Topten Herbs Skip to main content

Posts

Tembelea WEBSITE YETU MPYA

WANAWAKE MLIOOLEWA ZINGATIENI HILI:

Kama mwanamke unasumbuliwa na tatizo la kuwa mkavu wakatu wa tendo, hali inayopelekea kupata maumivu na kutokufurahia tendo basi fuata huo ushauri jaribu kutumia mara kwa mara, itakusaidia kuongeza hamu pamoja na ute. TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE  Masomo Mapya >>>> BONYEZA HAPA <<<<<<<<<<Masomo Mapya

FAIDA USIZOZIJUA KUHUSU PAPAI:

Karibu mpendwa mfuatiliaji wa Topten, huenda mara nyingi umekuwa ukisikia kuwa ulaji wa matunda ni kitu chenye faida nyingi sana mwilini, mara nyingi tulizoea kusikia maneno hayo kutoka kwa madaktari au wataalamu wa afya lakini hivi sasa wimbo huu umekuwa ukiimbwa mpaka na wanasiasa pamoja na viongozi wa Dini pia. Wengi weru tumekuwa tukijua tuu kuwa matunda yanafaida kubwa kiafya lakini huenda tukawa hatujui kuwa ni kwann tunasema tunda fulani ni muhimu sana, Leo napenda kuandika makala hii kuelezea kiundani faida nyingi za kula papai, faida ambazo watu wengi hawajawahi kuzijua kabisa. Baadhi ya sifa hizo ni kama vile 1. Uwezo wa ajabu wa kuzuia mtu asipatwe na Saratani (Cancer): Papai ni katika matunda yanayoingiza afya sana kwenye mwili wa binadamu. Papai lina vitamin C na vitamini A kwa wingi pia kuna potassium na folate. Pia tafiti zinaonesha kuwa antioxidant aina ya lycopene iliyomo kwenye papai husaidia katika kuzuia kupata saratani. 2. Husaidia sana kama dawa ya minyoo. Tunda h

OFA KWA WAFUATILIAJI WANGU:

Mara nyingi nimekuwa nikiandika vitabu mbalimbali vinavyohusu mambo ya kiafya na namna ya kujitibia maradhi tofauti tofauti yanayowasumbua watu, vitabu hivyo vimekuwa ni msaada mkubwa kwa wengi waliobahatika kuvisoma na wengi wao wamekuwa wakijitibia maradhi yanayowasumbua kwa kufuatisha tuu maelekezo yaliyoandikwa katika vitabu hivyo. Leo napenda nitoe OFA  kwa watu ambao wamekuwa wakinifuatilia kwa muda wote huu, hivi sasa kumekuwa na mkanganyiko mkubwa wa kifikra kuhusu jambo la CHANJO, wapo wanaoshauri kuchanja na wapo wanaoshauri kutochanja na huenda kila mmoja akawa sahihi upande wake kwa namna moja ama nyingine. Kutokana na hali hiyo niliamua kukaa chini kuandika kitabu hiki ambacho kimefafanua mambo mbali mbali kuanzi kijamii, kiafya pamoja na kiuchumi kuhusu suala la CHANJO. Kitabu hiki hakijaegemea upande wowote ule wa maoni ya watu bali kimetoa mchanganuo wa pande zote mbili kisha kutoa faida pamoja na hasara za pande zote mbili. Nimeamua kufanya hivyo si kwa lengo la kuhama

IJUE SIKU YA KUBEBA UJAUZITO: PART III

Baada ya kujua jinsi ya kuhesabu mzunguko wako kama nilivyoelezea kwenye part I nasikuu ya kushika ujauzito kama nilivyoelezea kwenye part II ya makala hii basi ni muda wa kujua kuwa je siku za hatari huwa zinakuwa zipo ngapi? Hii naamini itakusaidia sana wewe unaetaka kutumia karenda kama njia ya uzazi wa mpango. Kwanza kabisa  napenda ujue kuwa yai mwanamke huwa linakaa kwenye mji wa uzazi kusubiri mbegu za mwanaume kwa masaa 24 tuu. Baada ya muda huo yai hutengeneza gamba gumu kulizunguka ambapo gamba hilo huzuia mbegu zisiweze kuingia ndani ya yai na kutunga ujauzito. Hivyo baada ya kujua siku ambayo yai litashuka kwenye mji wa uzazi kutoka kwenye ovari kama nilivyoelezea Part II, basi kama yai limeshuka leo basi litakaa leo na kesho tuuu kisha baada ya hapo ujauzito hautaweza kutungwa kwani yai linakuwa limekwishatengeneza gamba gumu na tayari linakuwa limeanza kuharibika taratibu kusubiri mzunguko ujao. Ila mbegu za mwanaume huwa zinaweza kuishi ndani ya via vya uzazi vya mwanamk

IJUE SIKU YA KUBEBA UJAUZITO: PART II

Naamini mpaka sasa utakuwa umekwisha fahamu namna ya kuhesabu na kujua mzunguko wako kama nilivyoelezea Part I ya makala hii. Sasa baada ya kujua mzunguko wako kinachofuata kujua ni suala la siku ya kubeba ujauzito wako kulingana na mzunguko wako. Kwanza kabisa napenda kufuta dhana potofu ambayo imejengeka kwenye vichwa vya watu wengi kuwa siku ya 14 ndiyo siku ya hatari, kama nilivyokwisha tangulia kuelezea hapo awali kuwa mzunguko wa mwanamke mmoja huwa ni tofauti na mwanamke mwingine ijapokuwa wanawake wengi Duniani wana mzunguko wa siku 28 ila hiyo haimaanishi kuwa wote wapo hivyo, kama nilivyokwisha sema wapo wenye mzunguko 27, 29, 21, 35 na kadhalika hivyo endapo mtu mwenye mzunguko wa siku 34 au 25 akisema siku ya hatari ni siku ya 14 basi atakuwa anakosea na huenda akajikuta akishindwa kupata ujauzito kwa kufuata kalenda au akaja kupata ujauzito asioutarajia. Sasa jinsi ya kujua siku ya hatari au siku ya kubeba ujauzito kulingana na mzunguko wako unapaswa kufanya kama ifuatavyo

IJUE SIKU YA KUBEBA UJAUZITO : PART I

Moja kati ya kitu ambacho kimekuwa kikiwasumbua wanawake wengi sana kwa sasa ni jinsi ya kujua mzunguko wao wa hedhi na jinsi ya kujua siku za kubeba ujauzito. Leo napenda kuelezea somo hili kwa kirefu na kwa njia rahisi ambayo mtu yeyote atakayesoma makala ataweza kuelewa, nafanya hivi kwani nimekuwa nikipigiwa simu nyingi sana na watu wanaoshindwa kujua mzunguko wao. Kwanza kabisa napenda kutoa maana ya neno 'mzunguko'. Watu wengi wamekuwa wakichanganya maana ya neno mzunguko na idadi ya siku wanazokuwa kwenye period. Unakuta unamuuliza mtu una mzunguko wa siku ngapi anakwambia siku 3 kumbe anamaanisha idadi ya siku anazokuwa anatokwa na hedhi. Sasa iko hivi, mzunguko ni idadi ya siku zilizopo kati ya period moja na period nyingine yaani ili uweze kujua una mzunguko wa siku ngapi unatakiwa uanze kuhesabu kuanzia siku ya kwanza uliyoona damu mpaka siku moja kabla ya siku utakayoona damu awamu nyingine. Kwamfano mwezi huu umeona damu tarehe 10 tuseme, kisha ukaja tena kuona dam

TATIZO LA MTOTO KUKOSA CHOO:

Tatizo la kukosa choo kwa watoto au kuwa na choo kigumu hasa watoto wadogo limekuwa likiwasumbua wazazi wengi sana miaka ya hivi karibuni. Mara nyingi hali hii hujitokeza pale mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kupewa maziwa ya kopo au pale mtoto anapoanza kula vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama. Mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama pekee huwa hawasumbuliwi na tatizo hili. Leo napenda kuelezea baadhi ya vitu ambavyo unaweza kuvifanya hapo nyumbani na kumsaidia mtoto wako kuondokana na tatizo hilo. 1. Anza kumpatia mtoto wako maji safi, mpe walau kiasi kifo kwa siku kisha uendelee kumuongezea kiasi kadri siku zinavyosonga mbele. 2. Mpatie juisi ya tufaa (Apple) robo glass. Juisi hii huleta matokeo chanya kwa haraka zaidi. 3. Jitahidi kumpatia mwanao vyakula vyenye ufumwele (fiber). Kama mwanao amekwisha anza kula vyakula vigumu basi pendelea zaidi kumpa vyakula vyenye ufumwele kuliko vyakula vya wanga. Vyakula vyenye ufumwele kwa wingi ni kama vile apple, peas na

USIFANYE TENA HIVI:

Kama umepita mitaani naamini utakuwa umeona mara kadhaa wanawake wakiweka pesa katika sidiria zao, Jambo hili limekuwa ni kawaida sana kwa wanawake wajasiriamali na wengi wao huona ni kitu cha kawaida kabisa kwani kimekuwa kikifanyika kwa miaka mingi. Huenda madhara take yasiweze kuonekana moja kwa moja lakini madhara yake huwa ni makubwa hasa endapo mwanamke huyu anaeweka pesa kwa mtindo huu anapokuwa ni mama aayenyonyesha. Kihalisi tabia ya kuweka pesa kwenye sidiria ni hatari sana kwa afya ya mtoto. Najua utakuwa unajiuliza kuwa ni hatari kivipi wakati imekwishazoeleka siku zote?  IKO HIVI: Mara nyingi pesa tunayopokea kutoka kwa mtu huwa hatujui kuwa pesa hiyo imepitia mazingira gani huko ilikotoka na kila mmoja anajinsi ya kuhifadhi pesa anayoijua yeye kulingana na mazingira aliyopo. Kwa mfano, kuna watu wanafanya kazi buchani hivyo pesa zao hu wanavyozihifadhi lazima watashika na mikono yenye damu damu za nyama, wengine ni huhifadhi pesa soksi hasa hasa wanaume, wengine huweka pe

NJIA RAHISI ZAIDI YA KUONDOA KITAMBI

Katika ulimwengu tunaoishi sasa kitambi / au unene uliopita kiasi ni moja ya tatizo linalowatesa watu wengi sana, na hii ni kutokana na vitu mbalimbali kama vile ulaji mbovu wa vyakula na mitindo ya maisha yunayoishi sasa. Ijapokuwa huenda mtu asione madhara yanayoweza kuletwa na kitambi moja kwa moja zaidi ya kutokuwa huru (comfortable) yeye binafsi lakini katika uhalisia basi kaa ukijua kuwa matatizo mengi makubwa ya kiafya ambayo watu hupoteza mamilioni ya pesa katika kutafuta tiba yake asilimia kubwa husababishwa na kitambi au mlundikano wa mafuta ndani ya miili yetu. Kwanza kabisa kabla sijakupa njia rahisi yanayoweza kuitumia kuondoa kitambi basi kwanza naomba nifafanue vizuri kuwa kitambi husababishwa na nini. CHANZO: Kitambi ni mlundikano wa mafuta ambao umekusanyika maeneo ya tumboni, kadri mafuta yanavyozidi kurundikana zaidi ndivyo kitambi kinavyozidi kuwa kikubwa na kuna baadhi ya watu hupelekea baadae kuanza kuongezeka au kuota maziwa (kwa wanaume). Mafuta haya yanatokana

FAIDA 6 USIZOZIJUA ZA MZUGWA/MVUGA.

Dawa hii ni nzuri sana kwa matatizo yote ya mfumo wa uzazi wa mwanamke, Ni dawa ambayo imetumika kwa miongo mingi sana kutibia matatizo mbalimbali ya wanawake. Imethibitiksa kuwa na uwezo wa:-  1. Kusafisha Kizazi. 2. Kuzibua mirija ya uzazi 3. Inatibu kabisa matatizo ya change la uzazi 4. Inapevusha haraka mayai hivo kupelekea mwanamke kuwahi kupata mimba.  5. Inarekebisha mfumo wa homoni wa mwanamke 6. Inarekebisha Mfumo wa hedhi na kutibia maumivu makali wakati wa Hedhi.  MATUMIZI Chukua majani haya yatangwe vizuri kasha loweka ikae kwa masaa 12 kisa mgonjwa anywe kikombe cha cha kutwa mara 3 kwa siku 3 hadi tano. Ni vizuri sana kama mgonjwa atatumia kipindi chake cha hedhi. Lakini kama hapati hedhi basi atumie muda wowote ule. Hivo ni vizuri sana kuyapanda majani haya nyumbani kwako kwa kuwa ni muhimu sana. TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE  Masomo

JINSI YA KUJITIBU KWA KUTUMIA TANGAWIZI:

Tangawizi Ni moja kati ya mimea michache yenye uwezo wa kutibu maradhi mbalimbali kwa wakati mmoja. Kwa miaka na miaka tangawizi imekuwa ikitumika kujitibia maradhi mbalimbali pasipo kwenda hospitali, hata kipindi hospitali za kisasa hazijaanza mababu zetu walikuwa wakiutumia mmea huu na  umekuwa ukileta matokeo chanya kwa kiasi kikubwa sana. Baadhi ya maradhi ambayo hutibiwa kwa kutumia tangawizi ni kama vile: 1. Inatibu kuchelewa kupata siku kwa wasichana (hedhi) pamoja na matatizo ya hedhi kwa ujumla,  2. Husaidia nguvu za kiume. 3. Mafua baridi 4. Matatizo ya tumbo 5. Goita 6. Uvimbe 7. Koo 8. Kuharisha 9. Kupunguza tindikali (Acid) 10. Kipindupindu MATAYARISHO Chemsha, kunywa ikiwa yamoto. Unywe tangawizi mbichi iliyotwangwa kama chai bila sukari. Kikombe kimoja kwa siku, kwa siku 5 TAARIFA MUHIMU KWAKO MSOMAJI WETU Napenda kukujulisha kuwa kwa sasa tumeboresha Zaidi huduma zetu. Tembelea website yetu mpya ili kupata masomo mengine mengi zaidi BURE  Masomo Mapya >>>> B

DAWA YA KUFANYA MACHO KUWA MEUPE

Watu wengi sana wamekuwa kuwa wakisumbuka na tatizo la macho kuwa mekundu au rangi nyingine ambayo wao hawapendezwi nayo na kuna baadhi wamefika mbali zaidi mpaka kufikia hatua ya kubadilisha kiiini cha macho yao na kuweka mboni ya bandi ili tuu wawe na macho meupe. Katika maisha ya mwanadamu hakika hakuna tatizo dogo, ila kitu chochote ambacho kinaweza kumkosesha amani basi kitu hicho hugeuka na kuonekana kuwa ndiyo tatizo. Na hii ndiyo asili ya kila mtu kuna wengine hutumia mamilioni ya pesa kutafuta suluhisho la kitu ambacho mwingine anaona ni kitu kidogo. Hivyo leo nimeamua kuja na somo la jinsi ya kujiandalia dawa ambayo itatibu kabisa tatizo la kuwa na macho mekundu na hatimaye kurudisha macho yako katika asili yake ya weupe.  MAHITAJI: 1. Kabichi nyeupe robo kilo 2. Carrot kubwa nzuri 3  3. Maji safi nusu glass. MAANDALIZI NA MATUMIZI YAKE: Osha vizuri kabichi, kisha kata kata katika vipande vidogo vidogo kiasi.  Chukua karoti, zioshe vizuri kisha kata vipande vidogo vidogo pia.

HARUFU MBAYA KWAPANI:

Je wewe ni mmoja kati ya watu wanaosumbuliwa au kukoseshwa amani na tatizo la kutoa harufu mbaya kwenye kwapa? Endapo unasumbuliwa na tatizo hilo basi amini ya kwamba hauko pekeyako mwenye tatizo hilo na huenda ukawa umekwisha hangaika kwa njia mbalimbali lakini bado hali hiyo inakusumbua. Basi napenda kukuhakikishia ya kwamba kupitia makala hii fupi utaweza kupata suluhisho la tatizo lako. Kwanza kabisa napenda nikwambie ya kwamba kihalisi au kiasili jasho ya binadamu haina harufu yoyote ile. Kinachopelekea harufu siyo jasho lenyewe bali backteria ambao wanapatikana eneo hilo. Kama tujuavyo ya kwamba backeria hupenda kuishi na kuzaliana hasa katika maeneo yenye unyevunyevu hivyo endapo mwili wako hukaa na jasho kwa muda mrefu bila kufutwa basi sehemu hiyo yenye jasho inakuwa ni rafiki kwa backteria. Hao backteria wanapozaliana eneo hilo hutengeneza uchafu (takamwili ya backeria) hivyo uchafu utokanao na backeria hao ndiyo hupelekea harufu ambayo mtu huuiskia. Kwa maana hiyo njia bora

NI KWANINI UJAUZITO UNAHARIBIKA?

Hilo ni moja ya maswali ambayo wanandoa hujiuliza mara kwa mara, hasa wale ambao wametafuta mtoto kwa muda mrefu lakini kila mwanamke akifanikiwa kushika ujauzito basi baada ya muda mfupi au miezi kadhaa ujauzito huo hutoka. Kwa hakika jambo hilo limekuwa likiwasumbua na kuwaumiza watu wengi sanaa kwani anakuwa ameshajiandaa kisaikolojia kuwa hivi karibuni ataitwa baba au mama lakini ghafla ndoto yake inafutika. Kwa utafiti inaonesha kati ya ndoa 40 basi ndoa 10 hukumbana na tatizo la kukosa mtoto au ujauzito kutoka, ni jambo lenye kuumiza kwa hakika. Mara nyingi tatizo kama hili liikitokea basi kwa watu wasio na uelewa huanza kulaumiana wakihisi ni uzembe wa mwenzake nakadhalika. Kiukweli zipo sababu mbalimbali zinazoweza kupelekea ujauzito kutoka lakini leo napenda kuelezea sababu ambayo ni kubwa sana inayopelekea hali hiyo. Kwanza kabisa inatakiwa ujue kuwa ili ujauzito uweze kutungwa na hatimaye mtoto mwenye afya aweze kuzaliwa basi inatakiwa damu ya mwanaume na damu ya mwanamke zi

JINSI SIGARA INAVYOLETA KANSA

Kemikali za sumu zilizoko katika tumbaku ya sigara huharibu DNA za mwili wa binadamu dakika chache tu baada ya mtu kuanza kuvuta sigara. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, kemikali hizo zinazoitwa Polycylic Aromatic Hydrocarbons (PAHs) husababisha DNA ziharibike na kuongeza uwezekano wa mtu kupata kensa. Katika uchunguzi huo watalamu walichukua kemikali hizo katika miili ya wavuta sigara na kuzifanyia uchunguzi, ambapo waligundua kuwa, kemikali za PHA hubadilika haraka mwilini na kuwa sumu ambayo huharibu DNA baada ya kupita dakika 15 hadi 30 tangu kuingia tumbaku katika mwili wa binadamu. Sumu hiyo hubadilisha seli mwilini au kufanya mutation, kitendo ambacho huweza kusababisha kensa. Wataalamu hao wanasema, kitendo hicho hufanyika kwa haraka sana kama vile inavyoingizwa mada ya sumu kwenye damu kwa sindano. Habari hii ni tahadhari kwa watu wanaotaka kuanza kuvuta sigara, kwani takwimu zinatuonyesha kwamba, watu 3,000 hufariki dunia kila siku umwenguni kutokana na kensa y