Dawa mbadala 16 zinazotibu uvimbe kwenye kizazi (fibroids) haraka Skip to main content

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

Dawa mbadala 16 zinazotibu uvimbe kwenye kizazi (fibroids) harakaUvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama ‘uterine myoma’ au fibroid. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.

Uvimbe huu hutokea katika sehemu mbalimbali juu au ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke.

Ni uvimbe ambao hauhusiani na kansa na unaweza kubadilika rangi ukawa wa njano, unaweza kubadilika ukawa kama maji tu na kurudi tena kuwa mgumu.

Uvimbe kwenye kizazi hujulikana pia kwa majina haya kitaalamu: ‘Uterine fibroids’, ‘Myoma’ au ‘fibromyoma’.

Hujulikana pia kama ‘leiomyoma’ katika lugha ya kidaktari. Wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 50 ndiyo wanapatwa kirahisi zaidi na ugonjwa huu.

Chanzo cha moja kwa moja cha ugonjwa huu bado hakijulikani wazi, hata hivyo baadhi ya sababu za kutokea huu uvimbe ni pamoja na;


1. Kuongezeka sana vichocheo vya progesterone na estrogen kuzidi kiwango mwilini
2. Ujauzito
3. Uzito na unene kupita kiasi
4. Jenetiki zisizo za kawaida
5. Mfumo usio sawa wa mishipa ya damu
6. Sababu za kurithi
7. Lishe isiyo sawa
8. Sumu na taka mbalimbali nk

Dalili zitakazokuonyesha una uvimbe kwenye kizazi ni pamoja na;

1. Kupata damu nyingi wakati wa hedhi
2. Maumivu makala wakati wa siku za hedhi
3. Kuvimba miguu
4. Unaweza kuhisi una ujauzito
5. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
6. Kuhisi kuvimbiwa
7. Kupata haja ndogo kwa taabu
8. Kutokwa na uchafu ukeni
9. Kupata choo kigumu au kufunga choo
10. Maumivu nyuma ya mgongo
11. Maumivu katika miguu ikiwa ni pamoja na miguu kuwaka moto
12. Upungufu wa damu
13. Maumivu ya kichwa
14. Uzazi wa shida
15. Kutopata ujauzito
16. Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo
17. Maumivu ya nyonga
18. Mimba kutoka mara kwa mara (miscarriage)

Aina za Uvimbe kwenye kizazi

Kuna aina kuu nne za Fibroids

1. Intramural: Hutokea kwenye kuta za mji wa mimba (uterus). Wanawake wengi hupatwa na aina hii ya uvimbe.

2. Subserosal fibroids: Hii hukua nje ya kuta za mji wa mimba na hukua na kuwa kubwa sana.

3. Submucosal fibroids: Hutokea kwenye misuli chini ya ngozi laini ya kuta za mji wa uzazi.

4. Cervical fibroids: Hii hujenga kwenye shingo ya tumbo la uzazi (Cervix).

Dawa mbadala 16 zinazotibu uvimbe kwenye kizazi.

Ikiwa mwanamke hapati shida ya namna yo yote katika shughuli zake za kila siku, anaweza asihitaji tiba ya aina yo yote hata kama imegundulika kuwa ana uvimbe wa fibroid.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa mwanamke anapokaribia kukoma hedhi Uvimbe huu hunyauka wenyewe na mara nyingine kutoweka kabisa.

Ikitokea kwamba tiba imekuwa ni ya lazima, anaweza kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji kutokana na hali ilivyo.

Chagua dawa tatu hata nne kati ya hzi na utumie kwa pamoja kwa matokeo mazuri na ya haraka. Tafadhari usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktari, mganga au mtaalamu wako wa afya

1. Kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu ni chanzo kizuri cha vitamini B6, vitamini C, na madini mengine mhimu ambayo husaidia kuweka sawa homoni za kike.

Sifa yake ya kuondoa sumu mwilini husaidia kuondoa uvimbe kwenye kizazi. Kitunguu swaumu pia huzuia kujitokeza kwa uvimbe wa aina yoyote kwenye mji wa mimba (uterus). Tafuna punje 3 za kitunguu swaumu kutwa mara 3.

Kunywa maji glasi moja kila ukimaliza kutafuna kitunguu swaumu kuondoa ukali na harufu mbaya mdomoni.

2. Juisi ya Limau

Moja kati ya dawa nyingine za asili kwa kuondoa uvimbe kwenye kizazi ni juisi ya limau.

Ongeza vijiko vijiko vya juisi (majimaji) ya limau na kijiko kidogo cha unga wa baking soda kwenye glasi ya maji ya uvuguvugu, koroga vizuri na unywe mara mbili kwa siku kwa majuma kadhaa.

3. Tangawizi

Mizizi ya tangawizi ni mizuri sana katika kupunguza maumivu na kuongeza msukumo wa damu.

Andaa chai ya tangawizi (kumbuka ni tangawizi na maji tu, usiweke majani ya chai humo) na unywe kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa majuma kadhaa.

Kwenye hiyo chai tumia asli badala ya sukari kwa matokeo mazuri zaidi. Chai ya tangawizi husaidia kuondoa uvimbe kwenye mirija ya uzazi na kwenye mji wa uzazi kwa ujumla.

4. Mafuta ya zeituni

Moja ya tiba za asili kwa uvimbe kwenye kizazi ni mafuta ya zeituni. Mafuta haya huidhibitihomoni ya estrogen. Unahitaji kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni sambamaba na juisi ya limau asubuhi mapema tumbo likiwa bado tupu.

Unaweza pia kuandaa mafuta ya zeituni kwa kuyapika majani ya mzeituni kama chai ambayo pia husaidia kuongeza kinga ya mwili.

4. Mafuta ya nyonyo

Mafuta ya nyonyo ni mazuri sana kwa kuondoa uvimbe. Weka mafuta ya uvuguvugu ya zeituni kwenye bakuli. Weka kitambaa cha pamba ndani ya hayo mafuta mpaka mafuta yote yanyonywe na yahamie kwenye hicho kitambaa.

Kunja kunja hicho kitambaa na uweke juu ya tumbo ndani ya mfuko wa Rambo na kisha weka chupa yenye maji ya moto juu yake (ilaze) na uache hivyo kwa usiku mmoja.

Endelea na zoezi hili kwa kila siku kwa siku 5 hivi kisha pumzika kwa siku mbili, rudia hivyo hivyo siku tano kisha siku mbili kupumzika.

Ili kuyaona mabadiliko jaribu njia hii kwa wiki tatu hivi.

6. Siki ya tufaa

Katika kutibu uvimbe wowote ambao si uvimbe wa kansa, siki ya tufaa ndiyo namba moja. Unachotakiwa kufanya ni kuchukuwa vijiko viwili vikubwa vya siki ya tufaa na uchanganye na maji glasi moja (robo lita/ml 250) changanya vizuri na unywe.

Fanya hivi kutwa mara moja kwa majuma kadhaa.

Unaweza pia kuchanganya kijiko kimoja cha chai cha baking soda na vijiko viwili vya chai vya siki ya tufaa ndani ya glasi moja ya maji, tikisa vizuri mchanganyiko huo na unywe.

Mhimu – Kamwe usinywe siki ya tufaa ambayo haijapunguzwa makali (kavu kavu) yaani bila kuongezwa maji kidogo.

7. Maziwa

Maziwa yanasaidia kuondoa uvimbe vizuri kabisa. Maziwa huwa na protini ya kutosha. Kwenye glasi moja ya maziwa ya uvuguvugu ongeza kijiko kimoja cha unga wa giligilani (coriander powder) na kijiko kimoja kikubwa cha unga wa binzari.

Tikisa vizuri mchanganyiko huo na unywe yote. Fanya hivi kutwa mara 2 kwa wiki kadhaa.

8. Unga wa Binzari (manjano)

Sifa ya kimatibabu iliyomo kwenye binzari hupigana pia dhidi ya uvimbe kwenye kizazi. Chukua vijiko vikubwa viwili vya unga wa binzari au unga wa mizizi yake na changanya na maji nusu lita, chemsha kama chai kwenye moto kwa dakika 15, ipua na uache kwa dakika 40.

Ikipoa kunywa yote. Fanya hivi kwa wiki kadhaa.

9. Kitunguu maji

Viuaji sumu (antioxidants) vilivyomo kwenye kitunguu husaidia kuondoa uvimbe kwenye kizazi kirahisi zaidi. Kitunguu pia ni mhimu katika kurekebisha na kuweka sawa homoni za kike.

Kwahiyo kupunguza uvimbe anza sasa kutafuna kitunguu maji kibichi kama kilivyo, usikioshe na chumvi wala maji.

Kata nusu kitunguu maji na ule kama kilivyo kila siku kwa wiki kadhaa uvimbe utaondoka na homoni zako zitakaa sawa.

10. Zabibubata (Gooseberry)

Zabibubata ni moja ya dawa mbadala zinazotumika sana dhidi ya matatizo mengi ya ngozi na nywele kwa ujumla. Changanya unga wa zabibubata kijiko kidogo cha chai kimoja na kijiko kidogo kingine cha asali.

Changanya vizuri mchanganyiko huo na ulambe wote. Inashauriwa kutumia dawa hii asubuhi mapema wakati tumbo likiwa tupu.

Ni dawa nzuri sana katika kupunguza ukubwa wa uvimbe wa kwenye kizazi (fibroid tumors).

11. Maharage ya soya (soybeans)

Ili kuondoa dalili za uvimbe kwenye kizazi kula maharage ya soya mara nyingi. Maharage ya soya yana kiinilishe mhimu sana kijulikanacho kama “phytoestrogen” ambacho husaidia kudhibiti usawa wa homoni ya kike ‘estrogen’.

Andaa supu au mchuzi wa maharage ya soya, protini iliyomo kwenye maharage ya soya huzuia kuendelea kukua au kuongezeka kwa uvimbe kwenye kizazi.

12. Yoga na Meditation

Moja ya njia rahisi kabisa ya kuondoa uvimbe kwenye kizazi na kufanya mazoezi maalumu yajulikanayo kama YOGA.

Yoga ni sayansi ya kimatibabu yenye asili ya India na ina zaidi ya mika 5000 tangu ilipoanza kutumika. Haya ni mazoezi maalumu yanayoambatana na utulivu wa nafsi ikihusisha mambo ya kiroho.

Kuelewa namna hasa mazoezi haya yanavyofanyika ona video zake kwenye youtube kwa kubonyeza hapa.

Meditation ni kama Yoga lakini unapomeditate maana yake unajiondoa kwenye mazingira ya kawaida na kubaki peke yako kwa masaa kadhaa katika hali ya utulivu, kama ni kazi unaacha, unaacha pia kukaa na vitu kama simu, computer au kuwa tu karibu na yeyote.

Hii ni mhimu kwa mtu yeyote anayehitaji kuondoa msongo wa mawazo na kuungezea nguvu ubongo upya. Yoga na meditation (utulivu) husaidia kuweka sawa mzunguko wa hedhi na hata kuziweka sawa homoni zako.

13. Samaki

Samakai wana mafuta mhimu sana mwilini yajulikanayo kama omega-3 fatty acid ambayo ni mhimu sana katika kutibu uvimbe kwenye kizazi.

Unahitaji kutumia mara kwa mara samaki wa maji baridi kama samoni (salmon), jodari ( tuna), na samaki wengine wenye minofu wa maji baridi ili kuondoa uvimbe.

14. Asali

Ili kuondoa uvimbe maji katika mirija ya uzazi, asali inaweza kuwa msaada mkubwa kwa kazi hiyo. Changanya juisi ya aloe vera, asali na maji na unywe mchanganyiko huu.

Chukua glasi moja ya maji, ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi na kijiko kikubwa kimoja cha juisi ya mshubiri (fresh aloe vera jusi), tikisa vizuri na unywe mchanganyiko huu.

15. Kiazi sukari (beet) na kitunguu swaumu

Ili kuandaa juisi ya kuondoa uvimbe, saga kiasi kidogo cha viazi sukari freshi na uchanganye pamoja na kijiko kidogo cha chai kimoja cha unga wa kitunguu swaumu.

Changanya mchanganyiko huo vizuri na uongeze kikombe kimoja cha juisi freshi ya karoti, ongeza kijiko kimoja kidogo cha asali, tikisa vizuri na unywe mchanganyiko huu mara kwa mara mpaka utakapopona.

16. Aloe Vera (mshubiri)

Moja kati ya mimea kwa ajili kutibu maradhi mengi katika mwili wa binadamu ni aloe vera au mshubiri kwa kiswahili.

Aloe vera pia hutibu uvimbe wa kwenye kizazi bila shida yoyote. Unachohitaji ni kuchanganya ¼ ya kikombe cha juisi ya aloe vera na kikombe kimoja juisi ya viazi sukari (beet) katika glasi moja.

Ongeza kiasi kidogo cha juisi ya limau na jaza maji ya kutosha kujaza vizuri hiyo glasi. Kunywa glasi moja kutwa mara 1 kwa wiki kadhaa ili kuondoa uvimbe katika kizazi.

Tafadhari Zingatia haya kuwezesha uvimbe kupona haraka

1. Hakikisha una uzito sawa kila mara kulingana na urefu wako.
2. Kula sana mboga za kijani na matunda
3. Fanya mazoezi ya viungo kila mara, mara 4 mapaka 5 kwa wiki
4. Kunywa maji mengi kila siku lita mbili mpaka lita tatu
5. Kula sana vyakula vyenye nyuzi nyuzi (faiba) na punguza vyakula vyenye mafuta
6. Usitumie bidhaa zozote zenye kaffeina (chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote nk), nyama nyekundu na vyakula vya kuchomwa au kupikwa katikati ya mafuta mengi (maandazi, chipsi, nk)
7. Achana kabisa na mawazo mawazo (stress) na hamaki nyingine zozote
8. Acha kuvuta sigara/tumbaku na vilevi vingine vyote hadi hapo utakapopona kabisa


TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU

Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE 

Masomo Mapya >>>>BONYEZA HAPA<<<<<<<<<<Masomo Mapya

Comments

Post a Comment

Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku

Popular posts from this blog

Vyakula 6 vinavyoongeza Nguvu za Kiume Haraka

Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi. Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia " booster" . Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako. Sababu za kukosa nguvu za kiume  Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni

JINSI YA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni kama kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae. Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo " testosterone"  ambapo mwanaume huzalisha  mara 20 zaidi ya mwanamke  anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya. Sasa kimaumbile  mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu  alisema "Wanaume wapendeni wake

Namna Ya Kumfikisha Mwanamke Kileleni Ndani Ya Dakika Tano!

  Ili mwanamke kuweza kufika kileleni anahitaji wastani wa dakika 15-20, ndiyo wanawake wanachelewa kidogo kuliko sisi wanaume. Kuna wanaume wengi hawafikishi hizo dakika katika raundi ya kwanza, wengi hufikisha katika raundi ya pili, hivyo kama wewe huwezi kuunganisha basi unajikuta unamkatisha starehe mwanamek na hafiki kabisa. Lakini kuna wanaume wengi ambao mwisho wao ni raundi moja tu na hapo wanajikuta wamechoka na kulala kabisa. Wengi sana unakuta hiyo raundi moja hata hawafiki dakika kumi na wengine ni mbili mpaka tano. Ni ngumu kidogo kumfikisha mwanamke kwa dakika mbili au tano, ndiyo maana wanaume wa namna hii wengi huishia katika msongo wa mawazo, kuwa na hasira, kujifanya Malaya kwa kuwa na wanawake wengi na visirani vingine vingi kwakua wanadhani wanadharauliwa. Ila huna haja ya kupaniki, unaweza kumfikisha mwanamke kwa hizo hizi dakika mbili au tano, ni ufundi wako tu. ( 1) Acha kisirani muandae kisaikolojia kabla ya tendo;   Najua unadhani kwakua na kisirani laba nd

JINSI YA KUONGEZA UZITO AU UNENE BILA KUDHURU MWILI WAKO

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka kidogo uzito na unene wako kwa ujumla. Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa ujumla. Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala. Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana wenye kupendeza zaidi. Endelea kusoma … NINI MAANA YA KUWA NA UZITO PUNGUFU? Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri. Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au unaweza kusema ni utipwatipwa. BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano m

FAIDA 16 ZA MAJANI YA MPERA

                                    Kati ya mimea yenye faida kubwa katika mwili wa mwanadamu ni tunda la pera ni moja wapo. Majani ya tunda la mpera yakitumiwa vizuri yanaweza kukuletea matokeo ya kushangaza katika nywele hasa kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele na mwili kwa ujumla  Majani ya mpera yana kiwango kikubwa cha Vitamin C, Vitamin A, fiber na potassium. Wanawake wengi wanaopenda urembo wa nywele wamekuwa wakihangaika na ‘steaming’ za bei mbaya kisa tu kujaza nywele kichwani na kuzifanya zisikatike, Wasiokuwa na muda wa saluni na wasiokuwa na hela hizi ni habari njema kwao kwamba majani ya mpera ni mazuri kwa kukuza nywele na kuzitibu zile zinazokatika. Jinsi   ya   kuyatengeneza   kama   dawa  Chukua majani yanayotosha kwenye kiganja chako kisha weka kwenye sufuria yenye lita moja ya maji, chemsha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.  Baada ya hapo, yaache yapoe kisha paka kwenye nywele zako kuanzia kwenye mzizi wa nywele mpaka mwisho.  Ukimaliza fanyia

HAYA NDIYO MAAJABU 24 YA ASALI YENYE MDALASINI ULIKUWA HUYAJUWI BADO

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kwa kutumia asali. Inapotokea dawa za asili mbili zinachanganywa pamoja katika uwiano fulani, hutokea kuundwa dawa nyingine nzuri ambayo ni tiba kwa maradhi mengi sana. Moja kati ya muunganiko wa dawa hizo za kushangaza ni pale asali inapochanganywa na mdalasini. Muunganiko huu umekuwa ukitumika kwa karne nyingi kutibu magonjwa mengi mwilini na kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla. Watu wengi wanakiri maajabu yaliyomo kwenye hii dawa asili ASALI YENYE MDALASINI. Dawa hii ya asili ni maarufu kwa maelfu ya miaka katika tiba asili za China (Traditional Chinese Medicine - TCM), Ugiriki (Unani Medicine), India (ayurvedic) na Mashariki ya kati (The science of medicines based on natural treatment in the East - Tibb). Kwa mjibu wa wataalamu wa

UNGA WA MAJANI YA MLONGE(MORINGA LEAF POWDER) || TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI

  Huimarisha msukumo wa damu, Hudhibiti glucose kwa wenye sukari, Huondoa mashaka na wasiwasi, Huongeza  kinga na nguvu mwilini, Hutibu  kuhara na kuhara damu,  Huondoa  uvimbe kwenye utumbo mwembamba, na Huondoa  vimbe nyingine mwilini, Huongeza  kasi ya utoaji mkojo, Huondoa  matatizo mbalimbali ya moyo. Hutibu homa na kikohoza Unga wa mlonge hutengenezwa kutokana na majani bora ya mti wa mlonge, tumia kijiko cha chai 2 mara 3, kwa wiki 3. MBEGU ZA MLONGE (MORINGA SEEDS) Huondoa vipele kwenye ngozi Huondoa shinikizo la damu Huondoa saratani ya tumbo Huondoa homa za mara kwa mara Hutibu maralia Hupunguza vitambi , kwa wanawake na wanaume Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo Huongeza nguvu za kiume na za kike Huongeza uwezo wa kumbukumbu Hupunguza hasira Hupunguza tatizo la mafua Mbegu nazo huchumwa kutoka katika mti bora wa mloge MAFUTA YA KUPAKAA YA MLONGE Hulainisha ngozi Huondoa uchovu Hutumika kwa wanawake na wanaume kujipaka Huondoa mabaka na mibabuko Huondoa ukurut

FAIDA 12 ZA KULA NDIZI MBIVU

Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.   Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.

Vyakula Kumi(10) Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili. Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa kama vinavyoorodheshwa Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo: 1. Pilipili Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinai

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi. Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote. Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama: *Vyakula feki (Junk food) *Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi *Kutokunywa maji ya kutosha kila siku *Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala *Kukaa masaa mengi kwenye kiti *Kutokujishughulisha na mazo