kwa dawa

  ReplyDelete
 5. Dawa ya nguvu za kiume vp asali inatibu au inasaidia

  ReplyDelete

Post a Comment

Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.