Ni ukweli kwamba unapokuwa na ngozi yenye asili ya mafuta mengi hukera kwani muda wote uso huonekana kung'aa zaidi hata kama umepaka baadhi ya vipodozi vya kuzuia uso kuwa na mafuta mengi.
Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula ambavyo huweza kusaidia kupunguza hali ya mafuta usoni:-
1. Chungwa
Chungwa na limao huweza kupunguza hali ya mafuta usoni kutokana na matunda hayo kusheheni vitamin C nyingi pamoja na kutoa sumu mwilini na hivyo kutoa mafuta yasiyohitajika mwilini.
2. Mboga za majani
Mboga hizi huwa hazina kiwango cha mafuta, isipokuwa zinautajiri wa nyuzinyuzi (fiber) ambayo huweza kusafisha mafuta kwenye ngozi.
3. Parachichi
Kitu kikubwa kuhusu tunda hili ni kwamba mbali na kuliwa pekee, bali huweza kupakwa moja kwa moja kwenye ngozi na kupunguza kiwango cha mafuta usoni.
4. Ulaji wa vyakula vya nafaka
Vyakula hivi huwa na wingi wa nyuzinyuzi, ambazo husaidia kurekebisha mmeng'enyo wa chakula kuwa vizuri zaidi na kuifanya ngozi kutokuwa na mafuta mengi na hata chunusi pia.
5. Maji ya nazi
Nayo huweza kupunguza hali hiyo kutokana na kurejesha ukavu kwenye ngozi
Kuna vingine vingi ambavyo huweza kupunguza mafuta kwenye ngozi ikiwa ni pamoja na ndizi, broccol, samaki, zabibu na limao
TAZAMA VIDEO HII JINSI YA KUPUNGUZA UZITO
Comments
Post a Comment
Tembelea https://toptenherbs.co.tz/ ili kupata Masomo Mapya Kila siku